TUKIANGALIA ASILI YA MWANADAMU KUANZIA MWANZO KABISA.....
Mungu hakutuumba ili tuishi hapa Duniani bali alikusudia tuishi huko mbingu nyingine.
Kama umesoma dini "in details" utakuwa unafaham kuwa zipo mbingu (universe 7) na hii ya kwetu ikijumuisha Sayari zote ndio ya kwanza kabisa kutokea chini.
Sasa baada ya kuwa tumemkosea kupitia kwa baba yetu Adam, Mungu akaona atushushe huku mbingu ya chini kabisa kama sehemu ya Mtihani........TAMBUA KUWA, HAPA TUPO KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI
Kwa wale watakaofaulu, wakitwaliwa watarudishwa ile mbingu aliyokuwa akiishi Adam na mkewe Hawa(kabla ya kushushwa Duniani) na wale watakaofeli basi watapata adhabu kali sana.
Na hii inaingia akilini kabisa kwani haiwezekani, haya majizi, wachawi, wanaotesa wengine bila sababu, wauaji nk nk yapite tu hivi hivi; Lazima kuna mahala haki itatolewa.....
Kwa bahati nzuri Mungu kwa upendo wake akatupa na "marking scheme" kabisa ambayo ni QURAN pia Torati, Zaburi na Injili/Biblia kwa vizazi vya nyuma; kazi kwetu, kufaulu mtihani
Nirudi kwenye mada; Ukiambiwa kusudi la kuletwa duniani ni kumuabudu Mungu...maana yake ni kuwa, Watu wakinyenyekea kwa Mungu, watafanya matendo aliyo yaamrisha (kuepuka Wizi, Uchawi, kupunja kwenye mizani, kupindisha sheria, Uasharati nk) na hivyo kufaulu mtihani.
HUWEZI KUSEMA UNA MUABUDU MUNGU HALAFU UNAFANYA MATENDO MACHAFU ALIYOYAKATAZA , HUKO NI KUUCHAFUA UTUKUFU WA MUNGU!
Kwa utalaam uliopo hapa duniani hadi sasa hatujaweza kuona huko nyuma ya Jua kuna nini, inamaana hata mbingu ya pili hatuna elimu nayo....