Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Hivi upo serious unaamini nyoka aliongea na mtu akamwambia kula tunda ama, haya huyo nyoka alikuwaje maana naandiko yanasema alilaaniwa kwa kutambaa, so alikuwa na miguu au.. in short hizi story ni za mababu wakijaribu kuelewa mwanzo wa dunia. Ila in short sio hata original maana Gilgamesh story ni Kama hiyo na ni ya zamani kabla ya Biblia kuandikwa..so imeigwa .soma historia uelewe
Ngoja nijaribu kukujibu kidogo kuhusu Biblia.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia ni kwamba, Adam na Hawa pale bustanini walikuwa wanaishi pamoja kwa amani bila shida yeyote kabisa hata SIMBA n.k.

Na pia Adam,Hawa pamoja wanyama kabla hawajatenda dhambi walikuwa wanaelewana kabisa kwa lugha na walikuwa marafiki kiasi kwamba walikuwa wanweza kukaa hata na simba na kumchezea tu kama paka na hawang'ati.

Kwa hiyo hata nyoka walikuwa wanaweza kuongea na kuelewana kabisa lugha na Adam na Eva.

kilichotokea ni kwamba kwa sababu SHETANI ni kiumbe wa kiroho haonekani kimwili ili akaongee na Adam au Eva ilibidi apate auingie mwili wa kiumbe kimojawapo ili atimize azma yake.

Alichofanya shetani ni alimtafta kiumbe mjanja mjanja (mwerevu) kati ya wale aliowaumba Mungu na akaona nyoka ndiyo anafaa.

Hivyo shetani akaamua kumwingia nyoka alafu ndo akaenda kwa Eva kumdanganya hicho alichofanya na akafanikiwa kumdanganya.

Baada tu ya kula lile tunda waliloambiwa wasile, kila kitu kiliharibika kuanzia hapo.

Kwanza Adam na Hawa wakanza kuwa maadui na wanyama hapo hapo, simba akimwona akataka amle,akawa anaanza kuchoka,kutoka jasho,ardhi kuota mbigiri n.k

Hiyo ni kwa ufupi ila kuna Mengi kuhusu hapo dhambini
 
Unawajua Kasuku?

Elimu bahari mzee..... Hata tusome vipi hatutofikia stage tujue kila kitu, kama umekiri kwamba Viumbe wanawasiliana basi fahamu pia hata Ujuzi wa Lugha zao na jinsi wanavyofanya mawasiliano upo,... Ila Mimi na wewe ndiyo hatuna.
Kasuku nishawafuga. Wao wanaongea kwa kuiga sauti... wanaiga saut za ndege wengine, mbwa nk... ila huwez kuongea nae mkaelewena wala wao hawaongei lugha ya binadamu wakaelewana. Ni sawa ww ubweke kama mbwa... mbwa hawez kukuelewa
 
Ngoja nijaribu kukujibu kidogo kuhusu Biblia.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia ni kwamba, Adam na Hawa pale bustanini walikuwa wanaishi pamoja kwa amani bila shida yeyote kabisa hata SIMBA n.k.

Na pia Adam,Hawa pamoja wanyama kabla hawajatenda dhambi walikuwa wanaelewana kabisa kwa lugha na walikuwa marafiki kiasi kwamba walikuwa wanweza kukaa hata na simba na kumchezea tu kama paka na hawang'ati.

Kwa hiyo hata nyoka walikuwa wanaweza kuongea na kuelewana kabisa lugha na Adam na Eva.

kilichotokea ni kwamba kwa sababu SHETANI ni kiumbe wa kiroho haonekani kimwili ili akaongee na Adam au Eva ilibidi apate auingie mwili wa kiumbe kimojawapo ili atimize azma yake.

Alichofanya shetani ni alimtafta kiumbe mjanja mjanja (mwerevu) kati ya wale aliowaumba Mungu na akaona nyoka ndiyo anafaa.

Hivyo shetani akaamua kumwingia nyoka alafu ndo akaenda kwa Eva kumdanganya hicho alichofanya na akafanikiwa kumdanganya.

