Nadharia yangu namba 5 kwanini binadamu tumeumbwa duniani

Tumetoka Kwenye tumbo za mama zetu kisha tukazaliwa duniani.

Kwani kuna binadamu asiye na mama?

Au kuna binadamu ambaye hakuzaliwa na mama?
Kwanini binadamu yupo duniani?
 
Wazazi wa kwanza walizaliwa na nani
 
Sasa binadamu ametokeaje duniani, nadhani ndio nadhalia ya mtoa mada ilipokuja ya kuumbwa.
Mbona hujiulizi huyo unayedai kaumba binadamu na yeye aliumbwa na nani?

Kwa nini unalazimisha kwamba binadamu wameumbwa, Halafu ukiulizwa huyo aliyeumba binadamu na yeye kaumbwa na nani? Hujui.
 
Labda tujitoe kwanza, tuchunguze kwanini duniani kuna ngiri, kwanini wapo? Nasema tujitoe sababu huwa tunajipa uspecial kuliko viumbe vingine, sasa hivi viumbe visivyo special kutushinda, wengine wanasema havina soul, vipo kwa sababu gani? Tuanze na ngiri. A.K.A Kasongo.
 
Hakuna akili hapa boss. Hapa ni imani. Ujitoe ufahamu uamini. Ukitumia akili kufikiri hii nadharia yako utagundua haina logic yoyote na ndivyo ilivyo kwenye masuala ya imani.
 
Duh Hoja Fikirishi Sana natamani Upate Challenge za Kisomi Tujifunze Zaidi
 
Bado Hujajibu Maswali ya Mtoa Mada natamani Mtu aguse Mtoa mada anachomaanisha ili.Mjadala uwe mtamu
 
Bado Hujajibu Maswali ya Mtoa Mada natamani Mtu aguse Mtoa mada anachomaanisha ili.Mjadala uwe mtamu
Kwanza kwa nini mleta mada kahitimisha moja kwa moja kwamba tuliumbwa duniani pasipo uthibitisho?

Kuna uthibitisho upi unaothibitisha pasi shaka kwamba tuliumbwa duniani?
 
Kwa nini mtu anaamua kuoa na ikitokea ameoa na hapati watoto anamfukuza mke kwa kumtuhumu hazai?

Nini lengo la mtu kupata watoto huku akijua wakifikisha miaka ya utu uzima wataondoka kwake na kuanzisha miji yao?
Kumeanza Kuchangamka Maswali kama Haya ndo tunayahumitaji sasa..

Mimi naomba Nijaribu Kukujibu Hili swali!

Kwanza Kabisa Kuoa na Kutooa Ni Mindset tu hakuna Ulazima wa Kufanya Hivyo na Hata Ukiacha hutaweza Kuathirika Endapo mahitaji ya ndoa unaweza Kuyapata Bila kuoa..

Pili kuhusu Tuhuma za Kuzaa au kuhusu Hamu ya Kuzaa Pia ni Nzuri kwa sababu ili Kuweza Kuongezeka viumbe sifa yake Kuu ni kufanya Reproduction Kiumbe Chochote kisipofanya Production ya Copy yake kiumbe hicho Kipo katika Hatari ya Kupotea "Extinction"..

Ili Binadamu asiweze Kupotea Inabidi Kuzaliana sana na Hiyo ni cycle Vizazi hata Vizazi ili Viumbe visiweze Kupotea..

Kumfukuza Mke kwa Sababu hazai Hiyo Ni Hulka ya Mtu na Haiwezi Kuwa Normalised Kuwa Ni ya Jamii nzima..

Kwa mfano kwa Kuwa Wanaume wa Kibena Hupiga Magoti haimaanishi Kuwa hata Wanaume wa Kanda ya ziwa nao Hupiga magoti wanaposalimiana..

Sijui kama Una swali la ziada
 
Kwanza kwa nini mleta mada kahitimisha moja kwa moja kwamba tuliumbwa duniani pasipo uthibitisho?

Kuna uthibitisho upi unaothibitisha pasi shaka kwamba tuliumbwa duniani?
Kabisa Maswli kama Haya LIKUD Anatakiwa Kujibu πŸ˜€πŸ˜€
Kwa sababu Ukienda kwenye Hunduism na Budhism hukuti kuwa Tuliumbwa Eti adam na Eva πŸ˜€πŸ˜€
 
Umeumbwa ili uijaze dunia, kiumbe wewe umekuja kuijaza, shukuru Mungu uko hai unapumua, unashiba.una hata muda kuandika JF.
Kuna watu hata mnaanza kumuuliza Mungu maswali?
Badala ya kushukuru, unahema, unakula, unalala,
Unaanza kuuliza Mungu yupo.
Mungu yupo mpaka kakuweka we hai hapo ulipo.
 
Swali la nyongeza ndugu mjumbe.
Aliyeweka mbegu kwa mwanamme na yai kwa mwanamke ni nani na alikuwa na lengo gani?

Kwanini aweke kitu cha kutufanya tuzaliane na kuongezeka ili hali alikuwa na uwezo wa kumfanya mmoja au wawili tu na akawa ana-enjoy kuwaona?
Kumfukuza Mke kwa Sababu hazai Hiyo Ni Hulka ya Mtu na Haiwezi Kuwa Normalised Kuwa Ni ya Jamii nzima..
Ni sawa kabisa. Lakini hii kitu wengi huwaathiri sana wanapokaa ndani ya ndoa bila kupata mtoto (watoto). Na hao wanaofanya hivyo (kuwaacha wake/waume zao) ili waone na kuolewa au hata kutafuta mpango wa kando ili waweze kupata watoto, huwa na lengo lipi hasa?
Sijui kama Una swali la ziada
 
Ili tumuabudu na tumpe fungu la kumi. Ni uwongo uliotungwa na wajanja ila binadamu wengi wameamini bila kuhoji. Dini ni vyama vya wahuni wenye akili, kupumbaza tu akili za binadamu. Eti Mungu yupo mbinguni, ni wapi?
 
Kama mwenyez Mungu katupatia akili ya kujua kwanini katuumba,je tutajuaje kuwa majibu ya mwanadamu Gani ni sahihi!!! As long as hatojireveal wazi bas Kila mtu atakua anaguess tu majibu ya kuwa kwanini katuumba.
 
Wazazi wa kwanza walizaliwa na nani
Kama kila kila kitu kilichopo lazima kiwe na muumbaji wake wa kwanza, Hata muumbaji wa kila kitu lazima awe na muumbaji wake mwingine wa kwanza.

Huwezi kumu exclude huyo muumbaji kwenye uumbaji, Halafu uanze kufosi kwamba binadamu waliumbwa.
 
Kwanini Unawaza Kuna Mtu aliweka Mbegu Huwazi kuwa Mwili unatengeneza Mbegu zake mwenyewe katika Balaghe..
Kwa mfano Mtoto Mdogo Hana Uwezo wa Kutengeneza Sperm wala Kutoa Shahawa..

anapata Uwezo huo akiwa Mtu mzima kwenye Process ya Ukuaji Ya Kutengeneza Shawaha inayoitwa Spermatogenesis Ambayo Hutokea Kwa mwanaume akiwa amefikia Baleghe..

Hakuna Mtu ambayr Huja na Kuweka sperm kwenye mwili wa kijana Huyo zaidi ya Mabadiliko ya Mwili..

Japo sikatai kwamba Huenda Kuna Mungu anayesimamia Process zote ila Kuna baadhi ya maswli ya Kisayansi yajibiwe kisayansi na Sio Kiimani


Hili Nimelijibu na Inategemea Ethinicity na Community
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…