Nabii Mkuu Dkt Geordavie amzawadia gari la kifahari BMW X5 msanii Mkaliwenu

Katika hali isiyo ya kawaida mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mitandaoni Jackson Sakwile maarufu kama “Mkaliwenu “ametunikiwa gari la kifahari aina ya BMW X5 na Nabii maarufu nchini Dk GeorDavie baada ya kukunwa na mashairi ya nyimbo aliyoitunga kwa ajili yake.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika eneo la Kisongo katika huduma ya Ngurumo ya Upako ambayo inaendeshwa na nabii huyo ambaye hivi karibuni amejizolea umaarufu kwa kutoa misaada na zawadi kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii.

Akihojiwa na waandishi wa habari mchekeshaji huyo amesema kwamba anamshukuru Nabii Dkt GeorDavie kwa kumzawadia gari hilo kwa kuwa hakuwahi kuwa na ndoto ya kumiliki gari lenye thamani kubwa kama hilo.

Mchekeshaji huyo mwenye mbwembwe amesema kwamba awali wakati akitunga na kisha kutoa nyimbo hiyo baadhi ya wasanii nchini ambao hakuwataja kwa majina walimdhihaki kwa kumwambia kuwa njaa itamuua lakini yeye alifanya hivyo kwa mapenzi kwa Nabii Dkt GeorDavie.

“Wasanii wengi waliniponda kwa kuniambia njaa itaniua lakini namshukuru Mungu amejibu maombi “amesema Mkaliwenu

Hatahivyo,amesisitiza kuwa anamkubali Nabii Dkt GeorDavie kwa kuwa mbali na mafundisho yake kuhusu kanuni za kumjua Mungu lakini pia anafundisha kanuni za kuondokana na umaskini.

Mchekeshaji huyo mbali na kupewa gari hilo la kifahari pia alizawadiwa kiasi cha sh,1 milioni za mafuta huku akisisitiza kwamba imani yake hatimaye imezaa matendo.

Awali katika mahubiri yake Dkt GeorDavie alisisitiza kuwa lengo la kumzawadia gari msanii huyo limekuja kutokana na imani na hivyo anastahili tuzo hiyo.

“Imani yake ni kubwa na anastahili reward (zawadi)na ninayainua maisha yako kwa kukuzawadia gari aina ya BMW X5”alisema nabii huyo huku umati wa waumini kanisani hapo ukilipuka kwa shangwe

Huu ni mwendelezo wa nabii mkuu Dkt GeorDavie kutoa zawadi mbalimbali kwa makundi mbalimbali kwenye jamii ambapo hivi karibuni ameonekana akitoa misaada ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo wadogo,bajaji,fedha za mitaji na magari kwa wasanii mbalimbali nchini kitendo ambacho kimemjengea umaarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Mwisho
Huyu nabii ni km amesoma alama za nyakati kwa sasa bila ya kuwa na chawa bongo hii utadoda so anatengeneza machàwa wake ili kila kona wamtaje yeye.

reminding you ni mpenda sifa sana sana
 
Mkali wao mnk kwangu mm si mkali wngu chunga tu ndogo yako Ni haya tu mkali wao
 
All in all uchawa kwa sas inalipa haswaa na ndivyo matajiri na wanasiaaa wanachotafuta kusifiwa na kisha kugawa pesa na kugawa madaraka mm mwenye kuna diwani mmjoaj mwanamama namsifiaga sna unasiki tu goro pitia dukani kwangu jioni nashanga ananikunjia 30 ananimbiaga nenda kapige bia mwanagu wee Ni mpiga kura wangu na nakupenda sna angejuwa mm huwa sipigi kura kbsa bas nakunja zangu 30 nasepa wkt mwingine tunakutana kimara stop over ananimwagia bia mezani Kisha nakuondoka .so uchawa uanlipa
 
Usiache uchawa ndio zama zake hizi
 
Sasa ana nguvu za kulihudumia au amepewa mzigo mzito kuliko uwezo wake?.
 
Hizo ni pesa za Waumini Jamaa anazifuja tu atakavyo hana uchungu nazo.

Waumini wakitoka hapo wakapambane waamke saa kumi alfajiri wakauze uji stendi waende wakatoe sadaka nyingine Nabii atafute kwa kuzipeleka.
 
Katika hali isiyo ya kawaida mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mitandaoni Jackson Sakwile maarufu kama “Mkaliwenu “ametunikiwa gari la kifahari aina ya BMW X5 na Nabii maarufu nchini Dk GeorDavie baada ya kukunwa na mashairi ya nyimbo aliyoitunga kwa ajili yake.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika eneo la Kisongo katika huduma ya Ngurumo ya Upako ambayo inaendeshwa na nabii huyo ambaye hivi karibuni amejizolea umaarufu kwa kutoa misaada na zawadi kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii.

