Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

hata zimbabwe walianza mdogo mdogo kuisoma namba mpk kimeeleweka sasa ndo wanaamka.
 
Kila mara kwenye vijiwe vyetu vya kahawa na meza za magazeti utaskia, "tatizo washauri wake hawampi ushauri mzuri"... hivi hao jamaa wanaomshauri rais ni watu gani?? Mawaziri, viongozi wastaafu, wanazuoni wa vyuo vikuu... aisee hii ishu nimejiuliza muda mrefu sana hivi ni kina nani ndio washauri wake huyu rais wetu, na mpaka ifikie hatua askilize ushauri wao basi ni watu anaowaheshimu sana..
 

Washauri wake wakuu ni :
  1. Rais Mstaafu wa awamu ya tatu ( 3 ) Mzee Benjamin Mkapa.
  2. Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba.
  3. Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya.
Naomba niishie hapa tafadhali.
 
chief of staff...wa mjengoni.anajua..
ngoja aje hapa atuambie si yumo humu....anatumia jina la naniliuu....!!
 
Rais Magufuli anaonekana aidha
hana washauri wazuri au ana
washauri wazuri sana, lakini
wamechoka kumsharu au hawataki
kumshauri vizuri au yeye
mwenyewe ni mbishi hataki
kupokea ushauri wa mtu yeyote.
Ikumbukwe kwamba hulka za
watawala kutotaka kushauriwa
wala kutumia ushauri wa washauri
wao ndiyo sababu kubwa ya
maendeleo yaliyopatikana hapa
nchini kutolingani kabisa na
maendeleo ya nchi iliyojitawala
kwa kipindi cha miaka 55 iliyopita.


Rais Magufuli anaonekana
anazungumzia mabadiliko mdomoni
tu, lakini moyoni anarudia makosa
ya watangulizi wake wote
wanne…!!!”

Uongozi wa Rais Magufuli ulianza
vizuri, lakini jinsi tunavyozidi
kusonga mbele ndivyo ambavyo
udhaifu mbalimbali unavyozidi
kujionyesha. Zoezi la utumbuaji wa
majipu limekuwa muhimu sana na
hasa ndilo lililompa sifa na imani
kubwa toka kwa wananchi, lakini
zoezi hili limekuwa na walakini na
hata mapungufu mengi kwa vile
limekuwa ni zoezi ambalo halina
uongozi wa utaratibu. Tumeandika
sana kuhusu mapungufu haya
tukitaka tuwe na tume maalumu
ya kutumbua majipu na maridhiano
na tume hii ipewe mamlaka
makubwa ya kisheria ili malengo ya
zoezi hili yapatikane. Zoezi la
kutumbua majipu linaendelea, lakini
halina utaratibu maalumu na
matokeo yake limekuwa
linaonekana kama limeegemea
upande mmoja na huku eneo
kubwa likiwa lipo huru linaendelea
na hujuma kama kawaida.

Utumbuaji umekuwa wa kuchagua
au naweza kusema umekuwa wa
upendeleo kwamba nani
atumbuliwe na nani asitumbuliwe
na hii inategemeana na mahusiano
yako ya huko nyuma au ya sasa
hivi na washauri wa Rais Magufuli;
ukiwa una uhusiano mzuri na
washauri wa Rais Magufuli, basi
wewe huwezi kutumbuliwa, bali
utaendelea kulindwa kwa
kujengewa mazingira mazuri
ambayo muda wote unaonekana
raia mwema kumbe ni mhalifu.

Washauri wabaya na
wanaompotosha Rais Magufuli
wameuonyesha udhaifu wao
kwenye sakata la sukari ambapo
wamekuwa ndumilakuwili
wanaouma na kupuliza kwa wakati
mmoja; washauri hawa wa Rais
Magufuli wamekuwa wakipanga
mikakati ya hujuma na wazalishaji
na wauzaji wakubwa wa sukari na
wakati huo huo wameendelea
kumshauri Rais Magufuli ushauri
potofu kwa makusudi ili akwame
na aonekane kwamba
ameshindwa. Wamemshauri
kwamba azuiye uingizaji wa sukari
nchini kwa vile tuna viwanda sita
vinavyozalisha sukari ya kutosha,
lakini wakati huo huo
wanawaambia wazalishaji wa
sukari wapunguze kiwango cha
uzalishaji na huku wakiwashawishi
matajiri wanaouza sukari kuficha
sukari yao; yote hayo ni katika
mikakati maalumu ya kuhakikisha
kwamba Rais Magufuli anaonekana
siyo kiongozi makini, bali ni
mbabaishaji..!!!


