Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Status
Not open for further replies.
Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali.

Wadadisi wa masuala ya kiusalama wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lilipo,

Naelewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.

Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.

Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015.

Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,

Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,

Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"

Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.

Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (rais) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,

Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe)

Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa na machafuko ya kiroho.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.

What kind of reforms would you like to see? Are the reforms you want viable to our socio-economic and cultural conditions?
 
TISS tatizo ni sheria dhaifu. Serikali inahakikisha kuwa sheria ziko dhaifu ili waweze kuwadhibiti watu wa TISS.

1. Kuna haja ya kuisuka tena upya taasisi hii HASA KWA KADA YA CHINI kwa kuwapatia mafunzo mazuri zaidi ya NIDHAMU. Wafanyakazi wengi wa TISS wana tatizo kubwa sana la nidhamu.

2. Majukumu yao yasizingatie nani anamjua nani. Professionalism ijengwe, itunzwe kwa maslahi ya Taifa na sio kwa maslahi ya watawala.

3. There is enormous amount of bullying/discrimination/ and other malpractices in this department that need to be sorted out.

4. Kwa sababu hakuna sheria zilizo wazi hasa kwa wafanyakazi wa kada ya chini TISS wenyewe, na hasa kwa sababu ya style yao ya slavery(creating dependency for your master to rule efficiently), hali iliyozaa kuwa wana TISS wengi kuishi kwa kutegemea rehema za maboss wao.

5.TISS ni jeshi. Lakini imekuwa ikitumiwa kama kitengo cha propaganda cha serikali.

Lakini wakati huo huo kukiwa na vuta nikuvute kati ya serikali na TISS kila mmoja akitaka kumweka mateka mwenzie! (TISS wakitaka pesa kwa kuzusha uongo/prpaganda wakati serikali inataka TISS kufanya kazi zake chafu - TISS wakiamini ni wajibu wao.
 
Kwa taifa ambalo ni ambitious,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kiakanda(regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi.TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni more sophisticated katika kufanya information sharing wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama Mkakati waq ulinzi na usalama wa Marekani,Uingereza,Pakistan,Israel,Afrika Kusini,China,India na Canada

Ingawa miakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekua sensitive zaidi kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa(Power Interests) lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe ambitious na kwa kuanzia ni lazima tungeanza na kanda yetu ya Maziwa makuu,Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na power struggle hapa east afica ambao ni Kenya.Hatujaweza vya kutosha kwenye Economic intelligence kule Kenya inagawa wao wamewekeza hapa kwetu.Leo hii Kenya ina-export TANZANITE,Wana-Export gold n.k.Balance of trade kati ya Tanzania na Kenya ni subject of Economic intelligence.tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiinteligesnsia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie possible scenarios na move za washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi hapa EAC au ukanda kupitia economic power house(Kenya) katika ukanda huu?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu yetu.Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekua zikinunuliwa kwa wingi na kuwa smuggled kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi wetu na ku-frustrate fisical na monetary policy zetu?
Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe modern zaidi
Malengo ya TISS kulingana na trend ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri(si utabiri wa majini/tunguri bali utabiri wa kisayansi),Kupenya,na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu,na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye Nyanja za kimataifa(jamii nyingine)

Malengo makuu yanatakiwa kujikita katika

Mosi,Kuongeza nafasi na umuhimu wa idara ya mahakama na vyombo vya kutoa haki.Lengo hapa linatakiwa kuwa juu ya kuunganisha idara za mahakama,wizara ya mambo ya ndani na vitengo vyake kwa kuzingatia upeanaji wa taarifa huku haki za msingi za kiraia zikilindwa pamoja na uhuru wake tofauti na ilivyo sasa ambako TISS inatuhumiwa kutumika kuhujumu haki za kiraia kwa visingizio lukuki.Lengo kuu liwe kulinda haki na uhuru wa watu bila kuathiri maslahi ya jumla.Hili linahitaji ushirikiano kuanzia serikali kuu,mikoa,wilaya,majimbo ya uchaguzi,kata na hata ngazi ya mitaa pamoja na sekta binafsi

