Nadharia yangu namba 5 kwanini binadamu tumeumbwa duniani

Nadharia yangu namba 5 kwanini binadamu tumeumbwa duniani

Nimekuwa nikisema mara nyingi kuwa sikubaliani na fundisho la Dini hizi( Abrahamic religion/ ukristu, uislamu, na Judaism) kuhusu sababu kwanini binadamu tumeumbwa duniani

Mafundisho ya Dini hizi yanasema bila aibu kwamba ; 👇👇👇👇

" Mwenyezi Mungu alituumba wanadamu ili tumuabudu"

Nikasema kuwa hoja hii ni ya kitoto sana Kwa sababu kwanza inakwenda kinyume kabisa na sifa za Mungu kama zilivyo andikwa kwenye Biblia, Qur'aan na Talmud.

Kwa mujibu wa mafundisho ya vitabu hivyo ni kwamba Mungu ni Mwanzo na Mwisho. Hana Mwanzo wala mwisho . Wala hafananishwi na kitu chochote Kile.

Amekamilika na anajitosheleza Kwa kila kitu.

So unaposema " Mungu ametuumba ili tumuabudu", tafsiri Yake ni kwamba unasema " Mungu na yeye ni muhitaji. Anahitaji kuabudiwa" Ndio maana wasio muabudu kwa mujibu wa mafundisho hayo watachomwa kwenye moto wa Jehanamu..


Nikawauliza mashekhe na wachungaji.

Okay mnasema Mungu ametuumba ili tumuabudu Je tusipo muabudu atapungukiwa na Nini? Wakajiuma uma wakasema " Hatopungukiwa na kitu"


Nikawauliza Tena " Je tukimuabudu Mungu kitu gani kitaongezeka kwake?

Jibu likawa . Hakuna kitu.

Then nikawauliza kama ndo hivyo Sasa Kwa Nini mnasema Mungu ametuumba ili tumuabudu?

Majibu yao ni vitisho vitisho tu vya kitoto.

Ila sijawalaumu Kwa sababu najua tofauti Kati ya Dini na sayansi katika suala zima la kutafuta majawabu ya maswali ambayo universe inatuuliza ni moja.

Religion is searching for the answers from the conclusion where are science is searching for the answers towards the conclusion.

Kwa mfano swali " Hivi Kwa Nini binadamu tupo duniani?"

Dini tayari imesha conclude kwamba tupo hapa Kwa ajili ya kumuabudu Mungu but science bado inatafuta majibu.

As u can see tayari Dini imekuweka kwenye corner ya " Tumeumbwa ili tumuabudu" So udadisi wako lazima Uwe revolved around " Tumeumbwa ili tumuabudu"

Uanze kutafuta dalili kwenye nature ambazo Zina suggest kwamba Mungu ametuumba ili tumuabudu. ( The nature does not suggest this )

Ukiniuliza nina fikiri ni Kwa Nini sisi tupo hapa duniani, jibu ambalo ni sahihi kuliko yote ni hili hapa chini👇👇👇👇👇

Anaejua sababu halisi Kwa Nini sisi wanadamu tupo hapa duniani ni yule aliye tuumba na kutuleta hapa duniani.


Hilo hapo juu ndio jibu sahihi kuliko yote juu ya swali kwanini binadamu tupo duniani.

However pamoja na usahihi wa jibu hilo hapo juu still bado sisi kama wanadamu tunalo jukumu la kutumia akili ambazo ametupa Mungu ili tujue ni sababu Gani hiyo ambayo imemfanya Mwenyezi Mungu atuumbe na kutuleta duniani...

As a matter of fact , dalili kwenye nature Zina suggest kwamba, aliye tuumba na kutuweka duniani amejificha na bado haja communicate chochote na sisi viumbe wake kujidhihirisha kwetu ila anataka sisi wenyewe tutumie akili ambazo ametupa kumjua yeye ni nani,kwanini ametuumba, jina lake halisi anaitwa nani( So far mpaka Sasa hakuna mwanadamu ambae analijua jina halisi la.Mwenyezi Mungu) etc.

