Nabii Mkuu Dkt Geordavie amzawadia gari la kifahari BMW X5 msanii Mkaliwenu

Katika hali isiyo ya kawaida mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mitandaoni Jackson Sakwile maarufu kama “Mkaliwenu “ametunikiwa gari la kifahari aina ya BMW X5 na Nabii maarufu nchini Dk GeorDavie baada ya kukunwa na mashairi ya nyimbo aliyoitunga kwa ajili yake.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika eneo la Kisongo katika huduma ya Ngurumo ya Upako ambayo inaendeshwa na nabii huyo ambaye hivi karibuni amejizolea umaarufu kwa kutoa misaada na zawadi kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii.

Akihojiwa na waandishi wa habari mchekeshaji huyo amesema kwamba anamshukuru Nabii Dkt GeorDavie kwa kumzawadia gari hilo kwa kuwa hakuwahi kuwa na ndoto ya kumiliki gari lenye thamani kubwa kama hilo.

Mchekeshaji huyo mwenye mbwembwe amesema kwamba awali wakati akitunga na kisha kutoa nyimbo hiyo baadhi ya wasanii nchini ambao hakuwataja kwa majina walimdhihaki kwa kumwambia kuwa njaa itamuua lakini yeye alifanya hivyo kwa mapenzi kwa Nabii Dkt GeorDavie.

“Wasanii wengi waliniponda kwa kuniambia njaa itaniua lakini namshukuru Mungu amejibu maombi “amesema Mkaliwenu

Hatahivyo,amesisitiza kuwa anamkubali Nabii Dkt GeorDavie kwa kuwa mbali na mafundisho yake kuhusu kanuni za kumjua Mungu lakini pia anafundisha kanuni za kuondokana na umaskini.

Mchekeshaji huyo mbali na kupewa gari hilo la kifahari pia alizawadiwa kiasi cha sh,1 milioni za mafuta huku akisisitiza kwamba imani yake hatimaye imezaa matendo.

Awali katika mahubiri yake Dkt GeorDavie alisisitiza kuwa lengo la kumzawadia gari msanii huyo limekuja kutokana na imani na hivyo anastahili tuzo hiyo.

“Imani yake ni kubwa na anastahili reward (zawadi)na ninayainua maisha yako kwa kukuzawadia gari aina ya BMW X5”alisema nabii huyo huku umati wa waumini kanisani hapo ukilipuka kwa shangwe

Huu ni mwendelezo wa nabii mkuu Dkt GeorDavie kutoa zawadi mbalimbali kwa makundi mbalimbali kwenye jamii ambapo hivi karibuni ameonekana akitoa misaada ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo wadogo,bajaji,fedha za mitaji na magari kwa wasanii mbalimbali nchini kitendo ambacho kimemjengea umaarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Mwisho
Geordavie anaweza kuwa ni miongoni mwa manabii wa kizazi hiki mwenye akili kubwa. Just imagine, anampa Gari mtu kama Mkaliwenu, Goodluck Gozbert, mshikaji aliwahi kumshout-out Harmonize kanisani, that Interview na Millard Ayo went viral too... Sasa huyu jamaa anacheza na watu wenye ushawishi to get his name exposed kwenye media (which isn't bad). Hongera Mkaliwenu.
 
Mkuu, hiyo ulioweka ni BMW X5 G series (G05) ya mwaka 2019, bei yake ni kama mara 5 ya aliopewa (Kapewa E70 ya mwaka 2007).

Picha uliyoweka (G05) 2019
1280px-2019_BMW_X5_xDrive30d_M_Sport_Automatic_3.0_Front.jpg

Picha aliyopewa (E70) 2007

1280px-2007-2008_BMW_X5_(E70)_3.0d_01.jpg
 
Katika hali isiyo ya kawaida mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mitandaoni Jackson Sakwile maarufu kama “Mkaliwenu “ametunikiwa gari la kifahari aina ya BMW X5 na Nabii maarufu nchini Dk GeorDavie baada ya kukunwa na mashairi ya nyimbo aliyoitunga kwa ajili yake.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika eneo la Kisongo katika huduma ya Ngurumo ya Upako ambayo inaendeshwa na nabii huyo ambaye hivi karibuni amejizolea umaarufu kwa kutoa misaada na zawadi kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii.

