Pre GE2025 Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpasuko ni dhahiri,

Mzee Kamba naye Amerika kutuhakikishia kuwa waliotumbuliwa atawarudisha mezani.

Ngoja tusubiri.
 
Salaam, Shalom.

Katika Unabii wa mwaka 2024, Nabii Sanga ametoa ujumbe Kwa Watanzania kuingia katika maombi kukiombea chama tawala CCM, amesema ameambiwa kuwa mwaka huu 2024 kutakuwa na mgawanyiko mkubwa utakaokikumba chama hiki.

Amesema pia kuwa, mgawanyiko na mtikisiko utakaokikumba chama Cha MAPINDUZI CCM, haitakuwa Siri, itakuwa ni mtikisiko wa wazi ambao hata raia wa kawaida watajua.

Amesema Mungu amemwambia awaase raia kukiombea Chama Cha MAPINDUZI CCM Kwakuwa mtikisiko wa chama tawala utaathiri pia Nchi Kwa ujumla, na ujumbe wa kukiombea CCM ni Ishara kuwa Mungu BADO anapenda CCM iendelee kuongoza Nchi na amesema kuwa, adui amepanga kutumia mgawanyiko huo kuivuruga Amani ya nchi.

Amesema pia, amepata ujumbe kuwapa Marais wote wa Africa kuwa Waaminifu Kwa Nchi zao na kuwatumikia wananchi Kwa HAKI, la sivyo, patakuwako maandamano katika Nchi nyingi Afrika ikiwa hawatakuwa Waaminifu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.🙏

Source: POG family Tv.
Application ya usemi wa wahenga "Aidui muombee njaa"
 
Nabii ni cheo gani katika Ukristo? Mkuki kwa Nguruwe siyo!?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app

Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.

Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).

Watu wa namna hiyo wanapatikana katika dini nyingi, hususan katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.

Katika Uyahudi​

Katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) tunakuta vitabu vingi vinavyojumlishwa katika jina "manabii", kuanzia Yoshua hadi Malaki. Katika Ukristo baadhi ya vitabu hivyo vinahesabiwa kuwa "vitabu vya historia", kumbe kile cha Danieli kinapangwa kati ya "manabii wakuu" pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli, wakati Wayahudi wanacho kati ya "maandiko (mengine)".

Katika Ukristo​

Ukristo unakubali manabii wote wa Agano la Kale, lakini upande wa Agano Jipya ni wachache wanaoitwa hivyo, kwa mfano Agabo anayetajwa katika Matendo ya Mitume.

Kwa jumla ni kwamba Wakristo wote wanahesabiwa kuwa manabii kutokana na wajibu wa kutangaza Neno la Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

___Wikipedia----
 
CCM imeshikamana na Dola, ni kama mwili na ngozi!!

Kuvitenfanisha Kwa ghafula, Nchi itatikisika,

Kifo Cha kimkakati ndo suluhu!!

Sijui umeelewa?

CCM ikifa Zanzibar ndio mwisho wake .

Hilo wanalijuwa vizuri na ndio wanaogopa upinzani kuchukuwa madaraka Zanzibar kwani wanaelewa ndio kifo chao
 
Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.

Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).

Watu wa namna hiyo wanapatikana katika dini nyingi, hususan katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.

Katika Uyahudi​

Katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) tunakuta vitabu vingi vinavyojumlishwa katika jina "manabii", kuanzia Yoshua hadi Malaki. Katika Ukristo baadhi ya vitabu hivyo vinahesabiwa kuwa "vitabu vya historia", kumbe kile cha Danieli kinapangwa kati ya "manabii wakuu" pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli, wakati Wayahudi wanacho kati ya "maandiko (mengine)".

Katika Ukristo​

Ukristo unakubali manabii wote wa Agano la Kale, lakini upande wa Agano Jipya ni wachache wanaoitwa hivyo, kwa mfano Agabo anayetajwa katika Matendo ya Mitume.

Kwa jumla ni kwamba Wakristo wote wanahesabiwa kuwa manabii kutokana na wajibu wa kutangaza Neno la Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

___Wikipedia----
Jibu swali, Unabii ni cheo gani katika Ukristo?
Hayo maelezo hata upande wa Sheikh kila Muislam anaweza kuwa sheikh, hapa nataka kujua katika Kanisa (Ukristo) Nabii ni cheo gani? Then nitajie manabii katika taasisi za dini ambao ni viongozi, elewa neno taasisi (mfano wa taaisisi ni kama Roman Catholic, KKKT, Anglican n.k)

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Jibu swali, Unabii ni cheo gani katika Ukristo?
Hayo maelezo hata upande wa Sheikh kila Muislam anaweza kuwa sheikh, hapa nataka kujua katika Kanisa (Ukristo) Nabii ni cheo gani? Then nitajie manabii katika taasisi za dini ambao ni viongozi, elewa neno taasisi (mfano wa taaisisi ni kama Roman Catholic, KKKT, Anglican n.k)

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app

Mimi si mkristo nimekuwekea hapo nini unabii katika ukristo cheo mtakijuwa wenyewe mnaowaita hivyo

Si kila mwislamu unaweza kumwita sheikh

Utofauti wa Sheikh, Mufti na Kadhi
 
Basi usirudie kuandika usiyofahamu. Katika Ukristo Manabii walibaki kwenye Biblia. Ngoja nikujibu la Sheikh sasa....
Katika Uislamu, "sheikh" ni neno la Kiarabu linalotumika kumaanisha kiongozi wa kiroho, msomi wa Kiislamu, au mtu mwenye hekima na maarifa katika masuala ya dini. Kwa kawaida, sheikh anaweza kuwa:

1. Msomi wa Kiislamu: Mtu ambaye amejifunza na ana uelewa wa kina wa Quran, Hadithi, na masuala mengine ya dini. Anaweza kuwa na elimu ya juu kutoka kwenye taasisi za Kiislamu kama vile Al-Azhar, Madina University, au taasisi zingine mashuhuri.

2. Kiongozi wa Kidini: Anaweza kuwa imamu anayeongoza sala katika msikiti, au mtu anayetoa mawaidha na nasaha za kidini kwa Waislamu.

3. Mzee mwenye Hekima: Katika baadhi ya tamaduni, neno sheikh linaweza pia kutumika kumaanisha mzee mwenye hekima na heshima, bila kujali kiwango chake cha elimu ya kidini.

Kwa ujumla, sheikh ni mtu anayeheshimika kwa elimu yake, hekima yake, na uwezo wake wa kuwaongoza Waislamu katika masuala ya kiroho na kidini.

Sasa niambie Kiongozi gani wa kiislamu ambaye yuko sawa na huyo nabii wako Tito ??
 
Back
Top Bottom