Naandika nikijua hasa nini kinaendelea. Makonda fanya haya usidhurike

Hakika kikijitokeza chama kizuri cha Siasa chenye maono yanayogusa wengi kitajipatia wafuasi wa kutosha.

Bado kiu ya watanzania ni kubwa sana wengi wanakuja na kujinadi kwamba watakata kiu ya wananchi kumbe wanakata kiu yao binafsi na kufanya safari yetu Kuwa ndefu zaidi.
 
Mke wa Bashite ni mmeru na sasa wapo maeneo ya kwa msola njiro Arusha.

Eti rwanda 😂
By the way Bashite ameanza kupiga kelele kwasababu ameshapata taarifa kuwa file lake lipo kwenye final stage kabla halijafika kwa DPP.

NB: britanicca ungefanya citation kuwa huu uzi wako ni copy and paste kutoka Twitter kwa fbuyobe.
 
Du…kweli Makonda jua limemchwea!
Hata Riz alimtuhumu madawa ya kulevya!
Kibao kimegeuka.
Ataponaje?
 
Hata mm nilikuwa najiuliza kwann Ids ni zilezile kwa mambo yale yale?...Toka 2016 nijiunge rasmi humu ndani. Watu wanalipwa kumpambania mtu mtandaoni
Wanalipwa ndo maana kelele mingi, tunajuwa ukweli kuwa hao wapenda mabadiliko nao wana maboss ambao wako upande wa pili, hatuhangaiki tena.

Kwa ufupi upinzani ni ka genge ambako kqzi yake ni kuisaidia serikali kufanya mambo yake.

Lazima vikelele kelele viwepo.ndo nchi ibaenda.

Bure kabisa
 
Serikali ikichukua hatua mapema kumshitaki Makonda kwa matumizi mabaya ya madaraka, ndiyo pona yake.

Mtoa mada kasema kinaga ubaga, kuna wazito wanaoweza/kutaka kulipiza kisasi kwa waliyotendewa.
Wa kumuokoa Makonda ni serikali kumshitaki kisheria.
 
Tell her
 
Du mpaka sasa ulikuwa hujaelewa?
 
Ndg nikajuwa wanaowindwa kama swala v simba ni wa nje ya chama pendwa,kumbe hadi ndani kwa ndani!!.Kweli cheo ni mapambo ya muda ishi na watu vema.Maskini hafilisiki.
 
Angeenda hata Angola huko ama hata Congo tu kwa njia za panya si mshiko anao anakaaa huko hata miaka kumi anageuka huku watu wameshatulia sasa anapo kaaa watu wanamuona wanazidisha hasira.

Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
 
Makonda haruhusiwi kuingia US, kwa sababu ya "kuwanyima watu haki ya kuishi".

Muuaji mnamshauri akimbie bila ya kufikishwa mahakamani? Siungi mkono yeye kuviziwa mafichoni, lakini ni halali kabisa kwa yeye kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma dhidi yake.

Waliopo kwenye vyombo vya dola, wanaeleza kwamba mtu huyu aliongoza kikundi cha kuwateka, kuwaua na kuwapoteza watu waliokuwa wakimkosoa marehemu na serikali yake, na kwamba kikundi hicho kiliaminika na kupewa nguvu na marehemu kuliko taasisi rasmi ya TISS. Kikundi hiki kiliwajibika moja kwa moja kwa marehemu. Kikundi hiki, kwa kauli za Siro, zaidi kilifahamika kama "Watu Wasiojulikana", japo walikuwa wanajulikana.

Huyu ni vema akamatwe mapema, ajibu tuhuma dhidi yake, awataje watu wake aliokuwa akiwatumia kuendesha uharamia. Mmoja tunaambiwa yupo mahabusu kule Kusini mwa nchi kwa kosa la kumpora fedha mfanyabiashara na kisha kumwua.

Sabaya wakati akiwapora watu fedha kwa nguvu, alikuwa akiwaambia kuwa, hii inaitwa Makonda style! Sabaya naye ni shahidi muhimu dhidi ya Makonda.

Sanane kapotezwa
Azory kapotezwa
Kanguye kapotezwa
Lisu alimanusura
Mo alitekwa na kuachiwa
Roman alitekwa na kuachiwa
GSM waliporwa mamilioni ya pesa kwa vitisho mbalimbali
Mengi aliporwa mamia ya mamilioni kwa kudanganywa
Familia ya Chacha kule Mwanza waliporwa kiwanja Capripoint
Kuna watu wengine waliporwa fedha kwa ahadi kuwa ataongea na marehemu walegezewe kodi na wawe karibu na Serikali.

Makonda atendewe haki, asiviziwe mitaani, apelekwe mahakamani kama alivyofanyiwa Sabaya, akajibu tuhuma mbalimbali, ikiwemo za mauaji. Makonda ni mwovu mkubwa, kwa kiasi kikubwa, zaidi ya Sabaya. Mwanafunzi wake wa uovu, Sabaya, yupo jela, mwalimu wake yupo huru. Hii siyo haki.
 

hahahaha Mwenyekiti Mzee wa Saigon..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…