Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Habari wapendwa.

Leo naanza kwa kumshukuru Maxence Melo kwa kuanzisha hii platform ambayo leo nitaitumia kusema kitu ambacho nikikisema ktk maisha yangu halisi nitaonekana wa ajabu na nina hakika kuna wapendwa wangu watanitenga hivyo nitawaambia nyie japo najua mtanipopoa sana leo ila nataka nione nitajisikiaje baada ya kusema coz nimekua natamani sana nipate mtu wa kumwambia.

Kwa nitakayoyaorodhesha hapa chini nadhani mimi nitakua ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote hapa Jamii forums🙈🙈.

MIMI NI SINGLE MAZA wa one smart little boy mwenye ndoto za kuwa Astronaut na mchungaji.Katika vitu nimefaulu kwa max nyingi maishani ni malezi bora ninayompatia huyu mtoto.Nimefanikiwa kumfanya ashike namba 1 miaka yote shuleni.Nimefanikiwa kumfundisha maadili kiasi kwamba amekua mtoto anayetolewa mfano na kupendwa na majirani na kila anayekua nae karibu.Kikubwa nimefanikiwa kumfanya aupende na kujivua uanamme wake kiasi kwamba anasema ikitokea achague kufa au kuishi kama msichana atachagua kufa.👍👍.Mwanangu ni kembamba karefu ila ukikaona kanavyotembea kibabe huku kametanua mikono utasema baunsa😂na nimefanikiwa kumfanya aamini style nzuri ya nywele ni ya kipolisi tu na kuchukia tule tu jeans twenu twa kubana.Mwanangu pigo zake ni suruali za kisabato na hata kwa risasi humvalishi hivyo vimodel.Ikitokea vaseline yake imeisha yuko tayari kupaka mafuta ya kula kuliko kupaka lotion yangu.

Najivunia kuweza kumudu ada ya over 10M ili mwanangu apate elimu ktk mazingira bora na salama na yatakayompa connection hapo badae.Najivunia kuweza kumpa maisha mazuri na exposure ambazo watoto wengi hawawezi kupewa na baba zao.He can drive and ride(nyumbani tu),he can paint,he can put tiles na vitu vingi vya ufundi hadi kunyoosha koplo at only 12..

Najivunia kufanya ampende baba yake kwa kumwambia story nzuri kuhusu babake na hilo limefanya wawe karibu na yeye kufaidi malezi ya baba na mama.

Najivunia baba watoto wangu anavyonisifia kwa mtoto kuwa “your mum is a darling queen” hadi mtoto huwa anauliza(ga) sasa mbona hatuishi kama one big family na huwa anaambiwa muulize mama yako na hii ni kwa sbb mimi ndio niliyeomba tutengane tukiwa bado tunapendana ili nipambanie ndoto zangu na sijutii hilo coz nikifa leo mwanangu atakua miongoni mwa mabilionea watoto hivyo pamoja na kwamba kuna siku za upweke ila SIJUTII maamuzi yangu yaliyopelekea niwe SINGLE MOTHER.💕

MIMI NI ATHEIST.🙈

Nimekua na doubt uwepo wa Mungu tokea nikiwa primary.Nimebatizwa kilutheri lkn mpaka siku napata kipaimara tayari nilishaanza kujiuliza uliza vitu.


Ninakubaliana na Kiranga na wenzie kuwa Mungu,Allah,shetani,mbinguni,akhera,uchawi,majini,Firdaus na mapepo ni hadithi tu zilizotungwa na binadamu kwa lengo lakuweka hofu ndani ya watu.

Hata hivyo mimi ni tofauti na kina Kiranga kwa sababu mimi(mnisamehe sana) ni “mtumishi wa Mungu”. Ninasimama madhabahuni kuhubiri na pia ninaimba nyimbo za injili.Nyimbo zangu ziko youtube,nina account kubwa tu Insta na wapendwa wanakiri “kubarikiwa “sana na huduma yangu na wengine wanakiri hadi kupona magonjwa kupitia nyimbo zangu au “maombi” ninayofanya ila hiyo iko kisaikolojia zaidi hakuna anayepona kimiujiza.


KWANINI MIMI NI ATHEIST ila nasimama MADHABAHUNI?


1)Sitaki mwanangu ajue mimi ni atheist sbb akifikia ule umri wa ujana wa kusumbua biblia itakua moja ya silaha zangu kumtuliza wenge.


2)Napenda kufundisha (nina ualimu ndani yangu)!hasa wanawake wenzangu ila huwa sihubiri mambo ya kufikirika ya miujiza ila kwq vile jukwaa langu ni madhabahuni inabidi nitumie bible na kutaja Yesu na kukemea mapepo na mimi ni muhubiri mzuri sana ukiniona nikiwa nahubiri jinsi “nawasha moto wa upako” na ninavyonena kwa lugha halafu uambiwe mimi ni atheist na ninakunywa wine hutaamini🙈🙈.


3)Vile vile napenda kuimba so naimba gospel kama hobby tu ila ndo hivyo siamini ninachokiimba ila naburudika.

