Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Wakiwekwa wazi tukiwajua, tutawakosoa zaidi ya Mh rais
Inatosha kutambua Ikulu ni taasisi kubwa iliyosheheni wafanyakazi wenye fani na sifa bora katika kila kitengo.
basi ngoja abebe mzigo mwenyewe kwa kuwa yeye ndiye anawajibika,na sheria zinasema halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote kwenye jambo lolote
 
Kwanini tuamini kuwa ana washauri? Labda hana.

Na badala yake yeye ndio Mshauri.
Tunalishwa matanga pori eti urais ni taasisi! Upuuzi mtupu, urais hauna ubia!

Rais hana washauri wengine zaidi ya mawaziri wake!
 
Urais ni taasisi. Rais ni mkuu wa taasisi hiyo. Kiutendaji,Rais hutenda au kuamua baada ya kushauriwa au kushauriana na Washauri wake. Wapo Washauri wa kila sekta imhusuyo Rais.

Wapo Washauri wa kisheria,kiuchumi,kisiasa na hata kiutamaduni. Taasisi ya Urais imekamilika kila idara. Tangu kuanza utumbuaji,imekuwa ikijitokeza hali ya Washauri wa Rais kuwa 'wachonganishi' badala ya 'washauri'.

Mara baada ya utumbuaji,hudhihirika kuwa sababu zinazoelezwa na Rais katika kutumbua huwa ni tofauti na zile halisi. Nataja mifano ya utumbuaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC,Maafisa kadhaa wa TAKUKURU na hata Bodi ya TRA.

Je,Rais hujazwa hasira badala ya kushauriwa katika kuelekea kutumbua? Je,Rais wetu mpendwa amezungukwa na 'Washauri' au 'Wachonganishi'? Tatizo hasa ni nini?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mimi nadhani rais wetu ana wachonganishi lakini pia washauri. Lakini kutokana na maamuzi anayoyafanya nadhani husikiliza zaidi wachonganishi kuliko washauri.
 
ukiwa mgeni mjini lazima ukutane na bango
"kuelekezwa buku,kupelekwa 2000"

hutaki unaacha/unaachwa upotee
 
Urais ni taasisi. Rais ni mkuu wa taasisi hiyo. Kiutendaji,Rais hutenda au kuamua baada ya kushauriwa au kushauriana na Washauri wake. Wapo Washauri wa kila sekta imhusuyo Rais.

Wapo Washauri wa kisheria,kiuchumi,kisiasa na hata kiutamaduni. Taasisi ya Urais imekamilika kila idara. Tangu kuanza utumbuaji,imekuwa ikijitokeza hali ya Washauri wa Rais kuwa 'wachonganishi' badala ya 'washauri'...
Mmoja wa washauri wake ni Jamaa Mmoka Kigogo wa Mkoa wetu
 
Rais mzuri ni yule anaeomba ushauri kwa washauri na wataalam
kabla hajaongea au kuamua kitu

Sio rais anaenda kwa media na kulaani taasisi kuhifadhi hela kwenye fixed deposit
halafu anatokea mchumi anae heshimika na mmoja wa washauri wa Rais kwenye uchumi na kusema
hakuna kosa lililorendeka na fixed deposit ni sahihi....

halafu mtu bado anabisha kama Rais anasikiliza washauri?
The Boss, nitakuuliza swali baada ya kunijibu swali lifuatalo, kutokana na hoja yako ya Rais mzuri.

"Nchi yetu imekuwa na Marais wanne waliomtangulia Rais wa sasa hivi. Kwa tafsiri yako ya Rais mzuri, ni nani kati ya waliomtangulia Rais wa sasa anakidhi vigezo vyako?"
 
Swali lako gumu sana
ndo maana watu wengi wanaishia kusema Kikwete
simply sababu Kikwete aliacha wapinzani wamkosoe
na bunge liwe na nguvu na free media

So kwa vigezo hivyo labda
kwa maoni yangu binafsi hakuna....kila mtu alikuwa na mazuri yake na mapungufu
na changamoto

Nyerere labda kwa kuwa alikuwa founder...muasisi wa Taifa...
alikuwa na changamoto tofauti....
 
Acha unafiki na lawama zisizo na msingi, rejea kauli ya mh mkuu wa mkoa Dar alivyowasweka ndani viongozi wa upinzani kwa kisingizio kuwa wamechangisha wananchi fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kusema hiyo ni kazi ya serikali.
 
Hivi Trump anasubiri nini kuapishwa hadi hiyo January 20? Wageni waalikwa au?
Umeshasikia kitu kinaitwa"KATIBA "? Kama bado inaashiria kuwa Tanzania hakuna kitu kama hicho. Wenzetu hawaapishi viongozi wao haraka haraka kwani kura zao hazihesabiwi na NEC. NISEME TU NEC NI JIPU🙁
 
...huyo mpango wamemkumbatia tangu enzi za tume ya mipango...mi huwa najiuliza amefanya nini haswa cha kukumbukwa hata akitumbuliwa kesho???...HAMNA.....zaidi ya kuleta shida kwenye kila eneo la uchumi....hivi unawezaje kutumia njia ile ile iliyokutumbukiza kwenye matatizo kutatua matatizo???.....unajua mi huwa siwaelewi watawala wa nchi hii yani....
 
Urais ni taasisi. Rais ni mkuu wa taasisi hiyo. Kiutendaji,Rais hutenda au kuamua baada ya kushauriwa au kushauriana na Washauri wake. Wapo Washauri wa kila sekta imhusuyo Rais.

Wapo Washauri wa kisheria,kiuchumi,kisiasa na hata kiutamaduni. Taasisi ya Urais imekamilika kila idara. Tangu kuanza utumbuaji,imekuwa ikijitokeza hali ya Washauri wa Rais kuwa 'wachonganishi' badala ya 'washauri'...
Waganga njaa
 
Kama katika washauri wake yupo Philip Mpango basi kazi anayo
Huyo ndio tegemeo la ushauri wa kuongeza mapato ya nchi , ndio maana kodi ya kuweka majina badala ya namba kwenye magari aliipaisha hadi 10mil kutoka 5mil , badala ya 3mil kama sisi wajinga tulivyopendekeza .
 
Wafuasi wanachojali ni kumfanya mkubwa ao afurahi, lazima wajue anapenda mambo gani wamfurahishe.
Tatizo ni kwamba, wale wanaotakiwa kuwa washauri, wamekosa ujasiri wa kuifanya hiyo kazi vizuri wameamua kufuata upepo wa mkuu.

Kwa ufupi, hana washauri.
Nadhani yeye ndio anawashuri washauri wake
 
Washauri wa Magufuli...aaa no, Wachonganishi:
1. Abdallah Bulembo
2. Paul Makonda
3. Nape Nnauye
GARBAGE IN GARBAGE OUT!
 
Asilimia 60 ni jazba na kukomoana tunaita kumwaga unga au nakuua njaa na asilimia 40 ni sababu za kutumbua zinahusika.
 
Raisi ana wachumia tumbo tu wanaomwambia maneno anayoyapenda tu ili wapate kula.
 
Back
Top Bottom