Baada tu ya kula lile tunda waliloambiwa wasile, kila kitu kiliharibika kuanzia hapo.

Kwanza Adam na Hawa wakanza kuwa maadui na wanyama hapo hapo, simba akimwona akataka amle,akawa anaanza kuchoka,kutoka jasho,ardhi kuota mbigiri n.k

Hiyo ni kwa ufupi ila kuna Mengi kuhusu hapo dhambini
Mkuu. Adam,Hawa na hao wanyama walikuwa wakiongea lugha gani?
Nalog off
 
Wanasayansi wamesema kitu gani kuhusu Origin of Human beings na viumbe wengine,.... Scientific theories zinazoelezea Origin ya viumbe ukizichunguza utagundua ni uongo.

Ngoja nikuulize swali,..... Unahisi kila kiumbe kinaonekana kwa macho?

Kama kuna viumbe kama viruses, Prions, Mycoplasma,archaea na kadhalika, ambao miaka na miaka imepita kabla ya kugundulika kwa Microscope ulikua mtu huwezi kuwaona kwa macho ya kawaida,... Vipi unashangaa kuhusu majini?

Majini(Spirits) ni Viumbe wameumbwa kwa moto(smokeless and scorching fire)

Hivyo basi, sisi kushindwa kuwaona majini kwa macho haimaanishi kwamba hawapo.

Kumbuka miaka 5000 iliyopita,..... Mtu angekuja akasema kuhusu ishu za Blackholes angeonekana kichaa.

Hivyo tufahamu tu kwamba elimu ni bahari,.... Inasemekana Wapo wajuzi wa mambo wanamiliki mpaka majini Tembea uone au jaribu kufanya research kuliko kubisha tu.
Lakini mfano wako wa majini ni dhaifu kinoma. Coz huwezi kuwaona, na hutakuja kuwaona....tuna microscope za kuona electron...tuna telescope za kuona nyota za light years away. Hamna kitu Kama majini. Na magonjwa zamani yalikuwepo watu walijua mapepo majini na Nini Ila baada ya technology ndo ikaja germ theory watu wakajua kuhusu bacteria na Nini ndo maana wakaanza kutoana mapepo wakatengeneza dawa. Mtu kusema kitu hukioni kwa macho kwa hiyo kuamini tu unajua vitu vingapi mtu anaweza kutunga hivi. Haya Babu Christmas nae si haonekani je yupo. Ma vampires wapo, farasi wanaopaa je, Fairies, in short kwa Nini kitu kifichwe Kama kipo duniani. Na hamna theory ya uwongo kwa sababu Kuna evidence nyingi za evolution kuliko viumbe vyako vya Moto. Nikikuuliza evidence utaleta hekaya zako... Evidence za evolution zipo kibao museum tofauti ukitaka hata wewe nenda kafanye research ukaone sio unakaa nyumbani huna hiki Wala kile unasema wanasayansi waongo wakati wao wanafanya juu chini kila siku kuwaondoa nyie ujinga.
 
Ngoja nijaribu kukujibu kidogo kuhusu Biblia.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia ni kwamba, Adam na Hawa pale bustanini walikuwa wanaishi pamoja kwa amani bila shida yeyote kabisa hata SIMBA n.k.

Na pia Adam,Hawa pamoja wanyama kabla hawajatenda dhambi walikuwa wanaelewana kabisa kwa lugha na walikuwa marafiki kiasi kwamba walikuwa wanweza kukaa hata na simba na kumchezea tu kama paka na hawang'ati.

Kwa hiyo hata nyoka walikuwa wanaweza kuongea na kuelewana kabisa lugha na Adam na Eva.

kilichotokea ni kwamba kwa sababu SHETANI ni kiumbe wa kiroho haonekani kimwili ili akaongee na Adam au Eva ilibidi apate auingie mwili wa kiumbe kimojawapo ili atimize azma yake.

