Nabii Hakubaliki Nyumbani! Godbless Lema ni Nabii? Alianza na Ndoto, Ikatimia!, Akaja na Sabaya, Ikatimia!, Sasa ni Makonda, Itatimia? Asipuuzwe!

Lema kashamfanyia unabii Mama pia,naye ajiandae au ajirekebishe.
 
Mkuu Paskal, Lema hana salama pia- mwizi tu- watakutana huko wakamalizane
 
Itatimia hata P analijua hilo.
 
Mkuu Paskal, Lema hana salama pia- mwizi tu- watakutana huko wakamalizane
Rekebisha kidogo, sio ni mwizi, bali zamani anasemekana alikuwa mwizi wa magari, lakini sasa sio mwizi tena. Hata Mtume Paulo, hakuwa miongoni mwa wale mitume thenashara, alikuwa Saulo na aliwatesa sana Wakristo, mpaka siku Mungu akamtokea kwenye njia ya Jericho, ndipo akabadili jina kuwa Paulo.

Uzuri wa karma is reversible, ukitenda maovu, ukajitambua umetenda uovu, ukajuta, ukabadilika na kuanza kutenda mema, yale mema yako, yanafuta yale maovu yako, unatakasika, na mema yakizidi yale maovu, unabarikiwa. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!

Hivi ndivyo ilivyotokea kwa JPM hadi saa hizi yuko peponi, mbinguni kwa Baba yake, yuko na Baba yake!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
 
Karma is betch wakati wa bwana ni wakati sahihi not my word
 
Narudia kuwakumbusha Makondanyo ni Dekio ni muda unasubiriwa huyo atakufa kwa njia ya mateso makubwa sana
 
Itatimia hata P analijua hilo
not necessarly,ukifanya maovu, ukajitambua umefanya maovu,ukajuta na kuomba msamaha, hata kimoyomoyo, kisha ukatenda mema kuufidia uovu wako, unasamehewa,hivyo nimemshauri asipuuze,its not too late kuomba msamaha,hajachelewa,ila wahusika wakuu, karma imeisha shughulika nao!。

P
 
Ni heshima kwa Mungu kumzomea fisadi Lowasa ~~~ Nabii Lema

Nabii uchwara aliyeshindwa kuacha legacy yoyote Arusha, pia ameshindwa kuongoza kanda ya kaskazini vijana wamemgomea.

Mke wa Lema analelewa na nani Canada?
Acha wivu unaulizia mwenzako analelewa na nani unataka uchukue nafasi yake.
 
Bado wapo ambao karma inahitaji kushulikiwa,na sii kila kosa linasamehewa hasa ya kukusudia kama yale kama, ukisha hesabu kura unasema mungu ni samehe.
 
Toka alipotoa ile kauli ya kusema mama ntilie ni laana,bodaboda ni laana,Nicola ni laana basi nimetokea kumwona chizi flani ndani ya Tanganyika na ana impact yoyote kwenye siasa na jamii kwa ujumla.
Hivi Kuna nabii alianguka/kosea kusema katika kutekeleza kazi zake?
 
Godbless Lema,anajitambua!。
Baada ya Mama kuwapelekea moto Arusha,mtu yeyote anayejitambua hawezi kucheza na Moto!。
Gambo naye ajiangalie na kujitathmini!。
P
 
Namshauri Freeman Mbowe,auzingatie sana ushauri wa Lema,amoishe Lissu kwenye usukani Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…