1. Kuhusu gharika ya Nuhu kwa watu walioasi ni kweli Qur'an inasema gharika ilitokea, lakini hakuna sehemu inasema ilitokea Dunia nzima.
"And We saved him from the people who denied Our signs. Indeed, they were a people of evil, so We drowned them, all together." (Quran 7:64)
2. Kuhusu mwezi ku_split katikati ni kweli Qur'an inasema mwezi ulipasuka na hili tukio hata Wanasayansi mbalimbali wame prove, ukitaka nenda YouTube video zipo:-
Al-Qamar 54:1
"The Hour has come near, and the moon has split [in two].[1]"
3. Kuhusu jua Qur'an haisemi kwamba Eti Jua linazama kwenye matope, bali Qur'an inasema hivi kuhusu Jua:-👇🏽
Qur'an 21:33 {"And it is He who created the night and the day and the sun and the moon; all [of them] swim along in an orbit."}
Hiyo Aya ya Surah Kahf uliyosema haihusiani na kuzama kwa jua bali yenyewe inazungumzia jinsi Dhul-Qarnayn alivyoona kadri ya upeo wa macho yake Al-Kahf 18:86 {Until, when he reached the setting of the sun [i.e., the west], he found it [as if] setting in a body of dark water,[1] and he found near it a people. We [i.e., Allāh] said, "O Dhul-Qarnayn, either you punish [them] or else adopt among them [a way of] goodness."}
Mkuu Nadhani nimejaribu kujibu madai yako dhidi ya Qur'an, ukiwa na doubts siku hizi elimu imerahisishwa unaipata kijanjani tu,..... Soma Qur'an mwenyewe apps zipo nyingi, Ingia kwenye online sources YouTube, ChatGPT ukiwa free thinker naamini utaelimika fresh tu.
Nnavyo jua mimi iwe kisayansi au kiimani ya kikristo ambayo msingi wake ni biblia, enzi ya hapo zamani binadamu hawakuwa wamesambaa dunia nzima, it's like walikuwa ni wachache sana.
Mfano wa Kibiblia : Kipindi wanadamu wanajenga Mnara katika mji wa Babeli (Iraq ya leo) alafu Mungu alivoshuka na kuuangusha huo mnara na akavuruga lugha yao na kuwatawanya duniani kote, Biblia inaendelea kusema kuwa hapo ndipo mwanzo wa lugha nyingi kuzaliwa duniani na wanadamu kutawanywa sehemu zingine za dunia.
So, kwa mujibu wa Bible huo ni ushahidi tosha kuwa kipindi wanadamu walikuwa wamekusanyika hapo Babeli na kuujenga huo mji, walikuwa hawajatapakaa sehemu zingine za dunia bado mpaka Mungu alivyoamua kuwatawanya kwa kuangusha mnara wao na kuvuruga lugha yao ili wasielewane wasiwe na umoja tena.
Mfano mwingine hapa ni kuwa, kwa mujibu
wa wanathiolojia kipindi cha gharika ya NUHU dunia ilikuwa na watu almost laki sita tu, na baada ya gharika walibaki watu 8 tu alafu badae dunia ikaja kujazwa kwa hao watu 8.
So, kama mpaka kipindi cha gharika dunia ilikuwa na watu laki 6, sidhani kama watu hawa walikuwa wametapakaa dunia nzima, nadhani walikuwa katika eneo flani tu wakiishi kama jamii flani yenye utamaduni mmoja.
Na ushahidi wa hilo wanasema, kabla ya gharika NUHU alihubiri kuhusu hiyo gharika kwa miaka 40 kabla ya gharika akiwaonya wanadamu kuhusu Mungu atakavyoleta gharika iwapo hawatatubu, so unataka kunambia NUHU alizunguka dunia nzima kuwahubiria watu kuhusu hiyo gharika ? Hapo nadhani wanadamu walikuwa wako eneo flani tu la dunia, hasa MESOPOTAMIA (Iraq,Syria na uturuki ya leo).
Mfano wa kisayansi na kihistoria: Tafti zinaonesha Archeology zinaonesha kuwa ULAYA imeanza kukaliwa na watu miaka kama laki na nusu tu iliyopita, alafu Latin America ndiyo ilikuwa bara la mwisho duniani kukaliwa na watu (means chini ya miaka laki moja labda iliyopita), na muda huo huo inaonesha Africa ilishaanza kukaliwa na watu miaka zaidi ya milioni 3 iliyopita.
Ushahidi huu wa kuwa africa imeanza kukaliwa na watu kale zaidi upo Ethiopia,Sudan,Tanzania (olduvai Gorge) na South Africa, Zimbabwe pia.
So,.hizi ni ishara tosha kuwa hapo kale binadamu walikuwa hajatapakaa dunia nzima, na kama ni hivo sidhani kama GHARIKA YA kipindi cha NUHU iliifunika dunia nzima kwa maji.