4)Kanisa limenipa heshima.Najisikia raha zile VIP treatments ninazopata ninapoitwa sehemu kuhubiri/kuhudumu.

5)Kanisa ndio sehemu pekee nimekua na socialize toka niwe na akili.Sijui bar wala clubs wala sehemu nyingine ya starehe.Marafiki na ndugu zangu nimewapatia kanisani na ndo mana siwezi kamwe kuruhusu wajue mie ni atheist.

6)Sehemu ya kipato changu inatoka madhabahuni.(Sio unavyodhani).


MIMI NI YATIMA ila sina uhakika.

Hii na uatheist ndo vitu sitaki kabisa watu wajue.

Najihesabu kama yatima ila ukweli ni kwamba sijui kama wazazi wangu wako hai au wamekufa.Sijui majina yao,dini,kabila wala sina uhakika kama ni watanzania au la ila mama yangu kwa kigezo cha umri anaweza kuwa bado hai sbb nahisi alifanya aliyofanya sbb nahisi alipata mimba yangu akiwa mtoto na inawezekana aliificha mimba na hata kuzaa.Nashukuru hakupata wazo la kutoa mimba.


Wakati niko mdogo nilidhani mama aliyekua akinilea ndo mamangu mzazi kwa jinsi alivyonipenda kuliko hata wanae na wanae nilijua ni ndugu zangu wa kuzaliwa ila alipofariki ndo nikajua ukweli.Watoto wake wakagawanywa kwa ndugu ila mimi sasa hakuna aliyenitaka ila ndo hakuna aliyejua yule mama alinitoa wapi ili wanirudishe.

Hivyo Ikawa leo nakaa kwa huyu kesho yule akiwa hana dada wa kazi napelekwa kwake,kesho kutwa nitaadhibiwa niseme kwanini baba mwenye nyumba ananiangalia sana then nitafukuziwa kwa yule anayeaminiwa ni mkali aninyooshe eti nina tabia chafu n.k.

Kwa kifupi niliteseka sana sana sanaaaaaa ktk umri mdogo na sehemu pekee niliruhusiwa kwenda ni kanisani maana walikua walokole ukoo mzima😂.Walikua watu wa Mungu😀.

Kuna nyakati kuna vitu nilikua napitia nikafunga sana nikiomba Mungu anipumzishe navyo.Kuna siku nilitoroka usiku nikakimbilia kanisani nikapiga goti nikawa nasali huku machozi yanatiririka mashavuni hadi pakakucha,Nilisali nikimlalamikia Mungu usiku mzima bila kupumzika hadi miguu ikafa ganzi kwa kupiga goti.Nilikua namuomba Mungu kuwa ikimpendeza aidha aichukue roho yangu niende kwake nikapumzike au kama anataka niendelee kuishi basi aniondoe kwenye mateso niliyokua napitia.

Kufa sikufa ila cha moto niliendelea kukiona.Kuna siku nakumbuka niliropoka kwa mchungaji kuwa kama Mungu wetu sio kiziwi au kipofu basi hana huruma.

Wale ndugu zangu niliolelewa na mama yao wakati tuko wadogo kila tulipokutana tuliendelea kupendana ila tulipokua wakubwa na nikaanza kuwapiga gape la maendeleo wakanitenga kwa chuki kuu.

Ilifika sehemu nilifukuzwa kwenye msiba kwa madai kuwa kuna mtu wa Mungu ameoneshwa eti mimi ndio nimemtoa yule mtu kafara na kwamba wasiposimama kwenye maombi watarajie misiba zaidi.Nilikua nimetoa pesa nyingi ili mpendwa wetu azikwe kwa heshima ila nilirudishiwa zile pesa na kuombwa nikae mbali nao na niache kutumia ubini wao.

Niliheshimu hilo na nikawafuta maishani mwangu japo bado natumia ubini wao.

Kuna siku natamani na mimi niwe na shangazi,mjomba,mama mkubwa na mdogo,wapwa na mabinamu nikawatembelee na wao wanitembelee au tukutane kwenye sherehe za ndugu au niungwe group la ukoo ila ndo hata sijui ndugu zangu wa kweli wako upande gani wa dunia hii.

Mwanzoni nilikua nikipata mwanaume hata anitende vipi nakua king’ang’anizi sbb nilikua naona ndo kama baba,kaka ,mama mjomba na kila kitu so mpaka na let it go mtu anakua keshajuta kunijua😀au nipate mtu anichukulie kama ndugu yake yaani nitakavyojitoa na kumspoil na ikitokea akanitenda huwa naumia sana.

Hata hivyo kwa sasa rafiki zangu ndio ndugu zangu japo sitaki wajue kuwa sina ndugu sababu nahisi wataniona wa ajabu .Sometimes wakihadithia kuhusu ndugu zao na mimi nahidithia vya uongo 😃ila ukweli ni kuwa

ikitokea mimi na mwanangu tumekufa leo mali zangu zitakuwa chini ya kanisa katoliki zikawafae yatima.