Washauri wake pia wameshindwa
kumshauri kwenye mambo mengi
kama vile CELTEL kurudishwa
serikalini kwa 100%; walitakiwa
wamshauri alipoingia tu
madarakani atoe tamko rasmi na
apelike mswaada bungeni wa
kusimamisha uuzaji wa hisa au mali
zote za umma zilizobinafsishwa ili
kutoa nafasi kwa serikali kutimiza
malengo yake. Hili lingefanyika,
basi AIRTEL wasingeliuza mnara
yao kwa kampuni la Kimarekani
kwa vile serikali ilikuwa tayari
imeshatoa tamko, lakini washauri
wa Rais Magufuli hili hawakuliona
au hawakutaka kumshauri hivyo
na matokeo yake AIRTEL imebaki
na mitambo peke yake na huku
kampuni lingine likiwa linamiliki
minara..!!! Je, kuningana na
mazingira hayo tata serikali
itarudishaje 100% ya CELTEL..!?

Wameshindwa kumshauri kuhusu
katiba mpya yenye maoni ya
wananchi; wanafahamu fika
kwamba serikali yoyote adilifu
inaongozwa na kusimamiwa na
katiba nzuri iliyoandikwa na maoni
ya wananchi walio wengi.
Utumbuaji huu wa majipu utakuwa
hauna maana yoyote kama
utakuwa hausimamiwi na katiba
mpya yenye maoni ya wananchi.
Hatuwezi kuendelea kushabikia
utumbuaji wa majipu unaofanywa
na mtu mmoja kwa vile kila
mwanadamu ana mwanzo na
mwisho wake; sasa leo hii
tukishabikia tu Rais Magufuli
anatumbua majipu; Je, kesho au
kesho kutwa mungu akimpenda
zaidi Rais Magufuli nani
ataendeleza utumbuaji majipu bila
ya mwongozo na sheria..!!??


Wameshindwa kumshauri kuhusu
wenye pesa na mali nje ya nchi
kinyume cha sheria; walitakiwa
wamshauri kwamba pesa na mali
zote zikamatwe na kurudishwa
nchini ili zijenge uchumi mkubwa wa
nchi. Wameshindwa kumshauri Rais
Magufuli kwamba amwagize waziri
mkuu Majaliwa kwenye mkutano
uliomalizika London hivi karibuni
kutoa tamko kali kutoka kwa
serikali ya Rais Magufuli kuhusu
pesa na mali za Tanzania
zilizofichwa nchi za nje; matokeo
yake ameenda tu kama msikilizaji
wa mkutano ambaye aliishia
kufahamiana na viongozi
mbalimbali duniani..!!! Je, Tanzania
lini inakusudia kudai pesa na mali
zake zote zilizofichwa mataifa ya
nje kurudishwa nchini..!? Au
tunataka tuzirudishe kwa kufanya
vikao vya chini kwa chini vya siri ili
watanzania na dunia nzima wasijue
kwamba Tanzania kuna mafisadi..!?


Wameshindwa kumshauri kuhusu
bunge kuendeshwa gizani wakati
anajitangaza mtumbuaji wa
majipu..!!! Sasa wananchi
watachangiaje hoja mbalimbali
zinazojadiliwa bungeni ikiwa
hawajui nini kinachoendelea.
Wananchi wengi wanaona kwamba
bunge kuendeshwa gizani ni
kuficha madudu ya mafisadi wa
CCM na washirika wao. Kulingana
na mazingira hayo inakuwa haileti
maana yoyote kama Rais Magufuli
anajigamba kutumbua majipu,
lakini anaendesha bunge gizani ili
awalinde mafisadi sugu.

Wameshindwa Kumshauri juu ya kulinda katiba yetu ibara ya 18 inayoruhusu raia wake kutoa maoni na kupashana habari, badala yake tumeona mitandao ya kijamii, magazeti na radio zikifungwa kwa sheria kandamizi

Wameshindwa Kumshauri rais kutoka kauli zisizo na hadhi ya urais na zinazozua mijadala.

"atakayeleta fyokofyoko", "ningewalaza chini" ,"sijaribiwi" ni miongoni mwa kauli zilizozua mijadala.

Pia Washauri wameshindwa kumshauri rais aondoe zuio lake la vyama vya siasa kufanya siasa za majukwaani.

Kitendo cha kuzuia vyama vya upinzani kufanya siasa sio tu kinaua demokrasia lakini kinaonesha asivyo mvumilivu na mkomavu wa kisiasa.

Wangemshauri Rais aruhusu vyama vifanye siasa huru, wapumue waondoe vinyongo vyao, waondoe madonge yaliyoko rohoni, hatimaye kuwe na umoja na utengamano wa kitaifa.

Shukrani Ngonyani
Lilongwe
Desemba 18.
 
Mkuu umeeleza kwa kirefu sana hizo gaps zinazoonekana waziwazi kwenye awamu hii ya tano, na kwa namna gani basi washauri wake wangeweza kumshauri kuyaweka sawa haya mapungufu.

Just to let u know, hakuna cha yeye kushauriwa katika yote hayo uliyoyasema.. Yote anayajua vema lakini ameshaamua yawe ivyo.

Mfano mdogo... anahitaji kushauriwa ki vipi ili arudishe bunge liwe live..!!??

Unataka kusema hajui umuhimu wa Bunge kuonyeshwa live na siku zote lilikuwa live??

Na kelele zote zilizokwisha kupigwa unafikiri hajazisikia kuhusu kurudisha bunge live ivyo kwamba mpaka ashauriwe na washauri kulirudisha bunge live??

Unataka kusema hajui muhimu ni kipi kiwe live kati ya kwa mfano, Bunge na mkutano wa NEC wa CCM ulioonyeshwa live na Azam tv siku chache zilizopita??
Jibu ni kwamba Anajua kila kitu.

Ameshaamua iwe hivyo.. Hakuna wa kumshauri abadilike.

Na wala washauri wasilaumiwe kwa chochote..

Ameshaona hiyo ndio njia ya kuendesha nchi.

It's a one man show... let's continue watching..!!
 
Mbona mnazusha mambo mengine bila kuwa na uhakika? Issue ya Bunge kutokuwa live imeanza leo? Issue hii ilianza mabunge yaliyopita na ukapitishwa mswada na sheria ikatungwa Bunge kuwa lina media yake. Ukitaka habari za Bunge nenda kwa taasisi hiyo. Maana yake hakuna namna utapata habari ya bungeni nje ya chombo cha habari bungeni. Mnamlaumu kwa kipi? Kufuata sheria walizozitunga wabunge wenyewe?
 
najua rais anawashauri wengi sana lakini najua washauri wake na marafiku zake wakubwa ni kagame na mseveni na hao ndio watu pekee anao wasikiliza sana.

ila hawa watu nina mashaka nao sana na ninaona wanaweza wakawa wanampa ushauri rais wakuitumbukiza tanzania shimoni kwasababu huenda hawaipendi tanzania.

na ninajiuliza swali moja inawezekana vipi nchi ambayo wanasema ni nchi ya amani harafu kila siku inazidi kuwa maskini?

kama rais anaipenda tanzania hawa watu aache kufuata ushauri wao haraka sana.
 
Kwa wale wanaojitambua na kuona katika TV sherehe zile za jeshi ambazo baadae ziligeuzwa za ccm watajiuliza swali moja au mawili.
Hivi hawa wapambe wake na wasaidizi wake akiwemo PM, wanawezaji kumshangilia JPM wakati anasema maneno ya uongo kama ule kuwa aliingia madaraka sukari ikiwa shs 5000 na sasa ameishusha mpaka 2500 na wao wanampigia makofi na vigelegele kwa shangwe?
Hawaoni kuwa kwa akili ya bwana mkubwa anaona kuwa hata akidanganya watu wanafurahia? Jee shangwe hizo za wapambe sio kumfedhehesha kiongozi wa nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…