Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

South Africa ya siku hizi ina watu wema hivyo? Yani umkute mtu analia uende kumuuliza analia nini unamsemesha kizulu then unagunduwa ni Mtanzania unampeleka kwako.

Konda tafadhali nishushe hapahapa nimefika, mwendo wa dereva ni hatarishi.
Labda atuelekeze hapo park station jamaa alikua kakaa analia kajiinamia. Labda sio SA
Absolutely his lie. Labda Kama Kuna code kwenye hili andiko lake
 
Tatizo la wa bongo wengi wanaokkmbilia kwa kabulu ni kuwa na elimu ndogo sana, nafikiri wengi wao hata shule ya msing hawakumaliza. Yahaani hata ktk vidili vyao utakuta wanachomeanachomeana. Yahaani wametawaliwa na ujingaujinga
Hata hao ma middle class wa bongo dizonga, Ni walewale sema experience & exprossure. Ndio zinawafanya kuonekana ma alwatan wa kabulu.
 
Sisi ndio wabongo, umasikini ni asili yetu. Nilimchukua shemeji yangu akasimamie biashara ya kukata mbao porini.
Najinyima natuma pesa KILA siku dogo anachana mbao anauza pesa natuma dogo anafungua zipu na vizibo.

Mimi mjini nakula dagaa.Zingine anamaliza kwa waganga eti aniloge KILA akiniambia niwe nakubari,miezi 3 nimepigwa milioni 8.
Kufatilia shem kazima simu kakimbia,miaka 11 sasa sijaonana nae

Hawa ndio wabongo
 
wasaidie tu watz ukiwa nje na usitegemee shukrani. ila binafsi nilipokuwa majuu, kati ya watu niliokuwa nawakimbia ni wabongo. na sijutii kwa nilichokifanya. sitaki kueleza sana nisije kwuaharibia wengine walioko huko.
 
Imagine, wakenya ni mabingwa wa wizi lakini wakimwona mbongo huko Kenya hasa wachagga wanamwogopa balaa maana wanajua kupigwa ni nje nje.
Hata Wakenya tunawaogopa balaa,ukipeleka mzigo wa pesa nyingi ngumu kuondoka na pesa au wanakuchomesha kwa askari
 
Tatizo la wa bongo wengi wanaokkmbilia kwa kabulu ni kuwa na elimu ndogo sana, nafikiri wengi wao hata shule ya msing hawakumaliza. Yahaani hata ktk vidili vyao utakuta wanachomeanachomeana. Yahaani wametawaliwa na ujingaujinga
hata hivyo wabongo waliopo kwa kaburu wala hutakiwi kuwaongelea, kwasababu ni hawa wahamiaji walioenda kinyume na sheria. hao ogopa kama ukoma hadi ujambazi na kuua watz wenzao wanafnaya huko south. ila kwa ulaya labda kidogo wale walioenda kusoma na sio wale waliofeli maisha wanahangaika tu kwa kuishi huko, wanajifanya wajuaji na ukiingia cha kike wanakuzunguka na kukufanya mbala.
 
wasaidie tu watz ukiwa nje na usitegemee shukrani. ila binafsi nilipokuwa majuu, kati ya watu niliokuwa nawakimbia ni wabongo. na sijutii kwa nilichokifanya. sitaki kueleza sana nisije kwuaharibia wengine walioko huko.
Hata makazini urafiki uishie makazini huko huko kama una nyumba kali umepata msiba au sherehe bora uhamishe, maana utalia mara mbili watu wanafata kuona nyumba,baada ya shughuli lzm boss akuhamishe porini au upigwe zengwe kama ulidokoa mboga utasingiziwa umekula na mbegu kabisa
 
Mkuu niwe mkweli tu kwamba kwa sasa siwezi kukushauri uje Kaburu. Si kwamba nakukataza ili kukwepa kukusaidia, bali ni kulingana na uhalisia wa hali ya nchi kwa sasa. Nchi hii kwa muda wa miaka miwili iliyopita, imepitia katika misuko suko mikubwa mitatu ambayo imeharibu kabisa uchumi wake. 1) msuko suko wa kwanza ni ule uliyotokea tar 13/9/ 2019 ambapo wazawa walianzisha fujo na vurugu dhidi ya wageni hadi kupelekea baadhi ya kampuni kubwa za kigeni kufungwa, 2) msuko suko wa pili ni ule wa kufunga mipaka ya nchi na watu kuwekwa ndani bila kutoka kutokana na janga kubwa la uviko, 3) msuko suko wa tatu ni ule mshike shike uliotokea miezi kama miwili iliyopita baada ya mkuu wa nchi mstaafu kukamatwa, ulifanyika uharibifu mkubwa ambao mpaka sasa umeacha doa. So kutokana na hayo yaliotokea mambo mengi yamebadilika. Mfano vijana wengi wamepoteza ajira, vyakula vimepanda bei, kodi za nyumba hazishikiki, vibaka wameongezeka mitaani, biashara za matunda zimekuwa kila kona kiasi kwamba uuzaji umekuwa wa mdondo nk. Kwahiyo kwa uchache ni ngumu sana kukushauri uje maana inaweza kufika kipindi ukanilaumu kwa kukuacha uje bila kukwambia hali halisi. Kwa sisi ambao tuko hapa muda mrefu na tunafanya shughuli zetu ni sawa, maana tunajua tuingilie wapi na tutokee wapi ila sio kwa mgeni ndugu yangu.
 
Hahahaha.. aisee umenichekesha mpaka nabanja. Yah japo kuna wachache wema, lkn wengi ni hovyo mkuu.
 
Huyo yupo hapo hapo joberg itakua kakutana na mjanja mjanja wakashauriana kumpiga uyo mkenyaa wakaenda kufungua sehemu ingine maisha yanaendelea,
 
South Africa ya siku hizi ina watu wema hivyo? Yani umkute mtu analia uende kumuuliza analia nini unamsemesha kizulu then unagunduwa ni Mtanzania unampeleka kwako.

Konda tafadhali nishushe hapahapa nimefika, mwendo wa dereva ni hatarishi.

Aliniacha hapo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…