Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Kati ya huu Uzi na ule mwingine upi Ni wa kweli?
Yote ni ya kweli mkuu.
Ule wa “ushuhuda “niliongea nikiwa nimevaa joho langu la “THE GREAT WOMAN OF GOD”.
Lugha niliyotumia kule ndiyo lugha ninqyoiongea kila siku ktk maisha yangu halisi .

Huu wa leo si nimesema NAKIRI vitu ambavyo nimekua naogopa kusema?
 
Endelea kuamini mkuu🙏🏼
Mimi bana siwezi kuamini tena labda nikae board room na Sir God mwenyewe nimuulize maswali yangu ila hayo unayonihubiria huwa nawahubiria watu kila siku kwa hiyo hayana maajabu yoyote kwangu🙏🏼
Bold!
 
Sawa tuseme wanadamu hatuwezi kumdadis Mungui(sbb huwezi dadisi kitu kisichopo) ila basi si amesema “niite nami nitakuitika nitakuomyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua?
Trust me mkuu nishamuita sana ila hajawahi kuniitika hata mara moja akaacha nikateseka tokea niko mtoto wakati alisema “waacheni watoto wadogo waje kwangu” au kwa vile mimi nilikua mtoto masikini anapokea watoto point five tu au? ,lakini si yeye ni baba wa tatima ?Sasa hata uyatima wangu hakuuona atimize ahadi yake ?kwanini aache niteseke peke yangu ktk umri mteke?
Haya anasema “Na lolote mtakaloomba kwa jina langu nitafanya” nilishaomba sana tena nikiwa mdogo sina dhambi wala mawaa mana anasema hasikii maombi ya wenye dhambi ila hakufanya chochote mkuu,
HAYUPO na kama yupo ni muongo muongo kama wanaume wa Kipare hawatimizagi ahadi zao😃 au ni mbaguzi tena mwenye roho mbaya na katili au vyite kwa pamoja.
Mkuu hukosei chochote kuamini kuwa yupo ila kwangu HAYUPO NA HATAKUWEPO 🙏🏼
 
Asante mkuu🙏🏼
Uko sahihi.
Kuna nyakati yanatokea mambo basi unajiona mpweke na mnyonge sana ila kuna siku huwa nafurahia the way maisha yangu yapo
Nipo hapa ili kukamilisha furaha yako na kujaza hiyo empty heart. Angalia maisha yako ya baadae yatakuwaje kama utazeeka bila kuwana mwenza wa maisha yako ambae ndie mtu wako wa karibu hasa wa kufa na kuzikana. Karibu inbox tudiscuss.
 
Hivi nini maana ya Wakala wa shetena? andiko lako linaweza kuchangia kuwapoteza wengi. Najaribu kufikiria wote tungekuwa na mawazo kama haya dunia isingetawalika. Kuamini Mungu yupo kuna saidia kukuweka katika misingi ya kibinadamu compared to wanyama au viumbe wengine....
 
Soma waliomini na wakafanikiwa, ndiyo utajua wewe bado sana kwenye imani na imani yako ni haba
 
Kwa taarifa yako dini ndio imevuruga amani ya dunia mkuu.
Sheria za nchi zipo kuhakikisha kila mtu anaishi kwa amani
 
Nipo hapa ili kukamilisha furaha yako na kujaza hiyo empty heart. Angalia maisha yako ya baadae yatakuwaje kama utazeeka bila kuwana mwenza wa maisha yako ambae ndie mtu wako wa karibu hasa wa kufa na kuzikana. Karibu inbox tudiscuss.
Asante mkuu.
Ningekua single ningekuja🙏🏼
 
Pole kwa hili hongera pia, uliofaulu ni mengi muhimu japo uliokosa pia muhimu sana. Endelea kuamini ktk imani yako pengine ndo imekufikisha hadi sasa, nafikiri nikikwambia "kuwa jasiri" nitakuwa nimeongea jambo kubwa sana
 
Hakika utakua umeniambia jambo kubwa na sitachukulia kawaida.
Asante mkuu🙏🏼
Pole kwa hili hongera pia, uliofaulu ni mengi muhimu japo uliokosa pia muhimu sana. Endelea kuamini ktk imani yako pengine ndo imekufikisha hadi sasa, nafikiri nikikwambia "kuwa jasiri" nitakuwa nimeongea jambo kubwa sama
 
Endelea kuamini mkuu🙏🏼
Mimi bana siwezi kuamini tena labda nikae board room na Sir God mwenyewe nimuulize maswali yangu ila hayo unayonihubiria huwa nawahubiria watu kila siku kwa hiyo hayana maajabu yoyote kwangu🙏🏼
Bado uko shallow kwenye mambo mengi ila kosa kubwa ni kuamini una utambuzi mkubwa, kila unapoandika unadhihirisha unyonge wa elimu yako, yeye hawezi kukaa board room.

Ukitoka nje usiku tizama mbingu zilivyo pana na zimezunguka kila upande wa ardhi lakini pale juu kuna heavy bodies zinaonekana kama nukta tu, hizo bodies ukiingiza dunia yote inaingia zaidi ya mara 1000, sasa aliyeviumba hivyo akae na wewe board room.

Ndio maana kuamini uwepo wake ni kwa upendo kwanza kabla ya yote na kumtukuza na kumuheshimu, ukishaanza kumuweka nafasi ya mjumbe wa nyumba kumi basi kumkataa ni next, mimi najua mambo mengi kama utapenda unaweza kuwasiliana na mimi private, kama hutopenda it's okay.
 
ANALYSIS KIUFUPI
1.Atheist
2.Single Mama -1 Kid
3.Maisha safi -Ada ya Milioni kumi hata Feza unasoma
4.Gospel Singer -Unahudumu
5.Kataa ndoa -diehard fan
Najiuliza
1.Nani anakuondolea hamu za hapa na pale -Au atheist hampati hisia ?
2.Je makuzi /malezi yako yamechangia kutomjua Mungu?
Otherwise hakuna kitu kibaya Kama kupretend, Kama wewe ni Atheist basi mfundishe mwanao pia awe Kama wewe. Kwanini uigize maisha 😃😃
 
Habari, unatatizo linaitwa Ant glomia abolocture amigo, nicheki kwa pm nikusaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…