Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Mayala huwa haamini uwepo was Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni Mkisto Mkatoliki, ila kwenye mahusiono nimefuata asili ya kabila langu, mmoja hatoshi!.
Nilipofuatilia kwa makini kwenye Bible nikakuta hakuna amri yoyote ya Mungu ya mke mmoja, ila Wazungu ndio wameleta hizo sheria za kanisa za mke mmoja.
Niliwahi kushauri hivi
"Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?" - JamiiForums
P
 
Tuendelee kuomba wapi jomba Sasa wakati unasema tunayemwomba hatusaidii chochote..au unamaanisha nini,
 
Hehehe hivi hakuna mistari kwenye Bible inayokataza mke zaidi ya mmoja P. Is it, ngoja wake wasukununu watuambie tupate majibu hapahapa P
 
Siyo nabii sema anaejiita nabii
Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu anaitwa jina alilojitambulisha
Muadhama Polycap Cardnali Pengo
Mtume na Nabii Josephat Mwingira
Askofu Mkuu Zakaria Kakobe
Mchungaji Kiongozi, Getrude Rwakatare
Askofu Gwajima
Professor Maji Marefu
Dr. Ngwizukulu Jilala
Dr. Mwaka
etc, wote hawa ndio majina yao.
P
 
P turejee kwenye mistari ya Bible tujue je ni mke mmoja au zaidi?which is which..wake wengi ni dhambi au sio dhambi..
 
P turejee kwenye mistari ya Bible tujue je ni mke mmoja au zaidi?which is which..wake wengi ni dhambi au sio dhambi..
Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismaili na Wakristo ni uzao wa mwanae wa pili Isaka.
Sheria ya Mungu ni sheria ile ile moja ya Musa, Kikristu ni Torati, Kiislamu ni Taurat.

Yesu hakuja kuitengua Torati bali kuikamilisha.
Kwa mujibu mujibu wa sheria ya Mungu, hata nyama ya kitimoto au sungura ni haramu!.
Bikira Maria na wanawake wa enzi hizo walivaa hijab, ila Wazungu wakatufanya vibaya sana.
Maadam sheria ya Mungu ni sheria moja tuu ya Musa, na hakuna popote Mungu amesema mwanaume ataoa mke mmoja, hivyo kuoa mke zaidi ya mmoja sio dhambi.
P
 
Yan wewe ni kiumbe wa ajabu sana. Unawashangaa wanaoenda kuabudu kanisan leo licha ya kupoteza ndugu zao kwa Corona halaf na wewe ulivyo ndorobo unamalizia kwa kusema tuombe Mungu atuondolee huu ugonjwa. Ni Mungu yupi huyo so far aliyejionesha waziwazi kutibu Corona ambaye inabidi tumuombe sote!!

Na kama hayupo Mungu aliyejidhihirisha waziwazi kwenye kutibu ugonjwa wa Corona ni kwanini kila mmoja asiendelee kumuomba Mungu wake aliyemshindia mambo mengine kwa IMANI kwamba Mungu anajibu kwa wakati wake!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo inabidi aongee,kinyume na hapo anakiwa anajiingiza kwenye kazi zisizomhusu.
Hivi kwenye biblia hakuna mahali kumeandikwa "Usiue"? Kwa ivo Askofu anatakiwa asiwaambie wanasiasa kwamba wasiue wanasiasa wenzao?
 
Hawa watu wanaosema wamezungumza na Mungu huaga binafsi nawaogopa kama ukoma.
Sitaki kuulizwa swali kwa hii coment yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haahaaa!! "Eti Mungu Ameniambia".

Malisa bwashee !! ujue Mungu anakuona.
 
Mkuu una maarifa lkn haya hayajajitosheleza.
Uzao ni sawa (legitimate na illegitamate)

Mavazi ni tamaduni si dini. Utamaduni wa mavazi unaendan na mazingira na nyakati za maeneo hayo. Hijabu mashariki ya kati ni kutokana na majangwa na nyika katika maeneo makubwa ya nchi hivyo wanawake waliteseka kwa upepo na vumbi hivyo katika sehemu ya kuhifadhi mihili yao. Hijabu haikuwa mavazi ya kiroma ambao walitoka ulaya.
Ulaya ina utamaduni wake wa mavazi
Afrika tunaoutamaduni wetu ambao ni ngozi za wanyama ambao unapingwa sasa kwa hifadhi ya wanyama.

Ndoa.
Mwanadamu kwa asili ni mbinafsi hivyo hatatosheka na chochote. Mke mmoja ni kukufundisha kupenda, kusamehe, kusahau, kujinyima na kuvumilia. Wake wengi ni kutangatanga kwa imani yako.
Upendo kwa asili haugawanyiki na ndiyo maana pasco tangu ulipooa mapenz yalipungua kwa wazazi wako, rafiki na ndugu yakaamia kwa mkeo na ulipozaa mapendo yakaamia kwa watoto( ubinafsi) unaendelea kumpenda mkeo kwa kuwa ametimiza mapendo yako kwake. Wake wawili unagawanyika na huwezi.
Ndoa ni takatifu kwa kuwa ni sakrement ni sehemu ya kujichotea neema hivyo daima inapaswa kuwa pure( purelarity of marriage ni upendo usiogawanyika na usafi wa moyo(zinaa) vitakufanya kuishi ktk dhamiri safi
 
Kama kweli huyu Nabii Malisa kasema haya maneno na yamerekodiwa itakuwaje kama hayo aliyosema hayatatokea. Yeye ashukuru kwa nyakati tunazoishi maana enzi za kale nabii hakitabiri na utabiri wake ni wa uongo alikuwa anapigwa kwa mawe mpaka anakufa.
 
Hao wanabadilishaga maneno Sana ikienda mrama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…