Alichofanya shetani ni alimtafta kiumbe mjanja mjanja (mwerevu) kati ya wale aliowaumba Mungu na akaona nyoka ndiyo anafaa.

Hivyo shetani akaamua kumwingia nyoka alafu ndo akaenda kwa Eva kumdanganya hicho alichofanya na akafanikiwa kumdanganya.

Baada tu ya kula lile tunda waliloambiwa wasile, kila kitu kiliharibika kuanzia hapo.

Kwanza Adam na Hawa wakanza kuwa maadui na wanyama hapo hapo, simba akimwona akataka amle,akawa anaanza kuchoka,kutoka jasho,ardhi kuota mbigiri n.k

Hiyo ni kwa ufupi ila kuna Mengi kuhusu hapo dhambini
Hahaha... Okay kwa mujibu ya story hii hii Kati ya Mungu na shetani nani muongo. Mungu aliyewaambia siku hio hio mtakufa mkila au Shetani aliyewaambia mtakuwa Kama Mungu. In fact shetani kasema kweli coz baada ya hapo tumetengeneza maendeleo mpaka hatuhitaji Tena huyo Mungu. Kama ni mawinguni tushapita tumeenda mpaka mwezini Kama ni magonjwa sio mapepo ni vijidudu tuna dawa zake. Tuna maisha Bora saa hivi kuliko mtu yoyote kwenye Biblia hata mfalme. Sasa Nani muongo. Kwani walikufa pale au, Ila najua watasema hoo Mungu anajua yote sijui hajigeuki sijui ni Kama tu ile story ya punda anayeongea....yaani Biblia inabidi wahadithiwe watoto wa miaka 5 ndo maana mnafundishwa tokea utotoni ili ikukae kichwani ukubali uongo wote ukija kukua tayari ushapumbazwa...na ni ngumu Sana kutoka
 
Trump alivokuwa madarakani alisema mwaka 2020 atawarudisha wamarekani mwezini, lakini mpaka ametoka madarakani hakufanya.

NASA wenyewe wakaja wakasema wamesogeza mbele from 2020 to 2022 kwa sababu mambo flani flani ya kiufundi hayajaenda sawa lakini bado 2022 hawakufanya tena.

Wakaja wakasogeza tena hadi 2024, ndo tunasubiri wakifanya kweli basi tutaamini 1969 walienda siyo maigizo.

Ila wasipofanya, tutaanza kuamini huko nyuma walikuwa wanafanya HOLY WOOD.
Mkuu mbona mwezini ni vitu vidogo sana kwa NASA sema tu hizo propagandas ni chuki binafsi tu...Wakienda warusi mwezini basi ni kweli ila wakienda wamarekani basi ni movie za Hollywood🤣🤣🤣🤣🤣
Anajisahaulisha... wayahudi wenyewe wengi sio wakristo. ...shida wakristo tumeiba dini za watu na kuchanganya na ya kwetu ndo maana kila siku madhehebu yanaanzishwa coz hatueleweki
Ukrsto ni tawi la dini ya kiyahudi na ndio maana ni rahisi kwa wayahudi kua wakrsto kuliko dini nyingine yoyote.Hajisaulishi ila kwa asilimia 75% yupo sahii nilikua namkumbusha tu.....Huwezi kuutenganisha uyahudi na ukrsto sababu mafunzo ya imani ya kikrsto yametokana na mapokeo ya imani ya kiyahudi.
 
Hahaha... Okay kwa mujibu ya story hii hii Kati ya Mungu na shetani nani muongo. Mungu aliyewaambia siku hio hio mtakufa mkila au Shetani aliyewaambia mtakuwa Kama Mungu. In fact shetani kasema kweli coz baada ya hapo tumetengeneza maendeleo mpaka hatuhitaji Tena huyo Mungu. Kama ni mawinguni tushapita tumeenda mpaka mwezini Kama ni magonjwa sio mapepo ni vijidudu tuna dawa zake. Tuna maisha Bora saa hivi kuliko mtu yoyote kwenye Biblia hata mfalme. Sasa Nani muongo. Kwani walikufa pale au, Ila najua watasema hoo Mungu anajua yote sijui hajigeuki sijui ni Kama tu ile story ya punda anayeongea....yaani Biblia inabidi wahadithiwe watoto wa miaka 5 ndo maana mnafundishwa tokea utotoni ili ikukae kichwani ukubali uongo wote ukija kukua tayari ushapumbazwa...na ni ngumu Sana kutoka
By the way ukiisoma Biblia kitabu cha MWANZO hasa mazingaombwe ya pale Eden utagundua kwamba "Shetani hakuwa amedanganya ila aliusema ukweli ambao Mungu hakutaka Adam na Eva waujue"

Nasema shetani alisema ukweli kwa sababu aliwaambia hivi "siku mkila matunda ya mti huu na nyie mtafunguliwa macho na kuwa kama yeye mkijua Mema na mabaya"

Na kweli mbeleni ukiendelea kusoma inaonesha kuwa walipokula kula tu tunda kuna ufahamu uliwajia ambao hawakuwa nao, mfano pale pale wakajijua kuwa wako uchi wakaanza kujificha.

Lakini kwa Mungu kitendo alichofanya shetani kilikuwa ni uovu maana aliwasanua kina Adam na Eva kitu ambacho yeye Mungu hakutaka wajua, na madhara yake ndo mashida kibao yalianzia pale na kumiminiwa malaana kibao.

Lakini pia kusema Mungu alisema "wakila matunda ya mtu huo watakufa pale pale " sidhani kama ilimaanishwa ndo pale pale wafe as if tunda walilokula ilikuwa sumu ya kuua on the sport.

Aliiwambia tu siku mkila mtakufa.

Kumbuka tu kuwa lengo la awali la Mungu alimuumba Mwanadamu ili aishi milele, ila kifo kilikuja kama ajali tu baada ya Adam kushindwa kutii sheria ya Mungu.

NB : Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa biblia ina stori ambazo zinaweza kukukanganya, so hayo ni kwa mujibu wa mafundisho ya bible siyo mimi
 
Mkuu mbona mwezini ni vitu vidogo sana kwa NASA sema tu hizo propagandas ni chuki binafsi tu...Wakienda warusi mwezini basi ni kweli ila wakienda wamarekani basi ni movie za Hollywood🤣🤣🤣🤣🤣

Ukrsto ni tawi la dini ya kiyahudi na ndio maana ni rahisi kwa wayahudi kua wakrsto kuliko dini nyingine yoyote.Hajisaulishi ila kwa asilimia 75% yupo sahii nilikua namkumbusha tu.....Huwezi kuutenganisha uyahudi na ukrsto sababu mafunzo ya imani ya kikrsto yametokana na mapokeo ya imani ya kiyahudi.
Sawa basi mi Ni viking naamini Thor yaishe
 
Watakatifu wetu wanawaita mizimu/mashetani wakati huo huo wakaja na mizimu/mashetani yao wakatuambia ni watakatifu wakina yesu,,, mtume Mohamed,,,wakina petro,,paulo,,yakobo nk nk hao wote ni mizimu tu tunayoiomba kwa kuwa ni wafu tuu kama mababu zetu!!
Inasikitisha sana kwa kweli,tunadharau vya kwetu na kuviona bora vya kwao.
Léo hii ukiomba kwa kutumia majina ya mababu zetu eti ni kufuru.
Mfano wa maombi: Mzee Ncheji nimekuja kwako uniongoze na unipe ufahamu.
Eti ni kosa!😇
Ila kutumia majina ya mizimu ya kiarabu na kiyahudi eti ni thawabu 😂😂😂
Kwa jina la Yesu pepo toka (wakristo)
Inna Allaha wa malaikatu swallu ala nabii,yaa ayuhaladhina amanu swallu alaiyhi taslima.
Allahuma swali ala Muhammad,wa aliy Muhammad,kama swalaita ala Ibrahim wa ala aliy Ibrahim(waislamu hii ni lazima kuitaja ktk kila swala,usiwataja hao jamaa basi swala huna 😂)
Nalog off
 
By the way ukiisoma Biblia kitabu cha MWANZO hasa mazingaombwe ya pale Eden utagundua kwamba "Shetani hakuwa amedanganya ila aliusema ukweli ambao Mungu hakutaka Adam na Eva waujue"

Nasema shetani alisema ukweli kwa sababu aliwaambia hivi "siku mkila matunda ya mti huu na nyie mtafunguliwa macho na kuwa kama yeye mkijua Mema na mabaya"

Na kweli mbeleni ukiendelea kusoma inaonesha kuwa walipokula kula tu tunda kuna ufahamu uliwajia ambao hawakuwa nao, mfano pale pale wakajijua kuwa wako uchi wakaanza kujificha.

Lakini kwa Mungu kitendo alichofanya shetani kilikuwa ni uovu maana aliwasanua kina Adam na Eva kitu ambacho yeye Mungu hakutaka wajua, na madhara yake ndo mashida kibao yalianzia pale na kumiminiwa malaana kibao.

Lakini pia kusema Mungu alisema "wakila matunda ya mtu huo watakufa pale pale " sidhani kama ilimaanishwa ndo pale pale wafe as if tunda walilokula ilikuwa sumu ya kuua on the sport.

Aliiwambia tu siku mkila mtakufa.

Kumbuka tu kuwa lengo la awali la Mungu alimuumba Mwanadamu ili aishi milele, ila kifo kilikuja kama ajali tu baada ya Adam kushindwa kutii sheria ya Mungu.

NB : Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa biblia ina stori ambazo zinaweza kukukanganya, so hayo ni kwa mujibu wa mafundisho ya bible siyo mimi
Okay. Kasoma story ya Pandora's box, ni ya wagiriki way before hii ya wayahudi. Miungu ilimwambia asifungue box la zawadi Ila huyo Pandora ambae ni mwanamke hakutii akafungua na ndo hivyo matatizo duniani yakaje. Hizi story sio historia ndo maana hata mashuleni kwenye historia huwezi fundishwa chochote kinachohusu hadithi za Biblia.. hizi Ni story za watu kutafuta jinsi ya kumlaumu mwanamke wa sababu alikuwa dhaifu kipindi hicho na kumtungia story za kwamba ye ndo alisababisha yote. Matokeo yake ndo haya wanawake kuonekana duni. Hii Ni product ya society na sio Mungu jamani. Epic of Gilgamesh hivyo hivyo Kuna mwanamke sijui nyoka sijui tunda, hizi story zipo kabla ya wayahudi na inasemekana wayahudi wameedit waje na ya kwao... Hata mababu zetu wanastory zao hizi zinakuwaga origin myths. Sio historia kweli, shida zilikuwepo duniani, hamna mtu alitakiwa kuishi milele, nature has always been the way it is. Ndo maana hayo maajabu ya Biblia hatuyaoni saa hivi kwa sababu ni story tu..we unadhani mtu angeandika Biblia saa hivi itakuwa the same Kama kipindi kile ambacho watu hawana ujuzi wa Mambo mengi, the answer is no, kulikuwa hamna cameras hamna chochote ndo maana uwongo mwingi. Leo hii nyoka gani anaongea, malkia mwenye panga sijui la moto bwana story za watoto hizi
 
Vp kuhusu holy quran mkuu???
 
Vp kuhusu holy quran mkuu???
Sasa si imebeba story zile zile za wayahudi na ikawabambikiza wote walikuwa waislamu so ni Mitume wao...haijabadilisha kitu...Adam na Hawa ni ujinga ule ule, Musa cjui ule ule. Mambo ya Nuhu na safina vile vile. Wameedit edit tu yaani bana ee hizi story jamani me nawaambia...
 
