DOKEZO Nadai Tsh. Milioni 440 kwa Mkandarasi wa SGR. Naomba Serikali inisaidie, napigwa danadana tangu Desemba 2022

DOKEZO Nadai Tsh. Milioni 440 kwa Mkandarasi wa SGR. Naomba Serikali inisaidie, napigwa danadana tangu Desemba 2022

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Biashara na makampuni ya kimataifa inabidi uwe makini sana... Mkataba kama wa Tsh 400 Million umeshindwa kutoa Tsh 4 million kwa Wakili hapo? Uweke kipengele cha uamuzi kwenye Mambo ya kibiashara wameshindwa kukulipa unakama crane, Motor Grader, Excavator na Mitambo mengine ya maana ungeona kama wasingekulipa.
Next time jua kuwa haya makampuni usipokuwa makini wanakupiga mchana kweupe tafuta mawakili Lipa vizuri utapa hela yako.
 
WAKATI MNAINGIA MKATABA NTYJUZE PIS TYWAWEKE MAIMBINI MFANIKIWE
 
Haya Ni Ya Ajabu Sana Mtanzania Anatoa Huduma Hapa Hapa Tena Kwa Mkataba Ulio Wazi
Upande Wa Malipo Wanamsumbua Halafu Viongozi Wetu Wapo!!
Sijui Ulipo Ila Najua Una Uwezo Wa Kufika Dodoma Chap Uonane Na Waziri
Changamka Uukomboe Wakati Umeshatoa Huduma Hutakiwi Kulipwa Millions 10
Malipo Yako Yalipwe Yote


CC: Mwigulu Nchemba
CC: Makame Mbalawa
 
Haya Ni Ya Ajabu Sana Mtanzania Anatoa Huduma Hapa Hapa Tena Kwa Mkataba Ulio Wazi
Upande Wa Malipo Wanamsumbua Halafu Viongozi Wetu Wapo!!
Sijui Ulipo Ila Najua Una Uwezo Wa Kufika Dodoma Chap Uonane Na Waziri
Changamka Uukomboe Wakati Umeshatoa Huduma Hutakiwi Kulipwa Millions 10
Malipo Yako Yalipwe Yote


CC: Mwigulu Nchemba
CC: Makame Mbalawa
Huyo wakukimbiliwa (serikali) ndiye mdaiwa mkuu. Tatizo kubwa la Yapi lilikuwa ni cashflow, malipo yake yalisuasua sana.
Kuna kipindi alianza kulipa suppliers wake may be na huyu alishamalizana naye
 
Mimi sio mtu wa mitandao sana lakini nimeona malalamiko kadhaa yanayoandikwa na Jamii Forums kuhusu mambo mbalimbali yanafanyiwa kazi hasa kuhusu huku kwenye shughuli zetu tunazozifanya kwenye miradi.

Mimi ni mmoja wa Wakandarasi wadogo ambao tumekuwa tukifanya kazi na Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Kampuni ya Yapi Merkezi tangu Februari 2022.

Hadi kufikia leo naandika andiko hili, kupitia Kampuni ya Mzamiru Development Ltd namdai Mkandarasi huyo kiasi cha Tsh. Milioni 440 (fedha za Kitanzania), nimekuwa nikidai malipo yangu tangu Januari, Mwaka huu (2023) lakini nazungushwa kulipwa.

Nilianza kufanya nao kazi kuanzia Lot 1 (awamu ya kwanza), nawakodisha magari ya maji yanayotumika kwenye mradi, ikaendelea hivyo pia Lot 2.
View attachment 2778659
Nimeambatanisha na sample ya mkataba wa ukodishaji vifaa.

Huko siku za nyuma nilikuwa nalipwa japo sio katika kiwango ambacho tumekubaliana, mfano unaweza kudai Milioni 100 lakini wakakupa Milioni 10 na kuahidi kuendelea kukulipa baada ya muda.

Utaratibu tuliowekeana ni kuwa kila mwezi tunatakiwa kulipwa kiasi fulani, lakini ilipofika mwezi wa kumi na mbili mwaka jana (2022) ndipo malipo yalipoanza kukwama.

Mpaka sasa naendelea nao kwenye Awamu ya Tatu yaani Lot 3, hakuna malipo na magari yangu niliyowakodisha bado yapo kwenye kazi.

Nimesumbuka sana kufuatilia malipo yangu lakini sioni dalili za kulipwa, hofu yangu ni kuwa inawezekana mambo yakawa magumu zaidi siku za mbele hivyo kunipa hasara kubwa.

Naomba Serikali isaidie watu kama sisi ambao ni Wakandarasi tunaopambana kujiweka kwenye mstari, kwani mtaji wangu niliowekeza hapo haunisaidii peke yangu, kuna Watanzania wenzangu wengi wanaofaidika kupitia ajira hiyo.
Mkuu nenda kawashitaki Mahakamani na uweke Wakili apate kukutetea utapata haki yako kuliko kuja hapa kulalamika haupati kitu Waturuki huwajuwi watamaliza contract yao watakukimbia na kukuacha njia panda fanya upesi ukawashitaki kabla hawaja maliza mikataba yao ya ujenzi wa hiyo reli ya SGR.
 
Juzi Mama Saa 100 alienda Turkey...moja ajenda kuu ni Yepi kumalizia kipande Lot 3 Bahi hadi Tabora....naamini wameongea na kukubaliana Yeoi warudi kazini maana walitaka kuwauzia wachina wao wasepe
 
Back
Top Bottom