MIMI NI KATAA NDOA🤪ila naaamini ndoa ni kitu kizuri ila kwa upande wangu nikifikiria kuanza kuchanganya mambo ya uchumi na ikitokea tumeachana nawaza itakuwaje ktk kugawana mali na vitu kama hivyo basi naona acha niwe nungayembe😀.

NB: Atakayenisaidia kudaka risasi za watakatifu na za anti-single mothers nina vocha yako😃
Asante kwa kuunga mkono juhudi KATAA NDOA. kongole kwako kwa maisha uliyoyachagua na kila la heri
 
Na hapo kwenye kutokuwa na life partner aisee...sijui nisemeje ila two is better than one
Nakuombea upate mmoja atakayekupenda kama ulivyo bila kuangalia financial statement yako
Upweke mbaya sana bestie
I know bestie ila maisha yangu tayari yako kwa mvuragqno mambo ni mengi ila wazungu wanasemq never say never acha nibakishe akiba ya mneno
 
Salama mkuu.
Asante kwa kujali.
Nitakaribia ila hakuna kitakachobadilika🙏🏼
TRUst me, kipo kitakachobadilika wewe uje kwenye ibada utaona tofauti,nimeenda na watu ambao sio hata wakristo na maisha yamebadilika kwa sass nina ushuhuda wa kutosha Mchungaji Florian katunzi ana neema ya tofauti sana na ana vitabu hapo amevandika unaweza nunua na kusoma ni vizuri sanasana, huyu ni.mchungaji wa kweli sio wa mafuta wala upako, huyu ni mchingaji wa kweli amini ninalokwambia maana nimethibitisha kwa macho uje kwa kweli utapona na utapata mtazamo.mpya.mimi nakupenda sana dada yangu Bwana Yesu amekukumbuka amen.
 
Ndio.
Na unaona bora uendelee kulisongesha
mkuu kuna maswali unayaruka. kuna uzi ulianzisha mwaka jana ukiamini matendo ya Mungu leo umegeuka na unasema ni tangia utoto. emu fafanua hili.
 
TRUst me, kipo kitakachobadilika wewe uje kwenye ibada utaona tofauti,nimeenda na watu ambao sio hata wakristo na maisha yamebadilika kwa sass nina ushuhuda wa kutosha Mchungaji Florian katunzi ana neema ya tofauti sana na ana vitabu hapo amevandika unaweza nunua na kusoma ni vizuri sanasana, huyu ni.mchungaji wa kweli sio wa mafuta wala upako, huyu ni mchingaji wa kweli amini ninalokwambia maana nimethibitisha kwa macho uje kwa kweli utapona na utapata mtazamo.mpya.mimi nakupenda sana dada yangu Bwana Yesu amekukumbuka amen.
🙏🏼🙏🏼
 
mkuu kuna maswali unayaruka. kuna uzi ulianzisha mwaka jana ukiamini matendo ya Mungu leo umegeuka na unasema ni tangia utoto. emu fafanua hili.
Uzi upi huo mkuu nitag.
 
Mungu yupo Prida. The presence of adversity in your life does not guarantee the absence of God. More than 2000 years ago there lived a man called Job whose adversity shocked the early Eastern Middle East and Asian Continent . Sasa rafiki yangu adversity yako hata haijaenda viral ubamkana Mungu kweli {thanks for understanding sijaribu kuweigh down your pain} Read the book of Job with an open heart and willingness to understand God.

Lakini si hivyo tuu life is eternal . Our mortal bodies will perish but our souls will live for ever , our for ever is determined by our today’s choice of either accepting There is a God who loved us so much that He gave His only begotten son Jesus Christ to die for our sins and he rose in victory so as we may be heirs of God’s kingdom that’s eternity in Heaven. Or denying God and spending the res of your eternal life in a burning hell which was prepared for Lucifer the fallen angel alone and enemy of God’s mankind.



With love ❤️

A brother in the Lord!
 
Mungu yupo Prida. The presence of adversity in your life does not guarantee the absence of God. More than 2000 years ago there lived a man called Job whose adversity shocked the early Eastern Middle East and Asian Continent . Sasa rafiki yangu adversity yako hata haijaenda viral ubamkana Mungu kweli {thanks for understanding sijaribu kuweigh down your pain} Read the book of Job with an open heart and willingness to understand God.

Lakini si hivyo tuu life is eternal . Our mortal bodies will perish but our souls will live for ever , our for ever is determined by our today’s choice of either accepting There is a God who loved us so much that He gave His only begotten son Jesus Christ to die for our sins and he rose in victory so as we may be heirs of God’s kingdom that’s eternity in Heaven. Or denying God and spending the res of your eternal life in a burning hell which was prepared for Lucifer the fallen angel alone and enemy of God’s mankind.



With love ❤️

A brother in the Lord!
Asante kwa neno mkuu❤️
Samahani mkuu ila meenzio nimekulia kanisani na nitafia kanisani.Sina neno sijasikia kutoka kwa watumishi wakubwa na wadogo ila ndo hivyo labda nimuone Mungu live ndo nitaamini yupo..

Pepo yangu nafight kuitengeneza hapa duniani.
Akhera pia ipo hapa duniani na kuna watu wanaiiishi
 
Back
Top Bottom