Nabii Geor Davie rekebisha fundisho lako la uongo!

Nabii Geor Davie rekebisha fundisho lako la uongo!

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Huwa nafuatiilia mafundisho yako redioni kuona nini unafundisha. Jana kuna mafundisho kuhusu amri ipi iliyo kuu umeteleza. Jibu la Yesu ni: KATIKA AMRI HIZI HUTEGEMEA TORATI YOTE NA MANABII. Wewe umetoa tafsiri potofu (really very bad hermeneutics, sijui kama ni makusudi tu ili kujiuza au ni bahati mbaya), kwamba ati amri ya mapendo hutegemea anachosema nabii. Hii si sahihi.

Yesu alimaanisha yote yaliyoandikwa katika vitabu vya torati na manabii ambavyo wakati ule Wayahudi walikuwa navyo msingi wake umejengwa kwenye amri ya UPENDO. Usifanye promotion ya huduma yako kwa kugeuza tafsiri za maandiko na kutumia uelewa finyu wa waumini wako. Kuna vipindi vya maswali na majibu ulikuwa ukifanya vizuri lakini nataka kukurekevisha unapoanza kuwapoteza watu.

Fundisho kama la jana na mengine nitakusahihisha maana hata hiyo shahada yako ya uzamivu (Ph.D) naanza kuitilia mashaka. Hata tafsiri ya biblia ya kiingereza ya hiyo aya haiendani kabisa nawe na naona kila mara ukiwapotosha watu kufanya promotion ya cheo cha nabii. Correct yourself or else you will face God's judgment.

Kuna wakati pia uliongelea habari ya Ibrahim, tajiri na masikini Lazaro. Yesu aliposema WASIPOWASIKILIZA MUSA NA MANABII alimaanisha yale ambayo tayari yalishaandikwa kwenye maandiko ya Agano la kale na siyo manabii hawa wa mchongo wa enzi zetu!
 
Mkuu unapoteza muda, huyo nabii wa uongo anajua anachofanya kupotosha
kwani hukumsikia akokosoa biblia yenyewe akisema, biblia haiko sawa, hivyo ukimuambia afuate biblia anakuuliza biblia ipi?

kwahiyo haiamini biblia na hii ameamua makusudi ili asikosolewe kwa kutumia biblia
 
Jamaa ana mafundisho ya kujipa ujiko tu. Naona humo kanisani kwake hakuna watu wenye elimu ya maandiko matakatifu kwa hiyo wanaburuzwa tu!
Muacheni ajipakulie minyama, tena huyu mtanzania mwenzetu siyo yule mkongo.
 
Huyu si ndiye aliyemwambia MilardAyo kua alitokewa na Yesu physical na wakapiga story mbili tatu?
 
mkuu unapoteza muda, huyo nabii wa uongo anajua anachofanya kupotosha
kwani hukumsikia akokosoa biblia yenyewe akisema ,biblia haiko sawa, hivyo ukimuambia afuate biblia anakuuliza biblia ipi
kwahiyo haiamini biblia. na hii ameamua makusudi ili asikosolewe kwa kutumia biblia
Asante kwa mchango wako. Lengo langu ni kuwanasua hawa wanaomwamini wajitambue. Wanakokotwa tu kama kondoo kupelekwa machinjoni.
 
Hakuna fundisho la kweli.

Hata huyo Yesu mnaye hubiriwa habari zake kila kukicha ni UONGO.

Huyo Yesu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Huwa nafuatiilia mafundisho yako redioni kuona nini unafundisha. Jana kuna mafundisho kuhusu amri ipi iliyo kuu umeteleza. Jibu la Yesu ni: KATIKA AMRI HIZI HUTEGEMEA TORATI YOTE NA MANABII. Wewe umetoa tafsiri potofu (really very bad hermeneutics...
Mshaanza kutambuana huko
 
Jamaa ana mafundisho ya kujipa ujik wao tu. Naona humo kanisani kwake hakuna watu wenye elimu ya maandiko matakatifu kwa hiyo wanaburuzwa tu!
Waamini wake akili zao zishatekwa...
Hawana fikra

Ova
 
mkuu unapoteza muda, huyo nabii wa uongo anajua anachofanya kupotosha
kwani hukumsikia akokosoa biblia yenyewe akisema ,biblia haiko sawa, hivyo ukimuambia afuate biblia anakuuliza biblia ipi
kwahiyo haiamini biblia. na hii ameamua makusudi ili asikosolewe kwa kutumia biblia
Hakunaga Nabii wa ukweli.

Hata huyo Yesu mwenyewe ni Uongo.
 
Back
Top Bottom