Nadharia yangu namba 5 kwanini binadamu tumeumbwa duniani

Kwakua umeswma huiamin biblia basi hatuwez kukujibu tena ila kwa ufupi mungu ana jina na anataka tumwabudu na tunavyomwabudu tunampa sifa kwa wale wanaomzuhakimfano mzur ni kisa cha ayubu , uvumilivu na ustahimilivu ulimletea sifa mungu kwamba kuna binadamu wanao weza kumtegea hata wapatwe na nini
 
"still bado sisi kama wanadamu tunalo jukumu la kutumia akili ambazo ametupa Mungu ili tujue ni sababu Gani hiyo ambayo imemfanya Mwenyezi Mungu atuumbe na kutuleta duniani..."
NB:UKIACHA WENGE,SIYO MUDA UTAWAELEWA VIONGOZI WA DINI WALICHOKUJIBU. AKILI NYINGI,HUONDOA.....?
 
Hakuna anae lijua jina la Mungu. Sidhani hata kama Malaika wanalijua jina lake
 
Hata hujasomeka
 
So unataka kusema Mungu hajui matokeo yetu kwenye mtihani wake? Kwa maana ya kwamba hajui kama tutafaulu ama tutafeli?
 
Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kwamba tuliumbwa, wakati bado hauna uthibitisho huo?

Hivi wewe mwenyewe uliumbwa au ulizaliwa na wazazi wako?

Hakuna binadamu aliyeumbwa.

Binadamu hawaumbwi wala hawaletwi duniani.

Binadamu wanazaliwa duniani kupitia wazazi wao.
 
Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kwamba tuliumbwa, wakati bado hauna uthibitisho huo?

Hivi wewe mwenyewe uliumbwa au ulizaliwa na wazazi wako?

Hakuna binadamu aliyeumbwa.

Binadamu hawaumbwi wala hawaletwi duniani.

Binadamu wanazaliwa duniani.
🙏🙏🙏🙏
 
Swali la kwanini Mungu alituumba ni swala la kuamini wala huwezi kutumia theory utafeli Bro, akili za Mungu hazichunguziki:
Kama akili za Mungu hazichunguziki, Wewe ulitumia akili gani kumchunguza huyo Mungu ukajua na kufahamu kwamba hachunguziki?

Ulijuaje kwamba Mungu hachunguziki?

Au uliambiwa na kuaminishwa tu hivyo?

Na wewe unataka kuaminisha watu wengine ulicho aminishwa.
Wewe shika tu:
Mungu alituumba ili tuwe na uhusiano wa karibu naye, kumtukuza, na kutimiza kusudi lake la kipekee kwa maisha yetu, kwa kuishi katika upendo na kutunza uumbaji wake.
Kwa nini unataka watu washike tu, badala ya kujua?
 
"still bado sisi kama wanadamu tunalo jukumu la kutumia akili ambazo ametupa Mungu
Una uthibitisho upi kwamba akili zetu tumepewa na Mungu?

Au unajaribu kufosi imani na mafundisho yako ya kidini tu?
ili tujue ni sababu Gani hiyo ambayo imemfanya Mwenyezi Mungu atuumbe na kutuleta duniani..."
Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.

Mungu hayupo.

Huyo Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu.

Binadamu hawaumbwi na wala hatukuumbwa.

Binadamu Tunazaliana sisi kwa sisi.

Binadamu wanazaliwa.
NB:UKIACHA WENGE,SIYO MUDA UTAWAELEWA VIONGOZI WA DINI WALICHOKUJIBU. AKILI NYINGI,HUONDOA.....?
 
Una amini kwamba Mungu anajua mambo yote kuhusu kila kitu yaliyopita yaliyopo na yajayo?
 
Binadamu tulitoka Wapi kama hatujaumbwa?
 
Duuh dhambi ya Eva na Adam bado inatuhusu hadi leo ila dhambi nyingine ni personal hii nayo inafikirisha sana
 
Binadamu wa kwanza mkuu alizaliwa na nani??,
Hakuna binadamu wa kwanza duniani wa watu wote.

Kila binadamu alizaliwa kutoka kwa mama yake, Na process hii ni endless to infinity...

Uwepo wa utofauti wa vinasaba DNA 🧬 unathibitisha kwamba hakuna binadamu wa kwanza kwa watu wote.

Uwepo wa utofauti wa rangi zetu Unathibitisha wazi kwamba hakuna binadamu wa kwanza duniani wa watu wote.

Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weupe, weusi. Kuna wajapan, wachina na wafilipino. Kuna wakorea, kuna waarabu n.k

Utofauti huu wa rangi ni uthibitisho tosha kwamba hakuna binadamu wa kwanza duniani wa watu wote.

Kama kungekuwa na binadamu wa kwanza duniani wa watu wote, Basi binadamu wote duniani tungefanana kwenye kila kitu. Kwanzia rangi zetu, DNA zetu na tabia zetu.

Pia kuna uwepo wa hali kama Albinism pia na magonjwa ya kurithi. Ni uthibitisho tosha kwamba hakuna binadamu wa kwanza.

Kwa sababu kama binadamu wa kwanza angekuwa na hali kama ya ualbino, Basi binadamu wote tungekuwa maalbino leo hii.

Lakini sivyo tuko tofauti na tuna tofautiana kwenye vitu vingi sana.

Hivyo hakuna binadamu wa kwanza duniani.
 
Sasa binadamu ametokeaje duniani, nadhani ndio nadhalia ya mtoa mada ilipokuja ya kuumbwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…