Yericko tiss ilikuwa zamani sio sasa hivi ajira zake zinakwenda kwa vimemo, mtoto wa flani, nepotism nk. Nahisi sasa hata kagame ameshapenyeza watu wake pale sbb tuko vulnerable sana. zamani kuajiriwa pale mtu alikuwa vetted toka kijijini kwake alikozaliwa, shule aliyosoma na kila sehemu aliyopitia nk.
nakumbuka rafiki yangu mmoja aliajiriwa na tiss enzi hizo. kwanza yeye hakujua sbb kazi hii ilikuwa haiombwi na mhusika. watu walichujwa. jamaa kanambia kuwa alitumiwa ujumbe aende stand ya msamvu morogoro enzi hizo na kuwa ataikuta landrover ya kijivu saa sita mchana na akiikuta apande. baada ya hapo hakuonekana mwaka mzima na alivyorudi hakusema alikuwa wapi. lkn alitokea kuwa mmoja wa maofsa mahiri kitengoni.
hali ni tofauti na sasa. vuka tu pale ng'ambo ya makao makuu ya tiss kwenye bar ya SIMBA KAPAKATWA utawakuta wanakunywa pombe huku wakiongea mambo nyeti ya usalama wa nchi wakiwa njwiii. hakuna maadili wala secrecy ya masuala ya nchi. katiba mpya nadhani inaweza kuja na solution ya tatizo hili.
Nini kipimo cha ufanisi wa taasisi nyeti kama hii???? Nafikiri taasisi hii bado inafanya kazi japo kunawachache hawazingatii maadili. Hili la maadili sio kwa TISS tu ni kwa profesion zote, mwalimu anaeuza mtihani unamchukuliaje, dk anaeuwa au toa siri za wagonjwa, muhandisi anaesimamia kazi zake substandard(anajua jengo linahitaji 100 bags of cement yeye anajifanya kubalance, anaiba mifuko hamsini na anatumia hamsini baada ya muda jumba linaporomoka unamchukuliaje, mwanasiasa anaetumia na kupotosha ukweli ili apate madaraka kwa ngozi ya kondoo,ni mengi lakini niishie hapo halafu nije kwenye maada yenyewe.
Kulinganisha mambo wakati wa Nyerere na sasa kunawezekana si sawa, kwani zamani mlikua hamna uwezo wa kujadili TISS kama sasa, sasa kunauhuru mkubwa sana, ndio maana watu wengie humtukana hata rais wa nchi. Kwangu mimi utendaji wa TISS pengine ni bora kwa sababu za globalisation wameweza kuiweka nchi yetu kwenye usalama japo kuna pressure za hapa na pale. Mimi nafikri hawa mabwana wanatakiwa kuongeza umakini wa kazi zao.
Suala la maadili ni suala la taifa zima kwani kama mfumo wa taifa hauna maadili bora usitegemee kuwapata TISS wa maadili bora kiurahisi, tubadilikeni sote kuanzia ngazi ya familia muone kama hawatapatikana bora zaidi. Ofcourse chain yao ni kubwa manake wakati mwingine unatakiwa kuwa undercover wa vijiweni au wala dope, unategemea kuniteract kiulokole ili kudetect uhalifu waaina hiyo kweli??? Inabidi kujichanganya nao ilikujua japo ww hutovuta dope.
Nafikiri tusiwalaumu ukizingatia hatujui nijinsi gani wanafanya kazi zao ila wale wanaokiuka maadili waache ili taasisi isipakwe madoa. Mungu ibariki Tanzania.