Pili,Utengenezwe utamaduni mpya wa kuahamasisha mawazo mbadala na matumizi ya weledi(professionalism/expertise):Kubadili utamaduni ndani ya TISS ni muhimu sana ili kuepuka mimosa ya kimkakati. It is necessary to create an intellectual culture that promotes discussion as well as dissenting opinion. It will require the use of collaborative technology, where subject expertise is maximized, increased cross-agency communication, and the exploration of alternative analysis (Source: The Mercyhurst College Institute of intelligence Wikipedia Project Student Generated Articles Vol. 1 (2008-2009))
Tatu,Kurahisisha zaidi ukusanyaji wa taarifa za kintelijensia:TISS haina budi kuwa mbele katika matumizi ya teknolojia na pia ku-update wataalamu wake kitaaluma na katika matumizi ya zana za kisasa zaidi ili kurahisisha ukusanyaji huo kutoka Open-sources na kutoka Human-sources

Nne,Kuajiri watu kulingana na uwezo na taaluma zao na pia kuajiri watu ambao tayari wana ajira kwenye vitengo vingine lakini walipwe vizuri kwa ajili ya kazi ya usalama ili kupunguza gharama za kupachika watu wapya katika idara,mashirika na taasisi nyeti nchini.Pamoja na hili kitu cha muhimu watu hawa ni lazima wawe na sifa zinazofanana (common attributes) katika ujanja,uwezo wa hali ya juu na haraka katika utendaji huku maadili ya juu kabisa katika vigezo vya utendaji katika idara hii vikizingatiwa

Tano,TISS ibadili utamaduni wa kuhitaji-kujua kwenda Kuhitaji-kutoa taarifa(changing from the culture of need-to-Know to need-to-share):Ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kila ngazi ni lazima mtazamo wa idara hii ubadilike na suala la kutoa taarifa liwe ndiyo njia kuu ya kufanikisha malengo ya idara katika ngazi zote kwa hiyo kuna haja ya kuangalia jinsi taarifa zinavyofika kwa ubora unaotakiwa,kwa usahihi na kwa muda muafaka na hili ni muhimu na litasaidia zaidi kuwa karibu na watunga sera(policy makers)

Sita,Kuimarisha na kupanua zaidi uhusiano kati ya TISS na washirika wa ndani ya nchi na vitengo vingine vya kijasusi vya mataifa ya nje:Hii ni kwa kuwa tunaweza kuwa na common threats kwenye uchumi,kiitikadi,kiutamaduni,kiulinzi n.kHata hivyo taarifa za kijasusi kutoaka kwa washirika wetu ni lazima ziangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na pia tuwe na taarifa zetu ambazo tunaweza kulinganisha na taarifa za washrika wetu.Hizi kwa kijasusi zinaitwa 'Corroboration codification'
Saba,kitengo kidogo kabisa cha mwisho ndichokinachotakiwa kuwa na acces ya taarifa nyeti lakini kitengo hicho kiwe scrutinized kwa hali na mali.Hata hivyo nitajadili kuhusu juu ya mfumo wetu mbovu wa counterintelligence

Nane,Kujenga mfumo ambao ni uniform zaidi katika utekelazi kisayansi na kiteknolojia,Ni lazima sasa idara iwe centralized katika kutoa maelekezo na iwe more decentaliced katika utekelezaji kwa mtindo ambao unaitwa 'pyramid execution'.unified research itumike ili kuongeza ushirikiano na idara mbali mbali

Tisa,Mfumo wa kupongeza na kuzawadia utumike kuongeza performance

Kumi,mtindo wa kutumia miongo utumike lakini zaidi kwa haraka mtindo wa kutumia siku utumike badala ya miaka.Kwa mfano 720 days plan itumike badala ya miaka 2,180 days pla itumike badala ya 6 months plan kwa ajili ya monitoring na kuepuka urasimu na uvivu usio wa lazima

Pia ni vyema kutokana na power struggle ya ukanda tuunde vitengo vya ujasusi vya nje.kitengo hiki kifanane kwa muundo ingawa kutakua na marekebisho kidogo lakini kifanane na kitengo cha RAW cha india ambacho kiliundwa baada ya vita ya India na China.kabla ya hapo kulikua na kitengo cha IB ambacho kilikua na miaka 120 lakini hicho kilitumika kuchunguza watu zaidi na taasisi za kisaiasa.waingereza walikitumia kuwachunguza akina Mahatma Gandhi,Azad na Nehru zaidi.Kitengo cha RAW kinatumika kwa ajili ya military Intelligence na financial intelligence.Kuna haja ya kupima maofisa ubalozi wetu wanaopelekwa nje pamoja na Mwambata wa jeshi katika balozi zetu(defence attaché) kulingana na sera yetu.

Kwa bahati mbaya sera yetu ya mambo ya nje tumeipigia kelele sana ifumuliwe.Naamini Mungu akitupa uhai CHADEMA itakuja na sera bora zaidi ya mambo ya nje specifically kwa regions na strategic partners

kutoa Attributes hakukupunguzii maarifa kijana wa Masters ya India, live like a truly Masters graduated buddy!
 
Wengi humu JF hatujui kitengo hiki kinavyofanyakazi zake...Napenda niwahakikishie kuwa TISS haifungwi haijafungwa na haifungamani na taasisi, jumuiya ama chama chochote cha siasa. Method operamond ya TISS inatanguliza maslahi ya Taifa mbele. Mkiona vya elea mjue kuna watu hawalali wanapigania nchi yao yenye neema nyingi na yenye kuvutia maadui wa kila aina...Wengi wetu humu tuko projected! tunaamini tunachokiona na nirahisi kudanganyika kwa kudhani kuwa ni halisi! Adui hana sura inayotambulika, wanaweza kupitia milango ya kutoa misaada, makanisani, misikitini, kwenye taasisi ya elimu nk nk...
Kazi za TISS ni nzito na hatusababishi makelele kwakuwa hawatangazi biashara, hivy hofu ya kusema kuna tatizo la uongozi ni -Ve, Technologia TISS iko juu sana, Kimuundo TISS iko sawa, Watu wenye ueledi uliotukuka wapo wengi... Nchi hii itaendelea kuwa salama chini ya TISS kwa miaka mingi ijayo....
 
Hakuna kitu hapo, wangekuwa wanafanya kazi mambo yangenyooka tanzania, tatizo wamekuwa wala rushwa mstari wa mbele,kila mtu anaangalia hela na sio kazi, ni kama ilivyo polisi. hata wakikamata deal leo litaishia kugawana... usalama ulikuwa zamani bwana....ndg yangu ukitaka kujua hilo nenda bandalini usalama wapo lakini hivyooo, nenda mipakani usalama wapo lakini wizi mtupu kaririila siku wanaharamu wanapita... nenda airport deal kama kawa na usalama wapo ndani, mnaowafagilia hamjui kiendeleacho, kilichobakia tanzania ni usalama wa viongozi tu na si usalama wa taifa... maana hapo bandarini kila siku deal feki, meno ya tembo na kadhalika vinapita...chezea bongo wewe
 
Nini kifanyike kuondoa hali hiyo unayodai ipo mkuu?
 
