Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Tuchague lugha moja ya kufundishia kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
Ningekua mimi ni kiongozi maramoja ningechagua lugha moja iwe ya kufundishia kuanzia shule ya chekechea mpaka chuo kikuu.
Nilipata kuhudhuria kongamano moja tulikua nawaganda kwakweli sisi kiingereza kinapiga chenga na hata wengi wanaokizungumza wanazungumza maneno machache Sana.
Umesema kweli, hili ni jambo zuri japo mwanzo wake utakuwa mgumu kwa kuwa nachangamoto nyingi lakini ni jambo linawezekana.Kiswahili automatically kila mtoto akizaliwa ataongea tu.
Me nashauri tu lugha ya kufundishia kuanzia chekechea iwe kiingereza tu.
Na wote wanaopinga lugha ya kufundishia kuanzia chekechea mbona watoto wao wapo shule za English medium na International schools?
Kwanini hawataki kuwaangalia watoto wa maskini wanaongia shule za public wasio na uwezo wa kupeleka watito wao English medium na International School?
Ifike mahali viongozi wanaosimamia Educational Policy waliangalie hili. Linaumiza na kudumaza watoto wengi wenye vipaji wa maskini kushindwa kucompete internationally kwa sababu ya kukosa confidence ya kuongea International language.