Kimsingi watu wanaofanya mambo ya hivi huwa wanaamini ni namna ya kuonyesha kuwa umeshakuwa karibu na partner wako na upo nae comfortable kufanya lolote mbele yake.
Ila wanasahau kuwa watu wanatofautiana malezi na huu sio utamaduni wa jamii yetu ya kiafrika nadhani hata huko magharibi pia sio utamaduni wa kawaida.
Hizi ni tabia ambazo watu hufanya kwa kuiga lifestyle za mitandaoni ile ameona picha ya mwanamke yupo na boyfriend wake chooni halafu caption inasema "when you and bae are BFF at this level, love wins" au video ya demu wa kizungu anamjambia boyfriend wake kisha wanacheka kwa utani, wao mabinti wa kibongo wakiona vile wanaona haya ndio mambo ya kufanyiana na wapenzi zetu au akamfanyie mume wake.
Wanasahau kuwa nje ya mbwembwe za mitandaoni za meme za mahusiano, mahusiano yana misingi na kanuni zake za kuyaendesha. Hayaendeshwi kama vile akili inataka.
Kama huyo mkeo anataka kunogesha mahusiano why asicopy mambo ya tofauti ambayo yatakufanya umuone mtamu na kufurahia mahusiano kama kukuleta chai kitandani, kukununulia zawadi, kuwa msafi kwaajiri yako, kukuandikia barua ya shukrani kwa kuwa nae kwenye maisha kisha akaiweka katika mfuko wa suruali yako ili uje kuiona ukiwa njiani na kuisoma ukajisikia vizuri, au akutengenezee keki tu ya kukupongeza kwa uchakarikaji wako, au akununulie nguo mpya, au kukulipia mafuta ya gari. Yaani vitu fulani ambavyo vitafanya umuone ni mwanamke ambaye anakufikiria na kujali hisia zako.
Sasa mtu anakutolea hewa chafu halafu anaona ni kitu cha kuboresha mahusiano yenu au anakuja kujisaidia wakati wewe upo bafuni hivi anajua balaa ya ile kitu smell yake sasa wewe utakuwa ukimuona unakumbuka yale matendo na atakukinai na utamuona mchafu muda wote ukimuona unakumbuka zike harufu na uchafu.
Ni kukosa akili na adabu tu huko hakuna swala lingine hapo.