Naanda mashtaka ya kumtimua Mh Lema Chamani.

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima kwenu Wanajamvi,

Mimi kama Katibu wa Tawi la Lemara CDM,Wilaya ya Arusha.
Naandaa mashtaka ya kumtimua Lema katika Chama chetu kwasababu ya kukiuka taratibu,kanuni na miongozo ya chama.

Mh Lema alikuwa mjumbe wa kamati kuu kupitia nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini.Mh Lema hakugombea nafasi hii kubwa na nyeti ambayo ilimwezesha kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Mheshimiwa Lema sasa ni Mwanachama wa kawaida sana mamlaka yake ya nidhamu ni Tawi ambalo Mimi ni Katibu wake.

Tumemwona Lema kupitia vyombo mbali mbali vya chama akikibagaza chama chetu na kuwabagaza Viongozi wakuu.

Shughuli ya kumtimua Lema ipo ngazi ya Tawi si wilaya,Mkoa,Kanda wala Taifa.

Ngongo kwasasa Lemara.
 
Hiyo njaa yako inakutoa akili kabisa kwani akitoka Chadema atakosa oxygen, eti nyie ndiyo washauri wa Sultan Mbowe, bure kabisa.
 
Acheni udikteta uchwara. Mnataka nyie muwe na mawazo sawa kama visahani?
 
Acheni udikteta uchwara. Mnataka nyie muwe na mawazo sawa kama visahani?
Mheshimiwa Lema atapatiwa mashtaka yake na atapewa nafasi ya kujitetea na ataruhusiwa kuambatana na mawakili wasiozidi 5.
 
Lengo la Waropokaji wengi ni hilo, Lakini Chadema haitoingia kwenye huo mtego
 
Mchango wa Lema chamani tunaufahamu vzr, tunaomba kujua mchango pia ktk kuifikisha chadema hapo ilipo leo
 

..haitasaidia.

..dawa ni kumzuia asizoze zaidi kuhusu Mbowe na Wenje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…