Na hiki ndicho ninacho kifanya. So far tayari nimesha suggest nadharia kama 4 kwanini ninadhani sisi tumeletwa hapa duniani na Leo nina kuja na nadharia namba Tano ...
Kuabudiwa ilikuwa sio kusudi kuu la Mungu,Soma kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza yote upate kusudi kuu la uhumbaji wa mwanadamu (
Mwanzo 1:28
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. )hii la kiutawala zaidi hayo mambo ya kuabudiwa ni kueshimu kile Mungu alichokupa.

Stay tuned. Inakuja very soonk
 
Kama kila kila kitu kilichopo lazima kiwe na muumbaji wake wa kwanza, Hata muumbaji wa kila kitu lazima awe na muumbaji wake mwingine wa kwanza.

Huwezi kumu exclude huyo muumbaji kwenye uumbaji, Halafu uanze kufosi kwamba binadamu waliumbwa.
Muumbaji ni spirit/energy can not be created nor destroyed ila binadamu ni kiumbe lazima kizaliwe na mtu
 
Mtoa maada unatuambiaje sasa lengo letu la kuwa hapa duniani ni lipi, na unataka tuishije kama hatutokuwa na muongozo. hv kuna taifa lisilo na katiba
 
Muumbaji ni spirit/energy can not be created nor destroyed ila binadamu ni kiumbe lazima kizaliwe na mtu
Hata binadamu ni Energy.

Spirit is not an energy.

Spirit is a religious illusion.
 
Huoni kwamba walioandika Biblia waliandika mawazo Yao tu na Sio ufunuo kutoka Kwa MUNGU?
Inaweza kuwa sahihi na kama ikawa kweli ni hivyo basi hata hiyo reference ya andiko la kwanini tuliumbwa ni batili lakini pia italeta ukakasi kwenye mambo mengi ambayo tutakua tukiyasema hapa kwa maana kiini cha mambo haya ya kimungu huwa kinaanzia kwenye hayo maandiko kwa maana ya bible.

Unaweza ukasema hapana kwa maana ya nje ila kwa maana ya ndani huwezi kujenga hoja pasipo kuzipeleka fikra zako kwenye upande huo wa maandiko ingawa utajitajidi utoke ili uwe tofauti nayo ila lengo likiwa ni lile lile kukosoa kilichomo humo ndani.
Bado Hujajibu Maswali ya Mtoa Mada natamani Mtu aguse Mtoa mada anachomaanisha ili.Mjadala uwe mtamu
Nimemjibu moja kwa moja ya kwamba hapaswi kuwaza juu ya jambo hilo kwa maana mlengo wake mkuu ni kwanini tuliumbwa nami nikamwambia lengo la awali la uumbaji lilishapotea na badala yake watu tunaishi kwa kufuata taratibu zetu wenyewe pasipo kufuata malengo yoyote yanayotokea kwenye ulimwengu wa juu.

Kwahiyo hakuna lengo lolote lililopo zaidi ya kuzaliana na kuongezeka tu.
 
Hata binadamu ni Energy.

Spirit is not an energy.

Spirit is a religious illusion.
Enegy inazaliwa na binadamu??
Hata binadamu ni Energy.

Binadamu ni Energy inayozalisha energy nyingine.

Sasa huelewi nini?

Hata binadamu ni Energy.

Binadamu ni Energy inayozalisha energy nyingine.

Sasa huelewi nini?
duh: kwamba huu mwili unaooza ni energy na inapata mimba inaenda hospitali kuzalishwa ili izae enegry nyingine .nadhani hujajua nini maana ya energy
 
Nafikiri tuwe tunaweka ungalifu yani, mada hii tunajadili kwa rejea gani? Kama ni Sayansi twende kisayansi , kifalisafa iwe kifalisafa au kwa msingi wa imani..... maana kama hatuweki rejea nini? Hatuwezi kupata hitimisho, maana mwingine anasema mtu akuumbwa hiyo ni theory na mtu kuumbwa ni theory
 
Enegy inazaliwa na binadamu??



duh: kwamba huu mwili unaooza ni energy na inapata mimba inaenda hospitali kuzalishwa ili izae enegry nyingine .nadhani hujajua nini maana ya energy
What is energy?
 
Back
Top Bottom