Naenda Dar kununua pikipiki used mbagala zakhiem nina kesh ya 1.2m

Siku hizi huduma za LATRA kwa pikipiki na Bajaji ni online (kama ilivyo kwa Magari) hupati huduma kama una kadi FEKI maana mfumo umeunganishwa na TRA, Dar ujanja ni mwingi but kila lakheri.
Nielekeze vizuri mkuu kwa vip?
 
Kule kuna rafiki yangu yupo kongoe atanisaidia
Mmoja!?? Serious!?? Aya bhana!
Nilikwenda kununua Luninga tu! Niliongozana na jamaa sita! Tumefika nyumba ya tatu! Anakuja mtu anadai eti Luninga ni yake! Yaani tulipomtazama tu akajua MISSION IMPOSSIBLE 😃 watu wanatapeliwa saa saba mchana huko 😃
 
Una uhakika hyo tvs mkuu....!!?

Bongo used kununua labda gari...
 
Daah hizo comment zimeniacha hoi😀😀
Ila bwana mdogo kuwa makini usije uziwa baiskeli tu unatoka Dar Umenunua Boda inafika kwenu baiskeli
 
Actually humu kuna wajuaji wengi yaani JF imekuwa kama facebook alot of useless scumbags watu hawana ABC au hata hawaelewi muanzisha uzi anataka nn mpaka kuanzisha thread, soo pathetic!!!

Muanzisha uzi kama unazipata pikipiki vizuri ww fika ikague na itest pikipiki ukiipenda lipia.

Kwenye kusafirisha ww utachagua mwenyew kwa lori kwa Basi ni ww tu ukitaka kwa basi ni bora ukaenda kuulizia kwanza sio gari zote wanapaki.

Kabla ya kupakia toa side mirrors na mafuta kwenye tenki. Safari nje!!!! uzuri wa basi bei zao sio kubwa na kufika unafika unawasha chuma safari kuelekea unapoishi🤝

Kuhusu Pikipiki used hakikisha unazijua au unajua changamoto ya pikipiki unayotaka kununua iwe na kadi na uihakiki kwa njia ya mtandao piga menu kwenye hii mitando fanya kama unataka uikatie BIMA uone umiliki kama unafanana na ule wa kwenye KADI.

Kwa TVS kagua CABURATOR utendaji kazi wake,maana huwa zinasumbua ukizingatia hujui mtumiaji alikuwa na uelewa gani katika umiliki wa chombo na utunzaji wake ukoje. Kingine kwa TVS sikiliza mlio wa injini kama inavimilio humo visivyo vya kawaida baada ya kupandisha na kushusha sailensa achana nayo, ukiona muungurumo wa jiko(injini) huuelewi achana na hiyo chuma pia kagua NATI ZA kwenye engine kama zimesagikasagika ujue hiyo imefunguliwa funguliwa sana.

Vingine vinarekebishika ukifika fanya service ya ukweli badilisha break shoe zote,beringi na mwaga OIL weka mpya tumia oil ya TOTAL mwaga hiyo uliyokuta humo hata kama watakwambia wamekuwekea mpya mwaga weka yako,,,Dar wanaoil za kupima zile nzito(bei chee) ambazo sio nzuri kwa pikipiki.

TVS 125 HLX(ROHO YA PAKA)NDO PIKIPIKI YA KUNUNUA USED HIZO NYINGINE BORA UJICHANGE UNUNUE MPYA!!!!

🤝ADIOS AMIGOS🤝
 
Kwamba nikifika kitonga niendeshe? Jamaa vip weww
 
Mkuu shukrani kwa elimu nimekupm
 
Tafadhali usinialikie jeshi la matapeli
Ndo maana sijaweka namba ya simu, zaidi ya kukutajia "kipati". Ambayo ji vituo viwili kutoka hapo mbagala, napo kuna ofisi ya kuuza hizo pikipiki na bajaji mkuu.
Au nakua nimefanya marketing mkuu🤣?
 
Fresh sema sina imani kama wapo OFFICIAL
Ndo maana sijaweka namba ya simu, zaidi ya kukutajia "kipati". Ambayo ji vituo viwili kutoka hapo mbagala, napo kuna ofisi ya kuuza hizo pikipiki na bajaji mkuu.
Au nakua nimefanya marketing mkuu🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…