Naenda Kanisani lakini naenda kwa Shekhe kuloga ili mambo yangu yaende sawa

Naenda Kanisani lakini naenda kwa Shekhe kuloga ili mambo yangu yaende sawa

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Siyo kwa ubaya ndugu zangu, misumari ni mingi sana, ukiweka japo kabiashara kako sehemu ili kakusaidie wewe na familia yako ikianza tu kuchanua kuna viherere wanajifanya kuizima.

Sasa nikasema dawa na mimi ni kutembea, simlogi mtu ila naweka mambo sawa, nailinda biashara yangu. Kwani kuna ubaya ndugu zangu?
 
"Amelaaniwa amtegemeayae mwanadamu"

Haijalishi itachukua miaka mingapi ila unachokifanya Sasa kina implications zake, Utapata matokeo Yako unayoyatafuta.
Kama wewe ungekuwa ni Mungu ndio umekomenti hii hakika ningeogopa kumbe ni binadamu tu kama mimi, Mungu afikirii kama unavyofikiria wewe, acha niendelee kuweka mambo yangu sawa simlogi mtu lakini, naweka mambo sawa binadamu wabaya sana.
 
Yer 17:5 SUV​

BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

SI Mimi ni biblia ndio inasema hivyo.
Biblia ni kinywa Cha Mungu.
Mwenye neno na aseme neno Tena kwa ujasiri.
NENO LA MUNGU NI MOTO ULAO
 
Huyo si Sheikh.

Sheikh hafundishi watu ulozi. Ni mchawi tu aliyevaa kanzu na baraghashia

Yer 17:5 SUV​

BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

SI Mimi ni biblia ndio inasema hivyo.
Biblia ni kinywa Cha Mungu.
Mwenye neno na aseme neno Tena kwa ujasiri.
NENO LA MUNGU NI MOTO ULAO
Sawa, ni kweli kabisa lakini bado nasisitiza naweka mambo yangu sawa binadamu siyo watu.
 
Unachokifanya ni Apostasy and Syncretism na ni kama vile Unamtukanisha Mwenyezi Mungu.

Ushauri kuliko Kuchanganya haya Mawili yaani Imani ya Kiroho (Kidini) na Ushirikina (Shirki) chagua Kimojawapo na bakia nacho hiko hiko kama 'Kibobezio' chako.
 
Unachokifanya ni Apostasy and Syncretism na ni kama vile Unamtukanisha Mwenyezi Mungu.

Ushauri kuliko Kuchanganya haya Mawili yaani Imani ya Kiroho ( Kidini ) na Ushirikina ( Shirki ) chagua Kimojawapo na bakia nacho hiko hiko kama 'Kibobezio' chako.
Sijui nimeleweka simlogi mtu naweka mambo yangu sawa.
 
Back
Top Bottom