Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Najitahidi kuishi imani ambayo inanisukuma 'to do everything as if God does not exist, but in the background I know that he exists'. Hivyo, almost always namwomba Mungu anijalie kile anachoona yeye kinafaa kwangu na siyo ninachoona kinafaa na pia anijalie muda na wakati anaoona unafaa na siyo ninaoona unafaa. Haya maombi mengine na unabii wa kupiga ramli huu 'mimi simo'.
Mkuu Mseminari Telesphore, japo nuanga mkono hoja yako ya unabii wa kupiga ramli, ila kiukweli dogo, ame ni impress sana, unabii wake sio wa ramli chonganishi, huyu kila anayemtabiria ni kumfungulia toka vifungo vya shetani ni kuwatabiria neema.
TCRA: Vipindi vya Mahubiri Kwenye TV Pia Viangaziwe/Vithibitiwe!. Mungu Yupo Ila pia Shetani Yupo! - JamiiForums
P
 
Hivi kumbe vijana huwa mnamchezea sharubu mzee wa watu kwa kumuona kijana mwenzenu na kumwambia mnachojisikia kumbe mzee wa watu yuko kwenye miaka yake 50+ huko.
 
Huyo naona ameenda mbali.

Yupo mmoja huku kwetu Arusha yeye baada ya kuona Nchi zinazoripoti visa zinaongezeka, kwenye tarehe za mwanzoni za mwezi march akatangaza unabii kuwa corona itaingia na Tanzania.

Kwa hivi sasa Waumini wake wanasheherekea kutimia kwa unabii huku Wasaidizi wake wakihimiza utoaji wa sadaka lukuki kama sehemu ya kupongeza unabii huo.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waumimi wengi wa dini hua sio wazima kichwani.

Utashangaa leo watu wameenda kanisani kumuomba mungu ambae ameshindwa kuondoa corona.

Mbaya zaidi utakuta kuna wengine wamefiwa na ndugu zao sababu ya corona na bado wanaenda kumuomba Mungu, sasa sijui wanaenda kuomba kitu gani? Unaenda kuomba kitu kisicho na msaada kwako?

Tuendelee kuomba haka kagonjwa kapite.
Umeongea kama mtu mzima, mwenye afya,asiye na njaa na ambaye anaamini Mungu hayupo. Kiburi cha uzima kinatia moyo ujasiri wa kijinga.Mwanadamu ni mortal kufa ni lazima.Namna ya kufa na muda ndio tofauti.

Mimi binafsi siamini unabii na maneno ya Malisa, ni utapeli uliozoeleka kwa wenye vikanisa vya kupiga pesa.Tunaoamini juu ya uwepo wa Mungu tunaamini kuwa anaaweza kutenda apendavyo yeye na hapangiwi muda wala namna ya kutenda.
 
Mkuu P,
Kamdesea nabii fulani huko Nigeria, alisema CORONA itaisha 27 March, tarehe ilipopita alipohojiwa vipi? Akawaambia alisema 27 March hakutaja mwaka..😀

Sasa huyu Malissa, ikifika July, akiulizwa naye atasema hakutaja mwaka..muda ni mwalimu..

Everyday is Saturday........................😎
 
Umeongea kama mtu mzima, mwenye afya,asiye na njaa na ambaye anaamini Mungu hayupo. Kiburi cha uzima kinatia moyo ujasiri wa kijinga.Mwanadamu ni mortal kufa ni lazima.Namna ya kufa na muda ndio tofauti.

Mimi binafsi siamini unabii na maneno ya Malisa, ni utapeli uliozoeleka kwa wenye vikanisa vya kupiga pesa.Tunaoamini juu ya uwepo wa Mungu tunaamini kuwa anaaweza kutenda apendavyo yeye na hapangiwi muda wala namna ya kutenda.
Kiburi cha uzima ndio kitu gani? Kwa akili yako unadhani watu hawaoni kama Mungu hayupo kama kama wana njaa ama wanaumwa?

Hivi toka corona imeanza bado mungu hajapata muda wa kutenda? Ama toka ukimwi, ebola vimetokea Mumgu bado wakati wake wa kutenda haujafika? Sababu ni moja tu, hakuna cha muda wala nini, hayupo na kama yupo basi hana uwezo wa kutenda na hasikii. Mnaoomba mnapiga kelele tuu na kupoteza muda wenu. Mtapiga kelele sana na mtakufa na maombi yenu hayajajibiwa

Unataka kusema matumaini kwa Mungu ni pale tu una njaa, una magonjwa ila kama ni mzima Mungu hana mana tena?
 
Kiburi cha uzima ndio kitu gani? Kwa akili yako unadhani watu hawaoni kama Mungu hayupo kama kama wana njaa ama wanaumwa?

Hivi toka corona imeanza bado mungu hajapata muda wa kutenda? Ama toka ukimwi, ebola vimetokea Mumgu bado wakati wake wa kutenda haujafika? Sababu ni moja tu, hakuna cha muda wala nini, hayupo na kama yupo basi hana uwezo wa kutenda na hasikii. Mnaoomba mnapiga kelele tuu na kupoteza muda wenu. Mtapiga kelele sana na mtakufa na maombi yenu hayajajibiwa

Unataka kusema matumaini kwa Mungu ni pale tu una njaa, una magonjwa ila kama ni mzima Mungu hana mana tena?
Kwako hayupo,na hatendi hakuna cha kubishania hapo.wewe unaamini hivyo na mimi naamini kinyume chako hatuwezi kufikia mwafaka.
 
