Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama mmoja wa raia wa Tanzania una haki ya kujua usalama wa Taiafa nini?Kwa miaka ipatayo 51 sasa toka tumepata uhuru mtanzania wa kawaida ajajua maana ya usalama wa Taifa ina maana lengo kuu la Usalama wa Taifa halijatimizwa ilivyopaswa kwa uhalisia na uhakika usio tiliwa shaka na raia yoyote yule mwenye ufahamu wa kawaida [normal citizen] achilia mbalia raia mwenye upeo wa juu wa ujuzi wa mambo ya binadamu na mahusiano yake na viumbe wengine na mazingira yake [intellectual citizen].Naomba kuelimishwa usalama wa taifa ni nini?
Mkuu hii issue ilishapita huku tukajadiliana.Ni kweli TISS inamchango mkuu uliotukuka,lakini msimamo wa mbio za vijiti usiozingatia umahili wa kitaahasisi na nyakati hakika usalama wa Taifa kama jina lilivyo utakuwa shakani.Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali........
Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"
Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.
Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (rais) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,
Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe)
Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa na machafuko ya kiroho.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.
Rejea maandiko ya Yericko "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"usalama wa taifa wa kiukweli ulikuwa active under the late Mwalimu -- huu wa sasa unaegemea umekuwa kama usalama wa ccm.
Kwa mfano haya mambo ya rushwa za mabilioni , udini kuchinjana kwa imani za kidini, kuchoma makanisa, ukabila, ujangiri hadi watu wanatotosha twiga nje ya nchi, madawa ya kulevya, ushirikina (kuua maarubino) nk haya yanatakiwa yashughulikiwe na usalama wa taifa.
sasa ukiona vituko kama hivi unaweza kuhoji uwepo wa taasisi nyeti kama hii.
binafs naona policy yao ni kuwashughulikia wanaowakosesha usingizi,na wanafanikiwa japo kwa shida.:tape2:You guys are missing a fundamental principle kwenye national intelligence services - intelligence policy. Hivi mmewahi kujiuliza intelligence policy ya Tanzania ni nini? Hivi mnajua sera ya CCM kuhusu Intelligence ni nini?
nao wamekuja na utaratibu wao si mbayayericho, tatizo la msingi kwenye hii taasisi sio la kisiasa bali la wanausalama wenyewe. Ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa tatizo lake la msingi linaanzia kwenye recruitment yaani usahili. badala ya kutumia utaratibu aliuacha mwl. Nyerere ambao unatumika pia na mataifa mengine ambayo taasisi kama hizi zinanguvu. Utaratibu ni kwamba usaili sio zoezi la siku moja bali la miaks kazaa.
Mtu anachunguzwa kuanzia familia yake, primary, secondary hapo kama wamelizika wanamchukua na wengine walikuwa wanachunguzwa mpaka level ya chuo na ndiyo wanachukuliwa lakini sasa hivi wanausalama wenyewe wanashangaana kuwa huyu wa tabia hii ameingiaje humu? Kuna ukabira, udini, ushost, na mpaka ubazazi katika kupata kazi huko. Watu wameona ndiyo sehemu ya kuficha ndugu zao wasio na sifa.
Pamoja na kupewa meno na bunge lazima wabadilishe utendaji wao na ndiyo jamii itawapa heshima yao sitahiki. Vinginevyo watapewa meno na watayatumia kuuma watu wasio na hatia na kuwaacha wenye hatia wakijinafasi kama zilivo sekta nyingine za kutoa haki.
nao wamekuja na utaratibu wao si mbaya
hivi kama shirika hili likigeuzwa na kuitwa shirika la ujasusi la Tanzania itakuwaje?
Mkuu Mwanakijiji umegusa jambo muhimu sana,You guys are missing a fundamental principle kwenye national intelligence services - intelligence policy. Hivi mmewahi kujiuliza intelligence policy ya Tanzania ni nini? Hivi mnajua sera ya CCM kuhusu Intelligence ni nini?
Asante sana mkuu kwamchango wako murua, hakika taifa linaweza kufanya mageuzi makubwa ya taasisi hiiMkuu hii issue ilishapita huku tukajadiliana.Ni kweli TISS inamchango mkuu uliotukuka,lakini msimamo wa mbio za vijiti usiozingatia umahili wa kitaahasisi na nyakati hakika usalama wa Taifa kama jina lilivyo utakuwa shakani.
