Nabii GeorDavie: Yesu akirudi leo atataka kutumia gari yangu na atataka nimfuate Airport

Huu ni moja ya mifano hai inayodhihirisha upungufu mkubwa wa akili kwa kila mtu/jamii inayowaamini hawa WENDAWAZIMU,na kukubali kuongozwa nao kiroho.
Sasa waone namna wanavyoongozwa KUMWABUDU na KUMTUMIKIA Shetani waziwazi.
 
Atakuwa anamaanisha Yesu yule mchezaji wa kabumbu.
 

Nabii Geordavie​

Akili kubwa hii
Vilaza wafia dini hapo ni povu kwa kwenda mbele .....
 
Yaani nimesikiliza hayo maongezi huyo na bii ni tapeli asiye kuwa na shukurani . Anakula na kuvaa na kuendesha magari yanayo tokana na sadaka za mafukara huku akiwakejeri kuwa sadaka zao hazitoshi kununuwa kiatu chake. Hata maongezi yake hana mvuto kwa sababu ni fake kuanzia sauti mpaka kicheko. Halafu ni shamba anafikiri kutabiriwa na mzungu ndio ujaja. Pia uso wake na mikono yake utafikiri ni watu wailwili tafauti . Anatumia mkorogo?
 
Hawa manabii na mitume feki ni wapotoshaji sana wa imani kwa wasiojua vema neno la Mungu
 
Nyinyi wafia dini hamtamulewa...
Ana IQ above average mbongo.....
IQ kubwa kiasi gani pale kama si kulaghai watu wenye low IQ? Eti Yesu akija atapanda gari lake! Is he serious?
 
Amini usiamini, anapata waumini!
 
Yesu yuaja katika utukufu mkuu kuhukumu ulimwengu. Kama unatarajia kumwona Yesu mwenye madevu; Yesu mvaa kanzu; Yesu mpiga paji la uso chini hadi kovu jeusi tii utasubiri sana. Mwapotea kwa kukosa ufahamu na maarifa.
 
kYesu yuaja katika utukufu mkuu kuhukumu ulimwengu. Kama unatarajia kumwona Yesu mwenye madevu; Yesu mvaa kanzu; Yesu mpiga paji la uso chini hadi kovu jeusi tii utasubiri sana. Mwapotea kwa kukosa ufahamu na maarifa.
kwa hiyo atakaporudi ataachana na Ibada aliyokuwa akiifanya hapo kabla halafu ataiga ibada za wazungu?au ataenda kusali na Viongozi wa dini wanaosapoti ndoa ya jinsia moja?mda mchache mambo mengi
 
Wandugu, ukisoma Mathayo 24, mstari wa 1-44, utagundua Yesu alieleza kwa kirefu sana majira yanayokaribia kuja kwake. kutokea kwa manabii wengi wa uongo, vita mahali mahali n.k, na kwamba kuja kwake kutakuwa kwa ghafla, kama umeme utokeavyo mashariki ukaonekana magharibi, ndivyo itakavyokuwa. Manabii wa uongo wapo wengi sana.

kuan watu hawaelewi jambo hili, hapa duniani tunatembea na wanadamu wengi tu ambao ni nusu mtu nusu shetani, walizaliwa hivyo, hao hata watubu vipi hawasamehewi kwa sababu walishahukumiwa, sehemu yao ni ktk ziwa la moto na baba yao shetani, na shetani anawatumia kama maajenti wake kufanya yale anayotaka dhidi ya kanisa. ndio maana wanaweza kufanya makufuru, kupotosha injili, kujitajirisha na kutapeli, wapo tu, walishatabiriwa.

Ndugu zangu, tujiandae, ujio wa Yesu hatakuja kama mwanzo,

MATENDO 1:11, Yesu alipokuwa anapaa mbele ya machi ya mitume wake, alikuwa anapaa kwenda mbinguni. Malaika walisimama karibu yao wakwaambia,. Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Kama alivyopaa, ndovyo atakavyoshuka. hawezi kushuka akafikia airport akahitaji huyu mhubiri aje amchukue kwa gari yake iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…