utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,813
Tiss ndio mkombozi pekee wa mtanzania aliebaki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tiss ndio mkombozi pekee wa mtanzania aliebaki
Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali.
Wadadisi wa masuala ya kiusalama wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lilipo,
Naelewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.
Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.
Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015.
Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,
Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,
Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"
Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.
Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (rais) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,
Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe)
Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa na machafuko ya kiroho.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.
Yote ni muhimu yakatazamwa, lakini muhimu zaidi ni sheria na teknolojia
Miaka ya nyuma utendaji kazi wa taasisi hii haukuarithiriwa sana na mapungufu ya sheria hii, hilo lilitokana na mfumo wa siasa ya nchi hii kuwa ya chama kimoja, na uimara wa viongozi waliopita hasa kwa weledi na uadilifu,hivi kwa upande wa sheria unataka kusema miaka kadhaa ya nyuma performance ya TISS iliathiriwa na sheria hii?
Kuhusu technolojia,mbona inasemekana matumizi ya tecknolojia yamepunguza usiri wa kazi hii?
Usalama wa Taifa wameshindwa hata kudhibiti njaa nchini.
hahahaaaaaa. kumbe hawa usalama wa taifa ni hatari sana. kumbe wanaweza kuzuia hata mvua zisinyeshe?
What is this? Mental dyslexia?
Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali.
Wadadisi wa masuala ya kiusalama wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lilipo,
Naelewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.
Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.
Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015.
Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,
Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,
Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"
Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.
Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (rais) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,
Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe)
Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa na machafuko ya kiroho.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.
unajua kiranga, kuna watu nafikiri wana utindiwa wa ubongo. badala ya kuchangia hoja za msingi wanaanza kuiona idara dhaifu eti kwa sababu kuna njaa nchini. badala ya kuanza kuangalia nini chanzo cha kuwepo kwa tatizo la njaa mtu anapita njia ya mkato ya kuilaumu idara. hata matokeo ya form four 2012 yalivyokuwa mabaya kuna watu nimewasikia wanaigusia idara
Hiyo sheria isiyoipa meno TISS ilianzishwa lini? Tangu wakati wa Nyerere hiyo sheria ilikuwa hivyo hivyo ilivyo na bado usalama wa taifa walifanya mambo makubwa yenye tija kwa taifa, hata kuipelekea Tanzania kuwa nchi ya mfano katika suala zima la amani na usalama wa raia.
Nionavyo mimi, tatizo si sheria, ila tatizo ni mfumo wa serikali, hasa hii ya Kikwete kuendesha mambo kishikaji na kwa maslahi binafsi. Wakati zamani mtu alikuwa anaingia kwenye idara ya usalama wa taifa kutokana na maadili yake na pia uwezo wake wa kuchambua mambo na akili za darasani pia, siku hizi unaingia usalama wa taifa kupitia wazazi, ndugu na marafiki. Usalama wa taifa imekuwa ni ajira on its own, mzazi ambaye mtoto wake amefeli shule anampeleka usalama wa taifa. Zamani mtu anaweza kuwa mwalimu by profession lakini anafanya kazi za usalama wa Taifa, ndivyo ilivyokuwa wakati wa Nyerere. Lakini siku hizi usalama wa Taifa wanakaa ofisini. Nawafahamu usalama wa Taifa waliokuwa wanachoma chips pale Ilula miaka hiyo, lakini miaka ya leo ni usalama wa taifa gani atakayekubali kwenda kuchoma chips?
La pili, zamani usalama wa taifa ulikuwa unafanya kazi kwa maslahi ya taifa, sasa hivi usalama wa taifa, wanapokea rushwa! Kwa hiyo kwenye dili kama hizi za wizi wa pembe za ndovu usalama wa taifa wanakula cha kwao na kuwasaidia wezi kupitisha pembe za ndovu. Na sababu kubwa ya hili ni huu mtindo mpya wa kupeana nafasi za usalama wa taifa kwa misingi ya undugu na kujuana badala ya ule utaratibu wa zamani wa kumwandaa mtoto tangu yupo shule ya msingi kutokana na maadili na umakini wake katika utendaji wa mambo. Siku hizi wezi wanawapigia simu usalama wa taifa kuomba wapitishe mzigo wa wizi, zikiwemo nyara za taifa. Sasa hawa ukiwapa full authority si watafagia kila kitu?
Na lingine, viongozi wa serikali ni wababe wa kutetea maslahi yao binafsi na wasio na uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma. Watu kama akina Pinda hata wakiletewa taarifa yenye ushahidi wote kwamba Illunga ametangaza waislam waue maaskofu, ataanza ....nafikiri nafikiri tumpe kwanza muda tuone kama ataendelea. Watu wanahamisha hela mchana kweupe kupeleka nje ya nchi, lakini taarifa hizi zikifika kwa akina Kikwete wanampigia simu mwizi na kumwambia niwekee na mimi kiasi fulani kwenye akaunti yangu ya UK ili nikulinde. Katika hapo huwezi kutalajia ufanisi wowote.