Wengi humu JF hatujui kitengo hiki kinavyofanyakazi zake...Napenda niwahakikishie kuwa TISS haifungwi haijafungwa na haifungamani na taasisi, jumuiya ama chama chochote cha siasa. Method operamond ya TISS inatanguliza maslahi ya Taifa mbele. Mkiona vya elea mjue kuna watu hawalali wanapigania nchi yao yenye neema nyingi na yenye kuvutia maadui wa kila aina...Wengi wetu humu tuko projected! tunaamini tunachokiona na nirahisi kudanganyika kwa kudhani kuwa ni halisi! Adui hana sura inayotambulika, wanaweza kupitia milango ya kutoa misaada, makanisani, misikitini, kwenye taasisi ya elimu nk nk...
Kazi za TISS ni nzito na hatusababishi makelele kwakuwa hawatangazi biashara, hivy hofu ya kusema kuna tatizo la uongozi ni -Ve, Technologia TISS iko juu sana, Kimuundo TISS iko sawa, Watu wenye ueledi uliotukuka wapo wengi... Nchi hii itaendelea kuwa salama chini ya TISS kwa miaka mingi ijayo....
Hebu nikuulize swali Officer, kama sikosei Hans Kitine ndio alikuwa Boss wa TISS, lakini ni kitine huyo huyo aliyefoji invoince ya matibabu ya mke wake ili kuiba pesa za umma, sasa kama Boss ndio anakuwa namba moja kuhujumu maslahi ya umma hawa wengine hali ikoje?
 
Naomba ni kuhakikishie kuwa kila habari unayoipata si zote ni sahihi na zinaukweli...kama kuiba pesa za umma angeweza kujichotea kimya kimya mzee wa watu bila ya mtu yeyote kuhoji, hili la kufoji risiti ni muendelezo wa majitaka ambayo siku zote hutoa harufu mbaya ...
 
And your point is!!...
 
kutoa Attributes hakukupunguzii maarifa kijana wa Masters ya India, live like a truly Masters graduated buddy!

Mwenzio ametoa mchango wake wenye manufaa wewe unaleta vivu wa kike...kama huna la kuchangia chapa lapa! unataka masters ya SAUT ndo uje yeye ni msomi? shwain wewe...
 
Kitu ambacho mnapaswa kuelewa nikwamba usalama wataifa imekuwa ni kapu lawalio feli shule na maisha.

Mkubwa yeyote mwenye mtoto au ndugu aliye feli shule au maisha mtaani maisha yamemshinda anaunganishiwa usalama wataifa. Hii ni aibu kubwa sana kwa taasisi yenye majukumu nyeti kama hii. Imekosa kabisa mwelekeo na maana hasa kipindi hiki cha awamu ya jk.

Utakuta vijana mtaani wanalewa ovyo na kujigamba eti ni usama wataifa. Wengine tumesoma nao shule na wakafeli leo hii unawaona kwenye misafara ya viongozi wa nchi.

Chaajabu zaidi maadili yakazi hakuna utawakuta wana pepeta umbea na kuvujisha siri za ofisi! Sijui tutafika wapi kama kweli hali ndo hii.

Waneshindwa kabisa kusimamia sheria na taratibu zinazo waongoza na kuanza ushabiki wa siasa.

Utasikia mtu anajiita usalama wataifa anasema chadema hawaendi popote, hawana ujanja kwani kule tumejaza vijana wetu wa usalama wataifa! Unajiuliza kazi ya usalama wa taifa ni kuitumikia ccm au maslahi ya nchi?

Sasa usalama wataifa umegeuka kuwa chama cha siasa badala ya taasisi yauma? Nilazima hii taasisi iondoke chini ya mwenekiti wa ccm yaani ikulu na iwe huru kwa maslahi ya uma na sio ccm! Hii ni aibu sana kwa nchi.
 
Mwenzio ametoa mchango wake wenye manufaa wewe unaleta vivu wa kike...kama huna la kuchangia chapa lapa! unataka masters ya SAUT ndo uje yeye ni msomi? shwain wewe...
sio mchango wake bali ni kazi ya mtu aliyeigeuza yake tuliyokuwa tunaongelea humu ndani kuhusu Dr Shayo ndiyo yanafanywa na kijana wa masters toka india sasa!
 
