Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

%100chini ya %100 maana yake ni %1hahahaha mkuu umetisha
 
Rais huchaguliwa kwa kura kisha baadae serikali huundwa, rais hata awe mbabe vipi kamwe hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe, kwani raisi anaweza kuwa kitaaluma ni mwanasayansi ila inabidi atolee maamuzi masuala ya kisiasa uchumi na kijamii inaposhindikana dola husika huomba msaada katika dola rafiki kwa maslahi ya taifa lake,

kwa sisi tuliosoma na hatujaelimika huwa tunatupa lawama zote kwa rais lakini ukweli ni kwamba serikalini hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya hata kama kilichofanyika unaona ni makosa, hata yule raisi wa ufilipino anayeuwa watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya zile huwa ni SERA ZA NCHI KATIKA WAKATI HUSIKA raisi hupata lawama kama mtekelezaji tu.....

mara ohh raisi kafunga kiwanda raisi kavunja bodi hii ni ripoti anayoletewa na wataalamu wa mambo husika na sio kama anaamka tu na kuamua, nashangaa sana mtu na vi degree vyake viwili ana challenge maamuzi ambayo yametolewa na jopo wataalumu na kuishia kumlaumu raisi sababu yeye ndiye aliyetoa amri. Tryna think aloud.
 
Wewe ndio fisimaji kabisaaa! How can we praise or blame a void?! Afterall the BUCK STOPS AT THE PRESIDENT! Sijui kama unalijua hilo, na tuliyemchagua kufanya maamuzi kwa niaba yetu ni Rais; not every Tom, Dick & Harry!

Kwa hiyo kunapokuwa na jambo la kushangilia na kusifia; tunamsifu Rais hali kadhalika kulipo na malalamiko lazima yaelekezwe kwa Rais huyo huyo; hao wengine wanahudumu kwa utashi wake na wasipokubaliana na msimamo wake hawana budi kujiuzulu!
 
Naona ueamua kuja na povu kwa fisi maji?
 
Hilo tu huna jingine? Umehemewa na hoja?! Pole fisimaji!
Matusi matusi na jazba ni chanzo cha malezi mabaya na ule utafiti wa "katika kila watanzania wanne mmoja ....."
 
Huo ndiyo ukweli. After all washauri wakimaliza ķumshauri hum wacha aamue. So he is the decision maker
 
Lakini kuna mikutano mingine ya kimataifa haitaji uwakilishi itabidi aende yeye Rais anaewakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Julius Itatiro (gwiji wa kuchambua masuala ya kisiasa), leo (30/11/2016- kwenye gazeti la Mwananchi katoka na makala yenye kichwa hapo juu. Namkaribisha tulijadili hilo kwa muono/mtazamo tofauti, ila lengo likiwa lile lile.

Julius ameuliza: "Kama miongoni mwa washauri wa Rais wapo wale wanaofanya kazi hiyo kwa manufaa ya Taifa, watu hao hawamwogopi Rais? Wanamueleza ukweli bila kumficha? Kuwa hali ya uchumi wa Taifa siyo nzuri?

Hakika mada yake inazungumzia wenye mawazo kama yake ya kueneza habari mbaya kuhusu uchumi wa nchi, kwa sababu wanazozijua, ikiwa ni pamoja na za kisiasa.

Kwa sababu hiyo lawama inakwenda kwa washauri wa Rais Magufuli wakidai wanamwogopa.

Wengine wanadiriki kumsemea Rais (kumwekea maneno) yasiyo ya kwake.

Baadhi wanakuwa wasemaji (wakujipachika) wa Makampuni na Wawekezaji ati hali ni ngumu ya kibiashara, km Kiwanda cha sementi cha Dangote au CRDB, ambao wenyewe wamejitokeza na kusema tofauti na habari zinazosambaa mitandaoni au kwenye vyombo vya habari.

Waandishi wa habari wengine wamethubutu kudai kwamba "siasa za majukwaani hazitaifikisha nchi popote"!