Akihojiwa na waandishi wa habari mchekeshaji huyo amesema kwamba anamshukuru Nabii Dkt GeorDavie kwa kumzawadia gari hilo kwa kuwa hakuwahi kuwa na ndoto ya kumiliki gari lenye thamani kubwa kama hilo.

Mchekeshaji huyo mwenye mbwembwe amesema kwamba awali wakati akitunga na kisha kutoa nyimbo hiyo baadhi ya wasanii nchini ambao hakuwataja kwa majina walimdhihaki kwa kumwambia kuwa njaa itamuua lakini yeye alifanya hivyo kwa mapenzi kwa Nabii Dkt GeorDavie.

“Wasanii wengi waliniponda kwa kuniambia njaa itaniua lakini namshukuru Mungu amejibu maombi “amesema Mkaliwenu

Hatahivyo,amesisitiza kuwa anamkubali Nabii Dkt GeorDavie kwa kuwa mbali na mafundisho yake kuhusu kanuni za kumjua Mungu lakini pia anafundisha kanuni za kuondokana na umaskini.

Mchekeshaji huyo mbali na kupewa gari hilo la kifahari pia alizawadiwa kiasi cha sh,1 milioni za mafuta huku akisisitiza kwamba imani yake hatimaye imezaa matendo.

Awali katika mahubiri yake Dkt GeorDavie alisisitiza kuwa lengo la kumzawadia gari msanii huyo limekuja kutokana na imani na hivyo anastahili tuzo hiyo.

“Imani yake ni kubwa na anastahili reward (zawadi)na ninayainua maisha yako kwa kukuzawadia gari aina ya BMW X5”alisema nabii huyo huku umati wa waumini kanisani hapo ukilipuka kwa shangwe

Huu ni mwendelezo wa nabii mkuu Dkt GeorDavie kutoa zawadi mbalimbali kwa makundi mbalimbali kwenye jamii ambapo hivi karibuni ameonekana akitoa misaada ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo wadogo,bajaji,fedha za mitaji na magari kwa wasanii mbalimbali nchini kitendo ambacho kimemjengea umaarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Mwisho
Vizuri...anarudisha fadhila ?
 
All in all uchawa kwa sas inalipa haswaa na ndivyo matajiri na wanasiaaa wanachotafuta kusifiwa na kisha kugawa pesa na kugawa madaraka mm mwenye kuna diwani mmjoaj mwanamama namsifiaga sna unasiki tu goro pitia dukani kwangu jioni nashanga ananikunjia 30 ananimbiaga nenda kapige bia mwanagu wee Ni mpiga kura wangu na nakupenda sna angejuwa mm huwa sipigi kura kbsa bas nakunja zangu 30 nasepa wkt mwingine tunakutana kimara stop over ananimwagia bia mezani Kisha nakuondoka .so uchawa uanlipa

Tena ukiwa nae wala haumuombi hela unampamba unamweleza vijana huko wanakukubali sana wanajiuliza ubunge hautaki au, unamweleza wapambanaji tena ambao hatuna tamaa tupo wakati huo hata kitambulisho cha mpiga kura hauna
 
All in all uchawa kwa sas inalipa haswaa na ndivyo matajiri na wanasiaaa wanachotafuta kusifiwa na kisha kugawa pesa na kugawa madaraka mm mwenye kuna diwani mmjoaj mwanamama namsifiaga sna unasiki tu goro pitia dukani kwangu jioni nashanga ananikunjia 30 ananimbiaga nenda kapige bia mwanagu wee Ni mpiga kura wangu na nakupenda sna angejuwa mm huwa sipigi kura kbsa bas nakunja zangu 30 nasepa wkt mwingine tunakutana kimara stop over ananimwagia bia mezani Kisha nakuondoka .so uchawa uanlipa
Unamkawizia nini sasa mzee?!
 
Wana mnnadai hiyo sio gari ya kifahari, mi nadhani fahari ni proud kwa kingereza, hivo kama ndivyo basi hiyo ni gari ya kifahari hata kwangu
kwahiyo i am proud of you ni nimefaharika kwako?
 
Screenshot_20221006-004125.png
 
Wana mnnadai hiyo sio gari ya kifahari, mi nadhani fahari ni proud kwa kingereza, hivo kama ndivyo basi hiyo ni gari ya kifahari hata kwangu
Wabongo si wajuaji. Show room bila million 5O huuziwi hio gari watu wanafikiri ni kama dhaihtsu mira hio ya million 8
 
Back
Top Bottom