Nabii Geordavie amesema kwamba endapo Yesu angerudi leo, angehitaji kutumia gari lake na kumtaka amfuate uwanja wa ndege kwa ajili ya msafara wa hadhi yake. Nabii huyo alieleza kuwa Yesu angekuwa na mtazamo tofauti, akiamua kukaa naye na kuchagua gari miongoni mwa alizonazo ili kuendana na hadhi yake.
"Nadhani atakuwa na mtazamo tofauti, jambo la kwanza ataamua kukaa na mimi na atataka kutumia gari langu, atachagua katika hizi (gari) na ataomba nimfuate airport (uwanja wa ndege) kwasababu ndio hadhi yake na kutakuwa na msafara kabisa."
Wandugu, ukisoma Mathayo 24, mstari wa 1-44, utagundua Yesu alieleza kwa kirefu sana majira yanayokaribia kuja kwake. kutokea kwa manabii wengi wa uongo, vita mahali mahali n.k, na kwamba kuja kwake kutakuwa kwa ghafla, kama umeme utokeavyo mashariki ukaonekana magharibi, ndivyo itakavyokuwa. Manabii wa uongo wapo wengi sana.
kuan watu hawaelewi jambo hili, hapa duniani tunatembea na wanadamu wengi tu ambao ni nusu mtu nusu shetani, walizaliwa hivyo, hao hata watubu vipi hawasamehewi kwa sababu walishahukumiwa, sehemu yao ni ktk ziwa la moto na baba yao shetani, na shetani anawatumia kama maajenti wake kufanya yale anayotaka dhidi ya kanisa. ndio maana wanaweza kufanya makufuru, kupotosha injili, kujitajirisha na kutapeli, wapo tu, walishatabiriwa.
Ndugu zangu, tujiandae, ujio wa Yesu hatakuja kama mwanzo,
MATENDO 1:11, Yesu alipokuwa anapaa mbele ya machi ya mitume wake, alikuwa anapaa kwenda mbinguni. Malaika walisimama karibu yao wakwaambia,.
Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Kama alivyopaa, ndovyo atakavyoshuka. hawezi kushuka akafikia airport akahitaji huyu mhubiri aje amchukue kwa gari yake iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.