Sipingani na wewe, ila pia sisemi kwamba Mwalimu Mwakasege anaweza kuzuia kwa sababu yeye ni Mwalimu hapana.
Mwakasege anaweza kuzuia kama Kuhani na Mfalme katika ulimwenu wa Roho. Hata wewe unaweza kuzuia provided umeokoka na umemkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Yesu alipokufa msalabani, pazia la hekalu lilipasuka, pakawa hapahitajiki tena kuhani kama mupatanishi kati ya wanadamu na Mungu, isipokuwa kuanzia pale ukawa ni ukuhani wa watu wote (priesthoof of all nations). Kwa hiyo kuanzia pale wote waliomkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao, wakawa wamefanyika makuhani, na hivyo swala lolote la kiroho ambalo Mungu anaweza kuwaonyesha wanadamu na likawa liko katika level ya mwanadamu kui- intervene ili kulibadilisha kwa kuzuia matokeo mabaya, lkuanzia pale likawa ni la watu wote waliokoka.
Pamoja na hayo kwamba swala hili lilishakuwa ni la kila mtu kwa sasa hata yule ambaye ameokoka leo, expereience pia ima matter, namna ya mtu ambavyo ametemebea na Mungu na ku-interact naye katika mambo mengi makubwa makubwa ndiyo inayoweza kusababisha matokeo chanya kirahisi zaidi, na hii ndiyo sababu pekee iliyopelekea nimtaje Mwalimu mwakasege.
Uneongea vizuri juu ya karama mbalimbali na nilichosema tangu awali, nabii sasa alitakiwa awashirikisehe wenye karama zingine, watu sahihi kulingana na karama hizo ulizozitaja wewe hapo juu, badala tu ya kuibuka tu na kulipuka hewani mambo ambayo yanaweza kusababisha taharuki kwa watu wasiokuwa na uelewa mpana wa kiroho, lengo ikiwa ni kuvutia sadaka.
Watunishi uchwara wasitafute umaarufu wa kuongeza sadaka, at the expense ya maisha ya watanzania. Ana bahati sina mamlaka kwenye dola lakini ningekuwa nayo lazima tungefanya mahojiano naye kidogo