Mku huu ushauri ni mzuri sana.
Ila kubwa zaidi awaombe Watanzania Msamaha huu utamsaidia sana kwani tulio na huruma ni wengi.
Aombe msamaha kama aliowahi kuomba Rais Moi hili asipolifanya ninaamini atakuja kujutia wakati huo yuko Jela au la japokuwa simwombei hili limkute kabisa kwani ameshajifunza kuendana na mazingira au anayoyapitia aliyekuwa Mku wa Wilaya ya Hai
Makonda haruhusiwi kuingia US, kwa sababu ya "kuwanyima watu haki ya kuishi".
Muuaji mnamshauri akimbie bila ya kufikishwa mahakamani? Siungi mkono yeye kuviziwa mafichoni, lakini ni halali kabisa kwa yeye kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma dhidi yake.
Waliopo kwenye vyombo vya dola, wanaeleza kwamba mtu huyu aliongoza kikundi cha kuwateka, kuwaua na kuwapoteza watu waliokuwa wakimkosoa marehemu na serikali yake, na kwamba kikundi hicho kiliaminika na kupewa nguvu na marehemu kuliko taasisi rasmi ya TISS. Kikundi hiki kiliwajibika moja kwa moja kwa marehemu. Kikundi hiki, kwa kauli za Siro, zaidi kilifahamika kama "Watu Wasiojulikana", japo walikuwa wanajulikana.
Huyu ni vema akamatwe mapema, ajibu tuhuma dhidi yake, awataje watu wake aliokuwa akiwatumia kuendesha uharamia. Mmoja tunaambiwa yupo mahabusu kule Kusini mwa nchi kwa kosa la kumpora fedha mfanyabiashara na kisha kumwua.
Sabaya wakati akiwapora watu fedha kwa nguvu, alikuwa akiwaambia kuwa, hii inaitwa Makonda style! Sabaya naye ni shahidi muhimu dhidi ya Makonda.
Sanane kapotezwa
Azory kapotezwa
Kanguye kapotezwa
Lisu alimanusura
Mo alitekwa na kuachiwa
Roman alitekwa na kuachiwa
GSM waliporwa mamilioni ya pesa kwa vitisho mbalimbali
Mengi aliporwa mamia ya mamilioni kwa kudanganywa
Familia ya Chacha kule Mwanza waliporwa kiwanja Capripoint
Kuna watu wengine waliporwa fedha kwa ahadi kuwa ataongea na marehemu walegezewe kodi na wawe karibu na Serikali.
Makonda atendewe haki, asiviziwe mitaani, apelekwe mahakamani kama alivyofanyiwa Sabaya, akajibu tuhuma mbalimbali, ikiwemo za mauaji. Makonda ni mwovu mkubwa, kwa kiasi kikubwa, zaidi ya Sabaya. Mwanafunzi wake wa uovu, Sabaya, yupo jela, mwalimu wake yupo huru. Hii siyo haki.