Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Mkuu Pascal, herufi kubwa au ndogo ni utaratibu tu wa kiuandishi ila hauhusiani kabisa na nguvu au mamlaka ya kitu. Kwamba ukiandika Mungu/Yesu hapo ndio utukufu wake na nduvu wake zinakuja ila ukiandika mungu/yesu basi umebadilisha maana?[emoji23][emoji23]. Na je ukiandika MUNGU/YESU wanakua na mamlaka na nguvu mara 2 zaidi?

Na wewe pia umevutika kudanganyika kwenye kuhusisha mamlaka ya kitu na uandishi wa herufi. Okay, tuseme iko hivyo, je nikitamka pia itatofautisha?

Tuendelee kuomba haka kagonjwa kapite.
Paskali yuko sawa
Mungu na mungu ni vitu viwili tofauti sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali
Asante kwa kuleta hili hapa, binafsi huwa naogopa sana kujadili mambo yawahusuyo watumishi wa Mungu au wapakwa mafuta wa Bwana.
Tuanze na Corona...this is real na haitakiwi kufanyiwa mzaha wa kinabii. Sayansi haina unabii zaidi ya kufanya sanaa.
Pia naomba kudeclare kuwa mimi niko Mwanza ambako nabii Malisa kaanzia. Sitaki kujiingiza kuhusu ni Mungu gani anamtumikia hilo anajua yeye na Mungu wake. Naomba nijikite tu kwenye huo unabii anaouleta, nabii huonyeshwa yajayo sio yaliyopo...alitakiwa aje na unabii kabla Corona haijaanza na apewe suluhisho. Unabii gani huu hapa ni mtu anaangalia tu alama za nyakati kuwa hata ikienda sana haiwezi kulast long, lakini kusema huo ni unabii...labda Mungu wake anajua. Na kuhusu watu waliopiga simu na kupewa unabii on the spot,nikukumbushe tu miezi sio mingi South Africa mtumishi wa Mungu alimfufua mfu na matokeo yake tunayajua kwa hiyo hiyo ya watu kupiga simu is not a big deal. Japo sikatai manabii wapo but this is too cheap to be bought.
Corona is real nirudie tena,tukisikiliza hasa manabii tutaishaa...kwa nini haiendi walikolazwa wagonjwa akapige maombi ya kuzuia vifo?
Na je,kanisani kwake wamewela ndoo za maji na sanitizer? Kama wameweka ni kwa ajili ya nini wakati Mungu kamwambia hakuna kufa tena?
Watanzania tufuateni maelekezo ya watalaamu wa afya na wasemaji wenye dhamana ya kusemea gonjwa hili.
Hivi kwa hiyo airtime aliyopewa na kutizamwa na watanzania mamia kwa maelfu,akiaminiwa tutapata athari kiasi gani? Maana watu wataamini hakuna vifo na corona mwisho April,si wataachana na tahadhari zozote?
Serikali imuite na arudishwe WasafiTv akanushe kama yule anaitwa Mashimo aliedai anadawa kwa kuitangaza youtube na baadar kukanusha yeye mwenyewe...
Hii ni sanaa...watumishi wanashauri kusikiliza wataalamu huku wakimwomba Mungu kuliepusha hili balaa na si hii sanaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Manabii na mitume wa kilokole wanapenda sana kutumia fursa za matatizo ili wapate pesa na wafuasi, na ukiangalia waumini wengi wa kilokole uwelewa wao uko chini sana haijalishi amesoma ana madigrii au cheti au hana, wao wanachoambiwa na kiongozi wao ndo wanachokariri hata ukitaka kuwaeleza ukweli wa jambo mtabishana sana, nimeona hata huko USA wahubiri mwanzoni corona ilivyoingia huko kwao walijifanya kujigamba kuwa haitapenya lakini Leo matokeo tnayaona katika TV zao huko.
Viongozi wa dini wakubali tu kuwa corona ni hatari na haiponywi kwa maujiza za madhabauni, wawaelekeze waumini wao kusikiliza maelekezo ya wataalamu wa afya.
 
Mzee pasco unaonesha ni kwa namna gani mmegawana madaraka na mkeo, unaruhusu decision making regardless Utumi wa kisukuma na mamlaka ya wanaume tuliyopewa na Mungu over wanawake.

Stesheni karibia zote hazifuati maelkezo ya mamlaka. Mwanzo niliwahi shauri, vipindi visivyo vya lazima hasa michezo au vyovyote visitishwe kwa sasa.

Nabii Malisa, sijawahi mfuatilia na simjui lkn uhuru huu wa maono sidhani hata yesu aliwahi fanya! Kuhusu corona, ni trending reading capacity kama uliyonayo wewe kwenye siasa. Kulingana na tamko la WHO, ibada na misa za Pasaka na kauli za wakuu wa nchi inaonesha hivyo kulingana na maoni yake ; huo si unabii pasco.

Pilau inanukia jikoni
 
Atageuza atasema mungu alisema april mwakani sio mwaka huu, kama anahisi corona itaisha ndani ya wiki tatu ana matatizo ya akili
 
Kwanza eti anataka aombwe, anyeyekewe, atukuzwe, abembelezwe ndio atende.Baada kujinyeyekeza, kumbembeleza na kumtukuza hakuna alichoweza kufanya wala kutenda. Ni vituko.

Alishaombwa, alishabembelezwa, alishanyeyekewa na kusujudiwa miaka na miaka hakuna alichowahi kufanya hata kimoja. Huu ni ushahidi wa wazi kua kilichoandikwa kwenye vitabu vinavyoitwa vyake ni hadith tu za alinacha na wala kitu kama hicho hakipo.
Rias uko wapi kufunga jela hawa wanaomdharau mungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo nabii mwongo Sana N tapeli kama wengine. ..siku moja nilialikwa kanisani kwake akaja kuniombea.. Eti kaniambi Mungu amenionyesha unaKwenda kupandishwa Cheo kazini unapofanya kazi. ..baada ya Hapo akaniuliza unafanya kazi wapi Nikasema mi mfanyabiashara.. Akasema basi utapata sijui wateja blabla.. Nkahisi sound tu.. Hata hao wanaopiga simu Kuna possibility Kubwa ni Watu wake kawaseti.. Kama nabii kweli aende mloganzila akuponye wenye corona wote. Huyo nabii ni fake.. Kwanza analink na nabii mwingine Yuko south naye anakuinua fake kibao.

Sent using Jamii Forums mobile app
ualikwe kwenda kanisani punguza basi uongo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Heri ya Pasaka.
Naangalia Live ya Pasaka kwe Wasafi TV, kipindi kinaendeshwa na Mtangazaji mahiri Lilian Mwasha ila kiukweli somo la social distancing bado halijaeleweka. Kama hii ndio media iliyopaswa kuonyesha mfano wa social distancing, lakini wao ka Studio kadogo wanarundikana watu 14!, safari bado ni mbali!.

Naomba kukiri leo ndio mara yangu ya kwanza kumsikia mtangazaji huyu na kuiangalia Wasafi TV siku ya Jumapili asubuhi, huwa naangalia Chomoza kumsikiliza Dr. Ellie. Mimi kwa agewise ni 50+, hivyo kuna ile natural conservative opinion kuwa kuna TV za wazee, kuna tv za watu wazima, kuna TV za vijana na kuna TV za watoto depending on seriousness of contents, Clouds TV, TVE na Wasafi TV, nilizihesabu ni TV za Vijana, hivyo huwa sizifuatilii sana, ila leo wife amengangana nimejikuta naangalia Wasafi TV.

Kipindi cha leo, Studio za Wasafi TV, wamealikwa wanamuziki wa kundi la The Voice, John Lissu, Masanja Mkandamizaji, na Nabii kijana anaitwa Malisa, kiukweli huyu dogo ametisha!.