Kwa mawazo yangu, badala ya kufikiria kubadilisha sheria, tubadilishe viongozi wa nchi pia tubadilishe mfumo wa kuwaajiri hawa usalama wa taifa ili wawe hakika kwa ajili ya maslahi ya taifa na si vinginevyo. Kwa mfano wazo la kubadili hiyo sheria linaweza kuwa ni la hovyo sana katika wakati huu ambapo usalama wa taifa wanakula rushwa na wanafanya kazi kwa maslahi ya watu na chama fulani. Hivi niambie usalama wa taifa wakiwa na mamlaka kamili na wana rungu la kuitetea CCM au kuhalalisha rushwa ya uchaguzi unafikiri kuna kitu kitatoka salama hapo?
Mimi naona wabaki kama washauri lakini wawe na mahali pengine pa kusemea. Kwa mfano wawe na opportunity ya kushare mambo yao na kamati ya bunge ya ulinzi na usalama. Hii itasaidia kuwapa habari wananchi iwapo kuna mambo ya hatari kwa taifa ambayo Rais ameambiwa lakini hajataka kuchukua hatua. Kwahiyo wakiona Rais amewapuuza basi wapeleke habari kwenye kamati ya bunge ya ulinzi na usalama kwa ajili ya hatua zaidi. Hili kidogo linaweza kusaidia kuliko wao wenyewe kuchukua hatua. Na hasa pale ambapo siasa zinaingilia mfumo wa usalama wa taifa.
Nafikiri turudishe nchi yetu kwenye mfumo na maadili yanayokubalika ya uongozi. Na kwa mtizamo wangu, kama nilivyowahi kushauri wakati fulani, ni kwamba kama ataingia kiongozi mwenye maadili mema ni vema avunje kabisa hili jeshi la usalama wa Taifa na aanze kuliunda upya. Hili lililopo sasa lipo totally polluted. Na uongozi wa serikali ndiyo ten times polluted, full utilization ya usalama wa taifa kwa maslahi ya watu na maslahi ya chama fulani. Usalama wa taifa wa sasa uvunjwe, uundwe upya, kwa kuzingatia miiko, maadili na maslahi mapana ya taifa.
Hakuna ubishi kwamba taasisi hii imefanya mengi katika historia ya nchi yetu. Jambo la kusikitisha ni jinsi utendaji wa asasi hii ulivyoporomoka ghafla katika awamu mbili ambapo kumefanyika uhalifu dhidi ya taifa bila ya wao kuchukua hatua. Yaelekea wanasiasa wamefaulu kuwachakachua na sasa wana behave kama watumishi wa mtu Binafsi.Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali.
Wadadisi wa masuala ya kiusalama wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lil)lewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.
Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.
Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015.
Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,
Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,
Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"
Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.
Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (rais) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,
Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe)
Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa na machafuko ya kiroho.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.
Tatizo lako unaangalia mambo katika mawazo mgando wakati dunia ina evolve.
Nilikuwa naongea na Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kipindi hicho, Dr. Augustine Philip Mahiga, mwanadiplomasia aliyebobea ambaye aliwahi kuwa mkuu wa usalama wa taifa kabla hata usalama wa taifa haujarasimishwa, enzi za Nyerere. Kuhusu challenges za usalama za ulimwengu, na Tanzania, hususan in the wake of 9/11.
Dr. Mahiga, mmoja kati ya ma dokta wa ukweli ninaowaamini Tanzania ambaye akiongea mtu unamjua huyu ni msomi hata kabla hajakuambia "mimi ni Balozi Dr. Mahiga", akaniambia mataifa makubwa yana ajenda zao za usalama na ajenda hizi si lazima ziwe sawa na ajenda za mataifa madogo katika suala la usalama.
Tukazungumza sana jinsi gani swala zima la "food security" linavyokosa kuongelewa vizuri Umoja wa Mataifa kwa sababu tu mataifa makubwa yamekazania "terrorism" in the context of Al-Qaeda and similar threats.
Akajenga hoja, ambayo sikuweza kuipinga, kwamba huku nchi masikini kwetu njaa inaweza kuwa "terror" kubwa kuliko Al-Qaeda, na at least inatubidi tuipe kipaumbele angalau sawa na hizo habari za Al-Qaeda, kama si zaidi.
Alielewa "food security" as a part of "national security".
Sasa wewe unakuja na one track mind kufikiri tu kwamba "usalama wa taifa ni mashushushu, kazi yao ni upelelezi na ujasusi". Period. Huwezi kuona kwamba hata "food security" ni sehemu ya usalama wa taifa.
Na kama tuna ukame periodically, Usalama wa taifa unatakiwa kuandaa contingencies za kuweza kukabili ukame wakati wowote.
Na kwamba sehemu yoyote kukiwa na ukame ni failure ya food security ambayo moja kwa moja ni failure ya national security, hata in the context ya "a hungry man is an angry man" tu. Mitatizo kibao ya wananchi kuchoma moto nyumba za wabunge na wakuu wa mikoa ukiiangalia kwa juu juu utaona ni masuala ya failure ya usalama wa taifa katika context ya usalama wa taifa kukosa kujua nini kinaendelea na ku project nini kitatokea, lakini ukiangalia zaidi utaona ni failure ya usalama wa taifa zaidi kwa sababu ina correlation na food security.
Njaa ni mafuta yanayosubili cheche tu kulipuka na kutoa vurugu.Usalama wa taifa .
Njaa inaleta vishawishi hata mwananchi ahujumu nchi yake mwenyewe. Usalama wa taifa.
You cannot talk about addressing national security if you cannot address food security.