Binafsi nilichangia na kutoa mada kwenye angle ya TISS humu jamvini na nikasema umefika wakati TISS watoke kuwa IDARA [Department] wawe Taasisi timilifu [INSTITUTIONAL] yenye kujitosheleza na idala yake.Kwa kupewa nafasi ya kuwa Taasisi haki sheria unayo lia nayo tayari itakuwa imekufa kifo cha pekee yake na matamanio ya kuiona taasisi [by now department] yenye meno itakuwa imetimia.
Kwa TISS kuwa taaisisi matamanio yangu kwaweza kuzaliwa idara madhubuti zenye kwenda na nyakati kama idara
1: Ulinzi wa Viongozi
2: Elimu na Mambo ya Sayansi na Technolojia
3: Ujasusi ndani na wa kimataifa
4: Siasa za Ndani [Tanzania Bara na Visiwani] na Mahusiano Ya Kimataifa
5: Maliasili watu na mahusiano ya jamii [Administration and Public Relation]
6: Uchumi na Fedha
7: Maliasili za Taifa
Kwa hayo hakika tunaweza kufika mbali na kuwa na kamati maalumu ambayo pia nayo itakuwa mlinzi wa jicho la mwenendo mzima wa TISS [Watchdog] isiwe ile misemo ya the court break become the court breaker!!inapata nafasi ya kutumika. Ina maana kwa TISS kuwa taasisi itwajibika kwa Wananchi kupitia Bunge! Na DG wao atateuliwa na Rais lakini atapitishwa na Bunge. Na Kamati ikishateuliwa inawajibika kwa bunge kutoa maoni na mwazo huru kuhusu mwenendo mzima wa taasisi hiyo ya umma yenye jukumu kubwa la kulinda Nchi ndani na nje ya mipaka ya Taifa letu. Na wao TISS kuwa na meno ya kutenda na kutoa ushauri wenye TIJA kwa TAIFA.Na makosa yao yatakayo sababisha hasara au uzembe kwa Taifa yawajibishwe kwa wale wote wenye dhamana [vested] ya kitaasisi kwa wakati huo.
Hakika kunatakiwa mageuzi makubwa na elimu kubwa itolewa kwa umma kuwa usalama wa Taifa sio uhuaji au utishaji dhidi ya raia wema. Mtanzania ajisikie raha na huru kusaidia Taasisi hiyo popote pale anpoona panastahiki kwa mujibu wa elimu aliyonayo juu ya taasisi hiyo. Leo ukiwawauliza Wamerekani FBI na CIA ni nini hakika haraka sana watakwambia nini, na raia wa Tanzania leo hii wanajua kazi za CIA na FBI kuliko wanavyojua taarifa za Usalama wa Taiafa lao.
Information is Power,kitendo cha raia wa kawaida kuelimisha kazi za Usalama kuwa ni Ulinzi wa Taifa lake kwa ushirikiano wake hakika hata upatikanaji wa taarifa zao wigo wake utapanuka.
yote uuyasemayo bwana kiranga ni sahihi kabisa na wajumbe wengi wanajaribu kuainisha maeneo mengi ambayo idara inaweza ku play part ili kuhakikisha kuwa nchi hii inakuwa salama wakati wote bila ya kuathiriwa na matatizo hayo ya nmdani. ninaamini kuwa jukumu hilo wanalitekeleza. shida kubwa iliyopo hapa ni kwa kiwango gani idara ishughulikie masuala hayo. nijuavyo mimi ni kuwa kila jambo hapa nchini kuna wizara ambayo inajukumu la kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika wizara husika. kwa issue ya food security, tuna wizara ya kilimo na chakula. kwa mujibu wa sheria ya idara ya usalama wa taifa ya mwaka 1996, ambayo mchangiaji mwenzetu ametusaidia ni kuwa iodara hii jukumu lake kuu ni kutoa ushauri kwa waziri husika. kwa vile hatuna waziri anayehusika na masuala ya usalama wa taifa, ninaamini kuwa jukumu hilo lipo mikononi mwa rais wa nchi. kwa maana hiyo ni kuwa consumer wa information za idara ni rais mwenyewe. huo ni mfumo ambao waliouandaa akina chenge wanajua lengo lake hasa lilikuwa nini. ila kwa mazingra ya sasa ni vigumu kwa informations zote wanazopata idara consumer akawa rais tu. bila shaka hapo idara itaendelea kulaumiwa. tatizo kubwa lililobainishwa na wachangiaji wengi ni la kisheria na si utendaji wa idara yenyewe
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaripoti kwa Waziri wa Utawala bora
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaripoti kwa Waziri wa Utawala bora
Sizani kama tuko na usalama wa TAIFA bali ni usalama wa wachache wenye hela zao Tz.