Nabii Malisa aelezea jinsi alivyomfufua mama yake mzazi mara 3

Sijawahi kuziamini hizi dini zilizoletwa na ngozi nyeupe
 
Wife alianza kuabudu katika haya makanisa ni kampiga STOP kubwa.alikuwa anatumia mafuta ya mwamposa kila nikilala ananimwagia maji kitandani nikasema uyu anaweza kunifanya zombie bure ngoja nimuwahi.

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Nilienda family Moja nikakutana na hayo maji ya upako ya mwamposa Kwa kuwa ni mgeni sikubisha kabula hujalala Wana kumwagia Daah
Kwa watu ni Kwa watu ndio maana Kila mtu akae kwake nilienda Kwa mjomba ana uwezo mkubwa tu kifedha ni kiongozi wa kanisa nikaona niende kwake nokatafute maisha Nikakaribishwa vizuri mno Wanasali hasa.

Wakanionyesha ratiba ya maisha Yao ya Kila siku .Inasomeka hii ndio ratiba ya siku za kula

Jumapili tunakula ,Jumatatu ni siku ya kufunga na kuomba Jumanne tunakula ,Jumatano tunafunga na siku ya Alhamisi tunafunga ijumaa tunakula Jumanosi tunafunga jumapili tunakula

Nilikaa wiki moja nikarudi kijijini mkoani nilikotoka nilikoaga Kwa Mbwembwe kuwa mimi maisha ya kijijini basi Kwa heri ya kuonana
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mambo ya imani hayo hayahitaji akili kubwa kuyang'amua. Hata Gwajima alijaza sana watu miaka ile kwa uwezo wa kufufua misukule. Watu wakapinga kuwa kamwe hawawezi amini ujinga ule.

Akaja kuomba kura kwa wanakawe. Kuna baadhi ya watu wakampa jumlisha za wizi.

Video yake ya connection kuna waumini wake hadi leo wanapinga kuwa sio yeye. Waliionaje. Usiniulize

Wajinga hawajawahi kuisha ndio maana CCM ipo hadi leo inadunda tu. Wanaanzaje kuzuia hayo makanisa. Wajinga ndio mtaji wa CCM
 
Yaani umejua kunichekesha Leo [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji28][emoji28]
 
Du huu ni UTAPELI babu kubwa. Ni zaidi ya Gwajima kufufua miskukule kwenye kanisa lake la mchongo.
 
Afu kuna wanawake hapo mbele wanashangilia balaa. Sijui wanakuwa wanapangwa? Lakini kuna mmoja nimemuona akishangaa kwa kumtilia mashaka huyu tapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…