Akihojiwa na waandishi wa habari mchekeshaji huyo amesema kwamba anamshukuru Nabii Dkt GeorDavie kwa kumzawadia gari hilo kwa kuwa hakuwahi kuwa na ndoto ya kumiliki gari lenye thamani kubwa kama hilo.

Mchekeshaji huyo mwenye mbwembwe amesema kwamba awali wakati akitunga na kisha kutoa nyimbo hiyo baadhi ya wasanii nchini ambao hakuwataja kwa majina walimdhihaki kwa kumwambia kuwa njaa itamuua lakini yeye alifanya hivyo kwa mapenzi kwa Nabii Dkt GeorDavie.

“Wasanii wengi waliniponda kwa kuniambia njaa itaniua lakini namshukuru Mungu amejibu maombi “amesema Mkaliwenu

Hatahivyo,amesisitiza kuwa anamkubali Nabii Dkt GeorDavie kwa kuwa mbali na mafundisho yake kuhusu kanuni za kumjua Mungu lakini pia anafundisha kanuni za kuondokana na umaskini.

Mchekeshaji huyo mbali na kupewa gari hilo la kifahari pia alizawadiwa kiasi cha sh,1 milioni za mafuta huku akisisitiza kwamba imani yake hatimaye imezaa matendo.

Awali katika mahubiri yake Dkt GeorDavie alisisitiza kuwa lengo la kumzawadia gari msanii huyo limekuja kutokana na imani na hivyo anastahili tuzo hiyo.

“Imani yake ni kubwa na anastahili reward (zawadi)na ninayainua maisha yako kwa kukuzawadia gari aina ya BMW X5”alisema nabii huyo huku umati wa waumini kanisani hapo ukilipuka kwa shangwe

Huu ni mwendelezo wa nabii mkuu Dkt GeorDavie kutoa zawadi mbalimbali kwa makundi mbalimbali kwenye jamii ambapo hivi karibuni ameonekana akitoa misaada ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo wadogo,bajaji,fedha za mitaji na magari kwa wasanii mbalimbali nchini kitendo ambacho kimemjengea umaarufu ndani na nje ya mipaka ya nchi.

MwishoView attachment 2378181View attachment 2378182View attachment 2378183View attachment 2378184
Ndugu ma-rain bow hao....za chn kabisa
 
All in all uchawa kwa sas inalipa haswaa na ndivyo matajiri na wanasiaaa wanachotafuta kusifiwa na kisha kugawa pesa na kugawa madaraka mm mwenye kuna diwani mmjoaj mwanamama namsifiaga sna unasiki tu goro pitia dukani kwangu jioni nashanga ananikunjia 30 ananimbiaga nenda kapige bia mwanagu wee Ni mpiga kura wangu na nakupenda sna angejuwa mm huwa sipigi kura kbsa bas nakunja zangu 30 nasepa wkt mwingine tunakutana kimara stop over ananimwagia bia mezani Kisha nakuondoka .so uchawa uanlipa
Usisahau kuleta mrejesho litapo kukuta jambo
 
Nabii,waumini wako wana uhitaji kibao,unatoa magari kwa wasanii.
Wana uhitaji vipi wakati hilo gari wamenunua hao hao waumini? Au huyo nabii ana biashara nyingine zaidi ya kanisa?
 
Historical Churches ziliwekeza sana kwenye huduma za Afya (Hospital) na Elimu (Mashule,Vyuo). Ni huduma zilizosaidia wengi bila gharama kubwa.Wasomi wengi wametoka kwenye shule hizi na kupata tiba kwenye hopistali zile.

Modern Churches (Business Churches), hawana muda na fedha za kuanzisha taasisi zenye kusaidia wengi.zimewekea kwenye kutukuza mtu binafsi yeye kama yeye, na biashara zao hizo zinayumba tu Pale mwanizilishi wake anapo fariki. Ukiimba nyimbo za kutukuza yeye, una pewa pesa au gari!! HIVYO ZITAKUJA NYIMBO NA MASHAIRI KUTOKA HUKO NA KULE YA KUMTUKUZA NABII MKUU NA SIO YESU KRISTO.
 
Nabii mkuu natengeneza kikosi cha machawa
 
Nabii anatumia chopper ... siku akipita barabarani msafara wake ni kama raisi.

Anyway "Fateni wanayofundisha msifate wanayofanya" Alisema Yesu"
 
Back
Top Bottom