Akiizungumzia Corona, Nabii Malisa amesema Mungu amezungumza nae kwa maneno ya unabii wa Corona, Mungu amemuonyesha kuwa mwisho wa janga la Corona, mwisho ni Mwezi huu April, kuanzia mwezi May, hakutakuwa na ugonjwa wa Corona tena, na kuanzia sasa hakutatokea tena vifo vya Corona nchini Tanzania, hata hivyo vifo vya Corona vilivyotokea, the cause sio Corona bali ni matatizo mengine ya kiafya ya watu hao ambayo hayakutajwa, hivyo Corona imewasindikiza tuu, kwani tayari waliishakuwa wako njia moja, hata bila ya Corona, ilikuwa safari!.

Kwanza hiki wanachokifanya studio ya Wasafi kwenye janga hili la Corona, is not right, hakuna any social distancing, wameleta kundi kubwa sana watu 14 ndani ya ka studio kadogo!, tushukuru uwepo wa Mungu mahali hapo, lakini ikitokea kuna mmoja hapo ana Corona, ni hatari sana hiki wanachofanya.

Pia anachokifanya Nabii huyu is it right?, kusema definite Corona mwisho April na hakuna tena atakayekufa kwa Corona Tanzania, live on TV?.

Kiukweli huyu Mtangazaji Lilian Mwasha is so good, ana maswali yenye akili, amempigia simu Apostle Daniel Maboyo akizungumza kutoka Arusha, akamuuliza, Tanzania kuna wahubiri wengi wa miujiza ya uponyaji tunawaona kwenye TV mbalimbali wakifanya mambezi ya uponyaji na miujiza ya uponyaji, sasa dunia na Tanzania tumekumbwa na janga la hili gonjwa la Corona, mbona hawa wahubiri hawafanyi maombezi ya kuponya Corona?, mbona hawaendi kuwaombea wagonjwa wa Corona wakaonyesha hiyo miujiza yao ya uponyaji?!.

Apostle Daniel Maboya, mezungumza jambo la msingi sana kuwa Corona ni ugonjwa wa ukweli haihitaji kuufanyia longolongo za uponyaji, amewataka Watanzania tusikilize maelekezo ya viongozi wetu wa serikali na maekezo ya kitaalamu na kumuomba Mungu atuepushe.

Simu zinapigwa watu wanaongea na Nabii Malisa anawafanyia unabii live on TV!. Kama hizi simu zinazopigwa sio arranged or premeditated, then huyu Nabii Malisa anatisha sana kwa jinsi anavyowafunulia hao wapiga simu kuhusu maisha yao, hadi watu wanalia!.

If you have time, please Watch
Pasaka Njema.
Pasakali
Asante kwa kutujulisha habari za hao manabii. Wanaosoma maandiko hawatikiswi na habari za kuokoteza nje ya maandiko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro gwajizo nae alipoulizwa juu ya kwanini yeye kama mtenda miujiza anaeweza kufufua watu kama kauli mbiu ya kanisa lake (ufufuo na uzima) inavyojinasaba, kwanini asitende miujiza yake kwa wagonjwa wa corona? Alichojibu.. zilongwa mbali! Zitendwa mbali! Kajisemea mzaramo.
 
Waumimi wengi wa dini hua sio wazima kichwani.

Utashangaa leo watu wameenda kanisani kumuomba mungu ambae ameshindwa kuondoa corona.

Mbaya zaidi utakuta kuna wengine wamefiwa na ndugu zao sababu ya corona na bado wanaenda kumuomba Mungu, sasa sijui wanaenda kuomba kitu gani? Unaenda kuomba kitu kisicho na msaada kwako?

Tuendelee kuomba haka kagonjwa kapite.
Hii sentensi yako ya Mwisho, unataka tumwombe nani sasa ili haka kaugonjwa kabite???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom