Hongera kwa ujasiri mtoa mada. Ni hivi karibuni nimeamua kwa amani na akili zangu timamu kuwa atheist. Na mimi nimetokea kwenye mwamvuli wa Dini, na mimi nilitawazwa kuwa Mchungaji na ni mhubiri mzuri japo si maarufu. Simu yangu imejaa gospel za worship tena zile za kuugumia lakini maisha haya yamenifundisha kuwa hayupo Mungu wa kuja kuniokoa kwenye shida yangu yoyote ile. Wala sijifariji kuwa eti atalipa mabaya kwa wale walioniumiza, hayupo Mungu huyo 😂
He's too busy I guess. Nimeamua kujisifu mimi mwenyewe maana nina uungu ndani yangu. Nimeamua kuumba mwenyewe uhalisia wa maisha yangu. Kilichobaki ni Kuangalia namna ya kumsaidia mwanangu wa kiume kukua katika maadili mema awe na manufaa kwenye jamii yake. Hivyo nakuelewa.
It's a painful reality knowing kuwa hayupo huyo Mungu tunayemtegemea.