Kusema kutokuwepo ni vifo mwezi wa Aprili sio update hiyo P
Sent using Jamii Forums mobile app
No sio update. Update ni
  1. Corona status ya Maambukizi in Tanzania
  2. Idadi ya wagonjwa wapya
  3. Idadi ya waliokufa
  4. Idadi ya waliopona
  5. Idadi ya wanaendelea na matibabu
  6. Idadi ya tested
  7. Idadi ya walio kwenye quarantine
  8. Jumla kuu ya wote.
Kuendelea kuhimiza njia za kujikinga sio update
Viongozi wa dini kuwapa matumaini waumini wao kuwa Corona sio ugonjwa ni shetani tuu, tumemkabidhi Mungu sio update.
Nabii Malisa kusema Mungu amemwambia Corona mwisho April, kuanzia May hakuna tena Corona na hakuna atakayekufa sio update
P
 
Siyo nabii sema anaejiita nabii
Wanabodi,
Heri ya Pasaka.
Naangalia Live ya Pasaka kwe Wasafi TV, kipindi kinaendeshwa na Mtangazaji mahiri Lilian Mwasha ila kiukweli somo la social distancing bado halijaeleweka. Kama hii ndio media iliyopaswa kuonyesha mfano wa social distancing, lakini wao ka Studio kadogo wanarundikana watu 14!, safari bado ni mbali!.

Naomba kukiri leo ndio mara yangu ya kwanza kumsikia mtangazaji huyu na kuiangalia Wasafi TV siku ya Jumapili asubuhi, huwa naangalia Chomoza kumsikiliza Dr. Ellie. Mimi kwa agewise ni 50+, hivyo kuna ile natural conservative opinion kuwa kuna TV za wazee, kuna tv za watu wazima, kuna TV za vijana na kuna TV za watoto depending on seriousness of contents, Clouds TV, TVE na Wasafi TV, nilizihesabu ni TV za Vijana, hivyo huwa sizifuatilii sana, ila leo wife amengangana nimejikuta naangalia Wasafi TV.

Kipindi cha leo, Studio za Wasafi TV, wamealikwa wanamuziki wa kundi la The Voice, John Lissu, Masanja Mkandamizaji, na Nabii kijana anaitwa Malisa, kiukweli huyu dogo ametisha!.

Akiizungumzia Corona, Nabii Malisa amesema Mungu amezungumza nae kwa maneno ya unabii wa Corona, Mungu amemuonyesha kuwa mwisho wa janga la Corona, mwisho ni Mwezi huu April, kuanzia mwezi May, hakutakuwa na ugonjwa wa Corona tena, na kuanzia sasa hakutatokea tena vifo vya Corona nchini Tanzania, hata hivyo vifo vya Corona vilivyotokea, the cause sio Corona bali ni matatizo mengine ya kiafya ya watu hao ambayo hayakutajwa, hivyo Corona imewasindikiza tuu, kwani tayari waliishakuwa wako njia moja, hata bila ya Corona, ilikuwa safari!.

Kwanza hiki wanachokifanya studio ya Wasafi kwenye janga hili la Corona, is not right, hakuna any social distancing, wameleta kundi kubwa sana watu 14 ndani ya ka studio kadogo!, tushukuru uwepo wa Mungu mahali hapo, lakini ikitokea kuna mmoja hapo ana Corona, ni hatari sana hiki wanachofanya.

Pia anachokifanya Nabii huyu is it right?, kusema definite Corona mwisho April na hakuna tena atakayekufa kwa Corona Tanzania, live on TV?.

Kiukweli huyu Mtangazaji Lilian Mwasha is so good, ana maswali yenye akili, amempigia simu Apostle Daniel Maboyo akizungumza kutoka Arusha, akamuuliza, Tanzania kuna wahubiri wengi wa miujiza ya uponyaji tunawaona kwenye TV mbalimbali wakifanya mambezi ya uponyaji na miujiza ya uponyaji, sasa dunia na Tanzania tumekumbwa na janga la hili gonjwa la Corona, mbona hawa wahubiri hawafanyi maombezi ya kuponya Corona?, mbona hawaendi kuwaombea wagonjwa wa Corona wakaonyesha hiyo miujiza yao ya uponyaji?!.

Apostle Daniel Maboya, mezungumza jambo la msingi sana kuwa Corona ni ugonjwa wa ukweli haihitaji kuufanyia longolongo za uponyaji, amewataka Watanzania tusikilize maelekezo ya viongozi wetu wa serikali na maekezo ya kitaalamu na kumuomba Mungu atuepushe.

Simu zinapigwa watu wanaongea na Nabii Malisa anawafanyia unabii live on TV!. Kama hizi simu zinazopigwa sio arranged or premeditated, then huyu Nabii Malisa anatisha sana kwa jinsi anavyowafunulia hao wapiga simu kuhusu maisha yao, hadi watu wanalia!. Hii maana yake Nabii Malisa, ana nguvu, he has powers, swali linabaki ni jee powers hizo ni kutoka kwa nani?.
Kwenye mambo ya powers, kusema tuu "Kwa Jina la Yesu", hakutoshi!, kwasababu ni Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe alitufundisha kuwa, watakuja wahubiri watafanya miujiza na kutoa mapepo kwa jina lake, lakini sio wake.
Pasaka Njema.
Pasakali
Rejea za Manabii na Unabii
TCRA: Vipindi vya Mahubiri Kwenye TV Pia Viangaziwe/Vithibitiwe!. Mungu Yupo Ila pia Shetani Yupo! - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom