Mimi pamoja na kuendelea kuamini umuhimu wa chombo hiki nyeti kwenye nchi yetu bado napata tabu sana pale watendaji wake wanapo husishwa na utekaji na utesaji wa raia wanao onekana kuwa niwa pigania haki au usawa katika jamii.
Huwa nakuwa na maswali mengi bila majibu.
Mfano. Kupigwa na kutekwa kwa Dr Ully mwanahalisi lilianika namba za simu na majina ya watendaji wa chombo hiki ambao tumeambiwa wanahudumu ikulu.
Mmoja wa maafisa wa chombo hiki kwa mujibu wa Tanzania daima (sikumbuki toleo gani) alinyetisha kuwa Dr Slaa alishinda kiti cha uraisi kwa asilimia 61 na mpaka leo habari hii haijawahi kukanushwa.
Hapa ndio huwa najiuliza.
1. TISS inafanya kazi ya nani na kwa niaba ya nani?
2. TISS iko piha kwa ajili ya serikali inayo subiri nje ya dola au kazi yake ni kulinda serikali na chama dola kisianguke?
3. Kwa nini sasa hivi kuna malalamiko mengi juu ya TISS kukibeba chama tawala badala ya kuangalia maslahi mapana ya nchi bila kuegemea upande wowote?
Mkuu
Yericko Nyerere kama unaweza kudadavua haya hebu vunja kikombe.