Kwa vyovyote vile Serikali ya awamu ya Tano, kwa jinsi inavyoendesha na kusimamia uchumi, mimi binafsi nakubaliana na mageuzi hayo. Sababu ni zifuatazo:

Kwa miaka zaidi ya 50 ya uhuru:
1) Kilimo bado ni cha jembe la mkono.
2) Kilimo hicho, cha jembe la mkono, bado ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii.
3) Sekta ya viwanda ni kama ilikufa, nchi ikabaki ya kuchuuza isichokizalisha.
3) Sekta zingine za uchumi, km madini, uvuvi, utalii, nk vimetawaliwa na wawekezaji wa nje na kugubikwa na ufisadi wa hali ya juu, ikilindwa na mikataba isiyoinufaisha nchi. Bado tunadai nchi inawawekezaji, ambao sasa wanatishia kuondoka. Km, najiuliza almasi ya Mwadui (inaishia sasa) imesaidia nini, kimaendeleo, Mkoa wa Shinyanga hususani mji wa Sinyanga ambao bado wananchi wanapata maji yasiyo safi na salama!

Yako mengi yanayohitaji mageuzi makubwa, kama yalivyokuwa yakipigiwa na yanaendelea kupigiwa kelele na kambi ya upinzani.

Yumkini, hapakuwa na kiongozi ambaye alithubutu kuchukua hatua, kasoro Baba wa Taifa, marehemu Mwl JK Nyerere na sasa Rais Magufuli.

Nasema hivyo, kwa sababu kuu moja ambayo ni tofauti ya mazingira ya kisiasa wakati wa Mwl na sasa.

Baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa, viongozi wengi wamekuwa waoga kuchukua maamuzi magumu ya kimaendeleo, wakichelea kupoteza umaarufu wao kisiasa.

Kwa sababu hiyo, upande wa upinzani wametumia mwanya huo kudhoofisha juhudi za kimaendeleo kwa kushawishi wananchi kususia ushiriki wao katika shughuli za maendeleo yao. Mifano iko mingi km kuhamasisha wananchi wasichangie miradi ya maji ati ni wajibu wa Serikali. Kila mtu anajua athari za ushawishi huu kijamii. Hadi sasa wananchi sehemu bado hawapati maji safi na salama.

Kinachotokea sasa, Rais Magufuli hakika ameamua na siyo tu kuthubutu, kutekeleza maamuzi magumu kwa vitendo. Uthubutu wake huo ndio unachochea wateuzi wake kisiasa (Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya) kumuiga. Hawana woga wa kupoteza umaarufu wao kisiasa.

Matokea yake, hakika yanatia moyo kuwa nchi inakoelekea sasa ni kwenye mageuzi yenye tija kiuchumi. Mifano iko mingi ila michache yenye uzito ni kama ifuatayo:
1) Wanaotoa huduma za kijamii wameanza kuwajibika kiasi kwamba huduma hizo sasa zinaboreka.
2) Wafanya biashara wasio waaminifu (wakubwa kwa wadogo) wanafunga biashara zao ikiwemo mabenki - kilio chao kinasikika kila mahali.

Hakika na wapinzani wameisoma namba kiasi wamebadili gia angani na sasa ni "Operesheni Kata Funua). Wamechukua tahadhari ya madhara watakayoyapata kisiasa iwapo wanayoyatarajia na wasiyoyatarajia yatatokea.

Wengine siye, kama alivyodokeza Dk Ulingeta Mbamba, mhadhiri UDSM na Dk Oswald Mashindano, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) - Gazeti la Mwananchi, Jumatatu, Novemba 28, 2016:
1) Lazima tuwe "adaptive" (kubadilika kulingana na hali). Ni muhimu sana kubadilika
2) Hatuwezi kuishi maisha ya leo kwa kipato cha jana. Kama hali ya jana ilikuwa nzuri, tofauti na leo, tuishi kulingana na kipato cha leo (Dk Mbamba).
3) Unajua tulizoea kupata fedha za 'kupiga'. Watu walitumia vibaya fedha za Serikali. Kila mtu afanye kazi na alipwe kwa kazi hiyo. (Dk Mashindano)
 
Mi nionavyo Dsm ndo hali mbaya Kusini mbuzi wananywesha juice badala ya majani. Korosho zimejibu ukiwauliza watu wa Mtwara sidhani kama wana hali mbaya kiuchumi. 'Au nyie mnazungumzia uchumi upi ebu nielesheni jamani?
 
Reactions: Ame
Wakati watu wanalia hali mbaya ya kiuchumi, kusini mwa Tanzania watu wanasherehekea na hawajui matumizk ya mihela waliyonayo. Ukifanya kazi kwa bidii lazima utapata mafanikio
 
Huyu Kiti Wa Mganga Nae Kawa Mchumi Siku Hizi, Hii Nchi Ina Mambo
 
Si kuwa hashauriki ni yeye anayewashauri washauri wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…