Nabii Bushiri aaibishwa na muigizaji aliyemlipa kutoa ushuhuda wa uongo stejini

Nabii Bushiri aaibishwa na muigizaji aliyemlipa kutoa ushuhuda wa uongo stejini

Hahaha matapeli,ndio maana dini ya Kiislam inakataza miujiza,mijiza walipewa mitume tu,hawawengine ni matapeli tu....

Nimeona video ya dada mmoja mchungaji hapa Tanzania kasahau kuzima spika,kajisahau akamwambia amaemtibu "lia uongo,piga kelele"....sauti imetoka kwenye video..
 
Ila Hao manabii na Hao wanaoigiza kufanikisha unabii feki,,,adhabu yao moja Hakuna aliye salama
 
Waigizaji wenye vipaji vya hali ya juu, sio kama wale waigizaji wa Tapeli 'Nabii' Olivia ambao wanakuwa hawajapangwa vizuri hadi waambiwe "lia kwa nguvu, piga kelele"

 
Ona hili tapeli linavyotafuta kiki kwa nguvu, eti mijitu inapiga magoti kabisa kupokea buku buku
 
Hili tapeli lingine linadanganya wahindi kwamba linarefusha miguu, wakati jamaa amepindisha tu mguu wa kushoto ili wa kulia uonekane umerefuka, jinga kabisa..
 
Mchungaji awalambisha viatu waumini wake Ili wapate baraka za miujiza
1-jpg.720233

Mchungaji mmoja kutoka Nigeria (39), Andrew Ejimadu wa kanisa la Christ Freedom Ministries amezua gumzo mtandaoni baada ya ku-post picha zake katika mtandao wa Facebook wakati wa kuabudu mitandaoni.

Nabii huyo ameshangaza maelfu ya watu baada ya kuonyesha picha za waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake akidai kuwa kwa kufanya hivyo watapata baraka na miujiza.

Nabii huyo aliweka picha hizo katika ukurasa wake na kuandika.“Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.”

“Kitu cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” Andrew Ejimadu.

Mwaka 2016, Mchungaji Ejimadu alipamba vichwa vya habari na kushikiliwa na polisi nchini Zambia yeye na kaka yake, Cleopasa Ejimadu kwa kosa la kumbaka binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikwenda kwenye makazi yao kwa ajili ya uponyaji na kupata ushauri wa kiroho.
 
FRANCIS DA DON,
Baba fungua lako umewazi Bushiri acha akili Uchwara buku la bando yenyewe usikute unagongea Buda akili uchwara hizo [emoji23] [emoji23]
 
Mzee wa upako awatolea uvivu wanaojiita Mitume na Manabii

Copy and Paste kutoka FB page yake ...
Kwenye biblia utume na unabii ni miongoni mwa huduma kuu kubwa na tafsiri ya mtume ni mtu aliye tumwa na Mungu kuanzisha imani mahala ambako hakuna hiyo imani na sio kuanzisha zehebu.

Mfano ni kupeleka ukristo mahala ambako ukristo haupo hapo ndipo mtu ana sifa ya kuitwa mtume , sasa hawa watu wanao jiita manabii na mitume sikuhizi wanacho fanya ni kama kujenga msingi juu ya msingi wa mtu mwingine maana katika swala la mitume huku kwetu ile imani ilishaletwa tangia zamani na wale wa mishonari kipindi hicho imani ya kikristo haikuwepo.

watu wengi wanashindwa kufahamu hili swala kwamba uchungaji sio cheo ni huduma na kadhalika utume na unabii sio cheo ni huduma , mfano unaweza mkuta mtu anajiita mchungaji hata kanisa analo chunga waumini hana sasa hapo uchungaji uko wapi ? maana uchungaji ni maisha ya kila siku ya kuchunga waumini na kazi ya mtume ni kupeleka imani mahala ambako imani haipo .

Baadhi ya watu wanakimbilia kujiita mitume na manabii ili kucheza na saikolojia za watu maana hayo ni majina yenye utisho kwa mtu akiyasikia. Mungu atusaidie sana.
 
Back
Top Bottom