Well, tunaweza kusema mengi sana ya kwamba usalama wa taifa wamepoteza dira ama la. La msingi ni kwamba sheria ya usalama wa taifa inawabana. Usalama wa taifa wanariport kwa president, na president ndio anatoa maelekezo kwa vyombo husika vya usalama kama jeshi la polisi, mahakama ama JWTZ. Kwa hiyo umahili wa president ndio unaamua kama usalama wa taifa uonekane uko makini ama la. Lakini pia wao ni washauri tu, kwa lugha nyingine ni watafuta taarifa na kuzitoa, basi. Kama kuna la kufanya mpaka waelekezwe kufanya hivyo.Hii ni sheria inayowabana, na inawafanya waonekane mambulula pindi tuwapo na president mbulula. Naamini jamaa wanakusanya taarifa na kuzifikisha mahali husika, utekelezaji wa taarifa hizo ndio tatizo. Hiyo pekee inatosha kuwakatisha tamaa hivyo kuwapelekea kufanya kazi kivivu.Turekebishe sheria, usalama watafanya kazi yao, wako poa
 
Mkuu Yericko umeongea sana. What do u think would be wayfoward mzee??

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Well, tunaweza kusema mengi sana ya kwamba usalama wa taifa wamepoteza dira ama la. La msingi ni kwamba sheria ya usalama wa taifa inawabana. Usalama wa taifa wanariport kwa president, na president ndio anatoa maelekezo kwa vyombo husika vya usalama kama jeshi la polisi, mahakama ama JWTZ. Kwa hiyo umahili wa president ndio unaamua kama usalama wa taifa uonekane uko makini ama la. Lakini pia wao ni washauri tu, kwa lugha nyingine ni watafuta taarifa na kuzitoa, basi. Kama kuna la kufanya mpaka waelekezwe kufanya hivyo.Hii ni sheria inayowabana, na inawafanya waonekane mambulula pindi tuwapo na president mbulula. Naamini jamaa wanakusanya taarifa na kuzifikisha mahali husika, utekelezaji wa taarifa hizo ndio tatizo. Hiyo pekee inatosha kuwakatisha tamaa hivyo kuwapelekea kufanya kazi kivivu.Turekebishe sheria, usalama watafanya kazi yao, wako poa
Inashangaza yani Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kuarest? basi TRA ni zaidi ya Usalama wa Taifa maana kuna maofisa wao wa juu wana mamlaka ya kuarest in the manner of TAXES issue.
 
Wengi humu JF hatujui
kitengo hiki kinavyofanyakazi zake...Napenda niwahakikishie kuwa TISS
haifungwi haijafungwa na haifungamani na taasisi, jumuiya ama chama
chochote cha siasa. Method operamond ya TISS inatanguliza maslahi ya
Taifa mbele. Mkiona vya elea mjue kuna watu hawalali wanapigania nchi
yao yenye neema nyingi na yenye kuvutia maadui wa kila aina...Wengi wetu
humu tuko projected! tunaamini tunachokiona na nirahisi kudanganyika
kwa kudhani kuwa ni halisi! Adui hana sura inayotambulika, wanaweza
kupitia milango ya kutoa misaada, makanisani, misikitini, kwenye taasisi
ya elimu nk nk...
Kazi za TISS ni nzito na hatusababishi makelele kwakuwa hawatangazi
biashara, hivy hofu ya kusema kuna tatizo la uongozi ni -Ve, Technologia
TISS iko juu sana, Kimuundo TISS iko sawa, Watu wenye ueledi uliotukuka
wapo wengi... Nchi hii itaendelea kuwa salama chini ya TISS kwa miaka
mingi ijayo....

Mkuu ueledi wa TISS ulionekana pale;

(1) Tulipouziwa radar kwa bei ya kuruka.
(2) Wezi wa EPA kushindwa kukamatwa
(3) Twiga kubebwa wazima wazima pale KIA
(4) Shimbo kujichotea yale matrilion atakavyo
(5) Wauzaji wa madawa ya kulevya kuendelea kutembea vifua mbele hapa mjini etc....

Ila kazi ya kuwatoa wananchi meno, kucha na sasa macho inaonekana. Nawapongeza sana TISS, najua majukumu yenu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom