Hii taasis imefanya mambo mengi makubwa, huko nyuma, lakini kwa sasa ni muhimu sana ikaangaliwa kwa jicho la karibu na la kipekee ili iweze kukabiliana na ulimwengu wa sasa. Kuna makosa makubwa yamefanyika miaka ya karibuni kwenye 'recruitment', mafunzo na hata usimamizi mzima wa maofisa wake.
Zamani, hata ungemshikia bwana/bibi usalama panga, asingekubali kuwa yeye ni mtu wa usalama. Lakini leo kuna waha vodafasta wamezagaa kila mahali, wakijigamba wanakofanya kazi. Utendaji mbovu na 'kulundikiwa' watu wasio na uwezo wa kazi, naamini unawakatisha moyo hata wale watendaji wazuri. Mwisho wa siku Taasis nzima inaingia doa.
Kwa waliokula chumvi, kuna vichaa wengi sana walikuwa barabarani wakati wa Mwl Nyerere, na tetesi ni kwamba hao watu hawakuwa vichaa, bali watu wa usalama. Hata hivyo, kutokana na ueweledi uliokuwepo kipindi hicho, ilikuwa vigumu kupata ukweli, maana watu wa usalama hawakuwa wanaongea hovyo kama hawa wa siku hizi.
Kwa sasa hivi kuna milango iko wazi mno kwa adui kuingia kwenye 'damu' ya Tanzania. Kwa ujumla vipaumbele ni vya kupitia, siasa iondelewe, na pia tusiIgeuze hii taasis kuwa kama 'wambea wa mtaani kwetu', kwamba unata watu wachunguze fulani anasemaje kuhusu nguo yangu, au baiskeli yangu?
Pamoja na siasa zetu lazima tuwe na chombo imara kinachosimamia Tanzania.