Lakini mfano wako wa majini ni dhaifu kinoma. Coz huwezi kuwaona, na hutakuja kuwaona....tuna microscope za kuona electron...tuna telescope za kuona nyota za light years away. Hamna kitu Kama majini. Na magonjwa zamani yalikuwepo watu walijua mapepo majini na Nini Ila baada ya technology ndo ikaja germ theory watu wakajua kuhusu bacteria na Nini ndo maana wakaanza kutoana mapepo wakatengeneza dawa. Mtu kusema kitu hukioni kwa macho kwa hiyo kuamini tu unajua vitu vingapi mtu anaweza kutunga hivi. Haya Babu Christmas nae si haonekani je yupo. Ma vampires wapo, farasi wanaopaa je, Fairies, in short kwa Nini kitu kifichwe Kama kipo duniani. Na hamna theory ya uwongo kwa sababu Kuna evidence nyingi za evolution kuliko viumbe vyako vya Moto. Nikikuuliza evidence utaleta hekaya zako... Evidence za evolution zipo kibao museum tofauti ukitaka hata wewe nenda kafanye research ukaone sio unakaa nyumbani huna hiki Wala kile unasema wanasayansi waongo wakati wao wanafanya juu chini kila siku kuwaondoa nyie ujinga.
Mkuu, Jinsi majini walivyoumbwa hatuwezi kuwaona kwa macho, labda wabadilike kwenda kwenye form ya kiumbe mwingine( kumbuka Jini Jinsi walivyoumbwa wanaweza kuingia hadi kwenye mwili wa mtu)... Lakini nadhani watu kama Mkuu Rakims anaweza akakupa elimu kidogo juu ya majini.

Kuhusu majini sema kwamba huna elimu kuhusu wao, lakini usilazimishe kwamba hawapo, ndiyo maana nikakuambia jaribu kufanya research kuhusu majini... Mimi ukiniambia nikuletee Jini umuone sitoweza lakini hiyo haimaanishi hawapo... That's why nikasema elimu ndiyo limitation yetu ya kujua mambo mengi mtu angekuja miaka 5000 iliyopita akasema kuhusu ishu za Blackholes ungemuona kichaa kwasababu elimu hiyo huna.

Hakuna Evidence yoyote ya Evolution.... Mfano unaweza kuthibitisha kwamba Mtu wa kwanza alikua Sokwe? Unaweza kuthibitisha kwamba Mtu ashawahi kuwa na mkia?
 
Sasa si imebeba story zile zile za wayahudi na ikawabambikiza wote walikuwa waislamu so ni Mitume wao...haijabadilisha kitu...Adam na Hawa ni ujinga ule ule, Musa cjui ule ule. Mambo ya Nuhu na safina vile vile. Wameedit edit tu yaani bana ee hizi story jamani me nawaambia...
Ooh hapo sawa mkuu nimekuelewa
 
Wakuu poleni kwa upambanaji.

Binafsi mimi kuna mda huwa nikitulizaga kichwa changu huwa naanza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu mimi (binadamu) na ulimwengu kiujumla (Universe).

Maswali kama sisi (binadamu) ni kina nani,tumetoka wapi asili yetu, kwanini tupo (dhumuni la kuishi), mwisho wetu ama hatima yetu ni nini, Ulimwengu wa vitu je kama sayari, nyota, galaxies zimekuwepo vipi na nini hasa mwisho wake.

Hapo juu ni baadhi tu ya maswali ambayo huwa naiuliza sana akili yangu ikiwaga katika hali ya utulivu.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba, katika maswali yote hayo ambayo huwa najiuliza, sijawahi kupata jibu la uhakika kuniridhisha kuhusu hayo maswali yangu.

Nimekuwa nikifanya bidii kubwa sana kupata majibu ya maswali yangu kupitia usomaji wa majarida au vitabu vihusuvyo historia,sayansi, dini na Falsafa lakini kote bado sijapata majibu ya kuniridhisha tofauti na kuambulia majibu ya kinadharia tu ambayo yana strength kiasi chake lakini pia yana weakness sehemu nyingi tu.

Na nikiri wazi tu kuwa katika usomaji wangu wa nadharia hizo zote (historia, sayansi, dini, falsafa) sehemu ambayo nimeanza kuiamini kunipa majibu ya maswali yangu ni kwenye DINI.

Nikiwa na maana nimeanza kuamini kwamba uwepo na sisi tuliohai na visivyo hai hapa ulimwenguni ni matokea ya Uumbaji ya nguvu kubwa sana inayoitwa MUNGU/ALLAH kama ambavyo dini nyingi zinaelezea nguvu hiyo.

Na leo maswali yangu yanajikita huko kwenye hiyo nguvu (Mungu) maana nimeanza kuiamini lakini pia kila nisomapo BIBLIA (mimi mkristo) inanipa maswali chungu nzima.

Sasa leo swali langu limejikita kwenye UKAMILIFU wa MUNGU.

Naombeni wasomaji mnielewe kuwa sina maana ya kukufuru (maana mara nyingi niulizapo maswali kuhusu MUNGU huwa naambiwa nakufuru) bali mimi nataka kujifunza zaidi kumuhusu huyu Mungu.

Dini nyingi (hasa Ukristo na uislamu) zimekuwa zikimwelezea Mungu kuwa ni Mkamilifu sana,mwenye nguvu nyingi sana, uwezo na akili zake hazichunguziki, hashindwi na chochote n.k.

Je hilo lina ukweli ? kupitia Biblia mimi nimeanza kudhani kwamba huenda kweli Mungu ana nguvu nyingi sana ila siyo zote, ana uwezo mkubwa sana ila siyo uwezo wote,ana maarifa mengi sana ila siyo maarifa yote, ana ukamilifu mwingi sana ila siyo ukamilifu wote n.k

Nasema haya ni kutokana na maswali yafuatayo :

1. Kama Mungu ana ukamilifu wote, kwanini sasa alimuumba malaika (Lucifer/shetani) alafu badae akaja kumuasi?
Kama Shetani/Lucifer aliasi maana yake ni kwamba Mungu alimuumba huyu kiumbe akiwa na madhaifu kadhaa na ndiyo maana alishindwa kuitii amri/mamlaka ya muumbaji wake.

Kama Mungu angelikuwa na ukamilifu wote, basi malaika wote wangelikuwa wameumbwa katika namna ya utii pekee, uasi usingetokea na huo uasi unadhihirisha kwamba Mungu aliwaumba hawa malaika wakiwa na udhaifu flani, hawakuwa na uimara wote.

2. Uumbaji wa Eva (Hawa) unaonesha kulikuwa na madhaifu pia.
Katika Biblia takatifu kwenye kitabu cha mwanzo, kuna mistari inaeleza kuwa "Mungu alimpa usingizi mzito Adam, alafu akabandua sehemu ya ubavu wake na kumfanya/kumuumba mwanamke (Hawa/Eva)".

Alafu Mungu akamwambia Adam kuwa huyu mwanamke atakuwa msaidizi wako

Lakini ni huyo huyo mwanamke ambae shetani (kwenye umbo la nyoka) alienda kumdanganya akachukua matunda ya mti walioambiwa asile yeye akala na akampelekea na mumewe (Adam) pia akala.

Lakini Mungu alivyomuuliza Adam kwanini umekula matunda ya mti ambao nilikwambia usile, Adam alijibu kuwa "Ni huyo mwanamke uliyenipa ndiye aliyeniletea nikala".

Tukio hili linadhihirisha kuwa Mungu alimpa Adam msaidizi (Hawa) ambae ni dhaifu sana na ndiyo maana alisababisha dhambi ikaenda hadi kwa Adam.

Na huenda kama Mungu angelikuwa amempa Adam msaidizi imara asiye na madhaifu basi ile dhambi ya kula tunda ingeepukika.

Uko wapi sasa ukamilifu wote wa Mungu ikiwa aliweza kuwaumba malaika dhaifu (ambao walikuja kumuasi) na pia bado akampa Adam msaidizi dhaifu kabisa ambaye alisababisha dhambi imwendee hadi Adam?

Kwa leo naombeni comment zenu zinifunze kuhusu hilo tu (La ukamilifu wa Mungu) alafu mengine nitauliza siku nyingine, na mengine nitakuwa nauliza humo humo kwenye comments zenu.

NB: Naamini Mungu yupo, kutokana na baadhi ya vitu ninavyoviona ulimwenguni (hasa uumbaji/creation) ambapo kuna baadhi ya vitu hasa sayansi inakosa majibu ya kuridhisha, ila shida yangu kubwa ni sifa za Mungu ambazo anapewa na wanadamu naona kama zinashindwa kujidhihirisha kwenye baadhi ya mambo.

Karibuni mnifunze.
Mkuu maswali yako sio magumu ila itakuchukua mda hadi kupata majibu ya kukuridhisha, chakufanya nenda YouTube mtafute mtu anaitwa Dr Zakir Naik. Jamaa ni msomi na mbobez kwenye masuala kama haya na nina amini majibu ya maswal yak yote utayapata.
NB:hili si la kupuuzia, wewe fanya kama unaenda kujaribu tu. Utakuja kunishukuru baadae
 
Sawa
 
Mkuu, Jinsi majini walivyoumbwa hatuwezi kuwaona kwa macho, labda wabadilike kwenda kwenye form ya kiumbe mwingine( kumbuka Jini Jinsi walivyoumbwa wanaweza kuingia hadi kwenye mwili wa mtu)... Lakini nadhani watu kama Mkuu Rakims anaweza akakupa elimu kidogo juu ya majini.

Kuhusu majini sema kwamba huna elimu kuhusu wao, lakini usilazimishe kwamba hawapo, ndiyo maana nikakuambia jaribu kufanya research kuhusu majini... Mimi ukiniambia nikuletee Jini umuone sitoweza lakini hiyo haimaanishi hawapo... That's why nikasema elimu ndiyo limitation yetu ya kujua mambo mengi mtu angekuja miaka 5000 iliyopita akasema kuhusu ishu za Blackholes ungemuona kichaa kwasababu elimu hiyo huna.

Hakuna Evidence yoyote ya Evolution.... Mfano unaweza kuthibitisha kwamba Mtu wa kwanza alikua Sokwe? Unaweza kuthibitisha kwamba Mtu ashawahi kuwa na mkia?
Dogo mbona unakimbilia sokwe...hamna mtu Ashawahi kuwa sokwe...hamna mtu kasema hivyo...Ila Yale mafuvu hayafanani na sokwe au binadamu ndo inaishwa tumetoka kwenye family moja. DNA zetu zinafanana zaidi ya asilimia 50% unataka ushahidi gani mwingine. Sasa wewe niambie kwa Nini una amini majini usiamini vampires, fairies, dragons, leprechauns, ponies, vyote hivyo ..why umechagua majini tu..ni coz la kitabu chako tu...Kuna tofauti gani na kitu ambacho hakiwezi kuwa sensed na kitu ambacho hakipo..usisingizie technology sijui blackhole saa hivi tunatechnology ya kuachanisha electron..na Kuna technology ya kuona nyota zipo ma million ya ma billion ya kilometers kwa Nini jini lako tusilione, Lina ukubwa gani Lina udogo Gani lina umbali gani..na Kama ni Kama Gas, gas inauzito inajaa kwenye pipa...haya jaza majini kwenye mtungo wako afu uniletee acheni dhana za mababu kwanza.. okay kisa hujui binadamu katokea wapi au hutaki kuamini kitu ambacho Ni fact na unafundishwa Hadi mashuleni we shuleni unafundishwa majini.. unadhani hizo story hazijulikani au..lakini hawakufundishi coz Ni story za kitamaduni tu mwingine ana pepo sijui jini sijui malaika sijui bikra .lakini Sayansi haibagui haijirukiruki.. 2+2=4, hii Ni kwa mwarabu kwa mzungu kwa mwafrica ..ukipiga nyundo goti litasogea...Sayansi works religion lies na inatishia watu kuamini au mtaaungua huo moto hujauona unaishi kioga tu
 
Back
Top Bottom