Nabii Bushiri aaibishwa na muigizaji aliyemlipa kutoa ushuhuda wa uongo stejini

Nabii Bushiri aaibishwa na muigizaji aliyemlipa kutoa ushuhuda wa uongo stejini

Wengi nyie mloleta hizo video kutoka youtube hamjui hata mnachojaribu kuongea,unachukua kipande cha video arafu unakuja kumsema mtumishi wa MUNGU,usiyoyajua usishadadie kuongea,mfatlieni huyo alieanzisha bushiri must fall ameishia wapi ? kwa taarifa yenu Prophet bushiri hategemei sadaka katika kuendesha maisha yake anaviwanda vya madini kamavile acacia na viwanda vya nguo vipo china amewekeza kwenye mahotel dubai,sio maskini kama wewe uliyeenzisha hii mada hapa
Team forex

Sent from my SM-G903F using JamiiForums mobile app
 
Inaniuma sana nikimuona mwafrika anawapiga wenzake pesa huku akijua maisha yetu watu wanakufa kwa njaa daah mungu atusamehe
 
Amkeni wabongo...enzi za miujiza zilisha pita acheni kuambudu watu na masanamu...naona mmesha anza kuingiliwa na upotoshwaji wa kinaigeria .....kweli wajinga ndio waliwao
Siku ukibanwa na lusfer na maajent wake utawatafuta watumishi wa Mungu wakufanyie maombi.
Huna ujanja ndg.
 
News Alert: - Shepherd Bushiri: Nabii kutoka Malawi anayedai kutenda miujiza na kuwavutia maelfu ya waumini -
Utapeli mtupu

Shepherd Bushiri: Nabii kutoka Malawi anayedai kutenda miujiza na kuwavutia maelfu ya waumini

Bushiri anasema utajiri wake unatokana na Biashara zake binafsi
Watu wanapiga makofi, wanacheza, kuimba na kuruka wakati akielekea kwenye ukumbi, akiwa amezungukwa na walinzi. Lakini kwa nini wasifanye hivyo?

Huyu ni mwanaume anayesema kuwa ana dawa ya walioathirika na virusi vya Ukimwi, HIV, anawaponya vipofu, maskini wanakuwa matajiri, na wakati mmoja hivi karibuni anadaiwa kuonekana akitembea hewani

Nabii Mchungaji Bushiri alizaliwa na kulelewa mjini Mzuzu kaskazini mwa Malawi.

Siku hizi, hujaza viwanja vya michezo kwa maelfu ya watu walio wafuasi wake, wafuasi ambao wako tayari kusafiri hadi popote pale duniani kwa ajili ya kumtazama akihubiri yeye mwenyewe.

Amekuwa akitembelewa mara kwa mara na wageni kutoka Marekani, Uingereza hata bara la Asia.

Leo Bendera zao zinapepea kwa mbwembwe ndani ya ukumbi wa kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG). Maana ya jina la kanisa hilo ni Mkusanyiko wa Wakristo Walioongoka

Nakutana na mtu huyu anayefahamika kwa jina ''Mkuu'' ndani ya Kanisa mjini Pretoria Afrika Kusini.

Tulipokewa kuelekea mahala patakatifu, pakiwa pametandikwa kitambaa chekundu na zulia jekundu pembeni wamejipanga walinzi.

Kumponya mlemavu

Mhubiri huyu mwenye miaka kama 30 na zaidi hivi anafahamu fika kuhusu shutuma dhidi yake baadhi ya watu wakimuita msanii na mhubiri bandia, lakini amekua akizipuuzilia mbali haya yote.

''Kanisa langu si kwa ajili ya kila mtu, isipokuwa kwa wale wanaoamini," alinieleza.

''Mimi ni mjumbe wa kazi ya Mungu. Mungu huwaponya watu kwenye kusanyiko letu''.

''Kuna siku nilikuwa na madaktari hapa Pretoria walileta watu wenye virusi vya Ukimwi, waliwapima kabla kuthibitisha kuwa wameathirika. Niliwaombea na sasa hawana virusi tena
Nje ya chumba, wafuasi wanakubaliana.

Wanaamini si tu mchungaji huyu kajazwa na nguvu ya utume, lakini pia ana nguvu ya kuponya wanaougua na kuwaombea watu kuwa na mafanikio.

''Miujiza na mafundisho ambayo baba yetu (Nabii Bushiri) hufundisha kila juma ni ya kustaajabisha,'' anasema Xolani Msibi
Alisema dada yake alikuwa na shida ya kutembea na kuwa aliponywa na nabii ''bila hata kumuwekea mkono''

''Mwenyewe nimekuwa nikihangaika kupata kazi na nilikuja hapa nikapata kazi mbili kwa wakati mmoja ilikuwa suala la kuchagua tu''.

Wahubiri wengine wanaodai kufanya miujiza

Wanawake na wanaume wanaodai kufanya miujiza hawako Afrika Kusini pekee au Afrika pekee-wanapatikana katika maeneo mengi duniani.

Benny Hinn, Kiongozi wa Kanisa la Israel lililo na makazi yake nchini Marekani,Grace Copeland na Rienhard Bonnke wa Ujerumani, hao ni wachache tu.

'Baraka zimewavuta wafuasi wangu'

Kwa siku ya kawaida, Jumapili kanisani kwa Bushiri, watu takriban 40,000 hukusanyika kumsikiliza Nabii akihubiri, kisha hununua bidhaa zinazouzwa kanisani kama vile'' mafuta ya muujiza', kalenda, vibandiko vya mkononi na taulo zeye picha, fulana na kofia, vyote vikiwa na picha ya uso wake.

Wauzaji huwaambia wanunuzi kuwa bidhaa zote hizo zimeombewa na Bushiri mwenyewe na vina nguvu ya uponyaji
Kwa miaka mingi Bwana Bushiri amejipatia utajiri mkubwa.

Vipi kuhusu wanaohoji amepata wapi pesa zote hizo?

"Ubaguzi wa rangi huo," anasema.


Shepherd Bushiri ni nani ?


Ni "nabii" mzaliwa wa Malawi aliye na makanisa mataifa mengi Afrika, miongoni mwake Ghana na Afrika Kusini
Anadaiwa kupigwa marufuku Botswana kutokana na "pesa za mwujiza"
Anadai kwamba amewatibu watu wenye Ukimwi
Alidaiwa kutembea angani kwenye video iliyosambazwa sana mitandao ya kijamii
Ana ndege nne za kibinafsi

Hakuna hasa rekodi ya utajiri wake wote lakini inafahamika amekuwa akipata faida kwenye migodi kadhaa na anamiliki ndege binafsi na hoteli kadhaa kwa jina la kampuni yake ya uwekezaji Shepherd Bushiri Investments, makao makuu yake yakiwa Johannesburg.

Suala la yeye kupata utajiri huo kwa madai ya ujasiriamali haliaminiki


Mwenyewe alisema ''Mimi ni mfanyabiashara. Hiyo ni kando na kuwa Nabii. Mafanikio yamekuja kutokana na biashara zangu binafsi.

"Maswali ya namna hiyo hayaulizwi viongozi wa makanisa ya Wazungu, lakini Mwafrika akifanikiwa ni tatizo."

Kisha kidogo anaonyesha kuchukizwa, anaongeza ''inakuwaje kuuza bidhaa kanisani mwangu iwe tofauti na kanisa katoliki kuuza Rozari na makanisa ya Uingereza kuuza Biblia? hii si sawa."

"Kufanikiwa kwangu ni kioo kwa wafuasi wangu. Wanafikiri kama Mungu anaweza kunitendea mimi, anaweza kuwatendea wao pia. Kama waliamini kuwa kuna shida kwenye hilo basi wasingenifuata''.

Kupokea vitisho

Amekuwa akipokea vitisho kwa wale wanaomuona kuwa mshindani wao, wengine wamekuwa na wasiwasi namna ambavyo watu wamekuwa wakitumia pesa kwenye kanisa.

Kumekuwa na sheria nchini Afrika Kusini kuhusu makanisa ya kisasa, nako nchini Botswana Kanisa la Bushiri limefungwa kutokana na kutumia ''pesa za muujiza'' ambako kunakiuka sheria za matumizi ya pesa nchini humo.

Thoko Mkhwanazi-Xaluva ni mkuu wa Tume ya kulinda tamaduni, dini na lugha ndani ya jamii. Hivi karibuni alitoa ripoti kuhusu kuchipuka kwa makanisa mengi ambayo yamekuwa maarufu barani Afrika.

"Tumegundua kuwa baadhi ya makanisa yamekuwa yakijipatia faida kutokana na bidhaa za imani zinazonunuliwa na watu maskini wenye shauku ya kubadilisha maisha yao kuwa mazuri," anaeleza


Ripoti hiyo imeeleza zaidi kuwa kuna vitendo vinavyofanywa visivyo salama kwa waumini kama vile kula Panya, Nyoka, Majani na kunywa mafuta ya petroli kuwapima imani yao.

Pia kumekuwa na shutuma za udhalilishaji wa kijinsia kwa baadhi ya makanisa.

Hata hivyo Mkuu huyo anasema suala la dini ni uamuzi wa mtu mwenyewe

Chanzo Bbc swahili


 
OMBI: Makanisa uchwara yafungiwe

Wakuu habari...
Ukweli ni kwamba katika nchi yetu ya Tanzania kumekuwa na utitiri wa makanisa yani kila uchochoro unaopita kuna kanisa uchwara.

Pamoja na manabii hao matapeli ila wapo ambao wao sio matapeli wamekuwa wakiifanya kazi ya Mungu.

Ila manabii feki ni wengi mno wamekuwa wakiibuka kila uchao na lengo lao tu ni kuwalaghai wananchi kuchukua hela zao wakidai watapokea miujiza.

Wamefanya watu wamebweteka hawafanyi kazi wakisubiri miujiza, wengine pesa zinaishia kwa manabii na wengine wameharibu ndoa zao kisa hao manabii feki.

Hivi karibuni nimeona wenzetu Rwanda wameanza kufungia makanisa uchwara naona ni jambo jema.

#manabiifekiwafungiwe#
 
Ona hili tapeli lingine, eti linaweka microphone pembeni na kumwambia muigizaji aliyemlipa "Lia kwa nguvu..piga kelele..", na hapo hapo muigizaji anajiangusha na kupiga kelele, teknolojia inazidi kuwaaibisha hawa matapeli, tuko pamoja katika kudhihirisha utapeli huu. Halafu anasema "msimamishe", lakini cha ajabu ananyanyuka mwenyewe ghafla..badala ya kuinuliwa, hahahah..


Huyu ni mchekeshaji tu kama nabii Tito
 
Lugha bana. Hajui kingereza vizur so ana jichanganya
 
Usiwahukumu , hao waumini na Kuwaita wajinga , huenda hata na wewe ni mjinga kwa hapo unapo abudu, omba mwenyezi mungu aturehemu ,na atujalie mwanga wa roho mtakatifu , maana alisema kutakuwa na manabii wa uongo ,, like Elijah did at Mt Carmel for the false prophet.

Amwombe MWENYEZI MUNGU
ATUREHEMU
na atujaalie MWANGA WA ROHO MTAKATIFU

Haya tufafanulie hio sentensi yako huyo ROHO MTAKATIFU NDIO NANI,!!!???
Ukijibu ntajua nyinyi sio wakuitwa wajinga
 
Back
Top Bottom