Nadiriki kusema nchi za Afrika hususani viongozi wake hawajielewi

Nadiriki kusema nchi za Afrika hususani viongozi wake hawajielewi

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Nchi nyingi duniani zimepitia katika kandamizi za kimabavu za nchi nyenginezo (expansionism)) hii inatokana na kwamba mkataba wa mwanzo wa maisha ulikuwa unategemea sana vita (SURVIVE for war) nguvu zako katika vita zitakuhakikishia kutawaliwa au kutawala (State of Nature).

Nchi kama marekani, na Uchina ambazo ni nchi zenye uchumi mkubwa kwa sasa zimepitia shuruba hiyo lakini,zimefanikiwa kujitafuta na kuweza kusimama kama dola,lakini bado nchi zetu zinaendelea kushika mkia katika Kila nyanja kiasi ambacho nchi hizi hazijitambui kuwa zenyewe zinamamlaka na nguvu kama nchi kutokana na kwamba wanauza dola kwa maslahi na ujinga wa viongozi wetu.

Siwezi kuamini kabisa kuwa nchi ina miaka 50 bado inategemea kwa wamerekani kiasi cha kufika kuzarauliwa kwa kuambiwa ikubali ushoga na mengineyo, principle na kidunia zimeharibu mamlaka za dola hasa neno" Demokrasia" ambalo nchi nyingi kubwa imeianzisha kuendelea kuibaka Afrika kwa mlango wa Nyuma.

Ushauri

Nchi za Afrika zijitafakari na kukubali kuungana kupitia mawazo/nadharia za wapiganaji uhuru Kwame Nkurumah,Mandela na akina nyerere waliona kabisa Afrika itashindwa pakubwa itengenezwe Dola kama ya Marekani,japo viongozi wengi watanunulika lazima tuwe na mfumo mpya wa siasa tukiondoa wa sasa hivi.
 
Yaani watengeneze 'United States of Africa' ?...sio rahisi kabisa, isitoshe itabidi kila nchi isalimishe madaraka yake kwa serikali kuu.

Hata 'United States of America' iliundwa kimabavu tu kwa njia ya umwagaji wa damu.
 
Yaani watengeneze 'United States of Africa' ?...sio rahisi kabisa, isitoshe itabidi kila nchi isalimishe madaraka yake kwa serikali kuu....

Hata 'United States of America' iliundwa kimabavu tu kwa njia ya umwagaji wa damu.
Kaka njia ya kimabavu siku zote ndiyo ni sahihi ebu angalia hilo neno demokrasia linavyoiumiza Afrika!!

Viongozi wa uhuru wengi wenye lengo hilo wameuliwa nchi za ulaya na Marekani wanatuogopa sana ndiyo maana wakaamua kutumia mfumo wa "divide and rule".

Hata mfano uislamu unaouona sasa umekuwa mkubwa sababu ya mabavu/vita.
 
Back
Top Bottom