Naenda Kanisani lakini naenda kwa Shekhe kuloga ili mambo yangu yaende sawa

Aisee..
 
Chagua upande, hapo ni sawa na kuoga then unajigaragaza matopeni,
Kama unaona Giza ndio linakufaa sawa ikiwa Nuru ndio Bora kwako sawa
 
Hivi imani ya kristo ni ipi?
Imani ya KRISTO ni yale yote aliyoamini KRISTO na aliyoamini kutoka kwa MUNGU ndio aliyoyafundisha.
Hivyo basi "imani ya KRISTO" ni yale yote aliyoyafundisha KRISTO na aliyoyaishi kwa vitendo. Ndiyo maana kwenye kitabu cha Ufunuo 14:12 utaona kuwa Watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na imani ya KRISTO.

Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema, "watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na mafundisho(imani) ya KRISTO.

YESU KRISTO aliwafundisha wanafunzi wake kile alichokiamini yeye. Na alichokiamini ni yale yote aliyoyasikia kwa BABA (MUNGU). Yohana 8:28-29
 
Acha tu nichelewe nibaki kwa Mungu... Mungu hana mashart...nitalala nitaamka kwa amani...nitaomba muda wote ajibu asijibu sawa tu.
Jiandae kufa masikini dear!
Yani uishi kwa shida na uende motoni... Kwa uzinzi na unafki na uongo mfano tu sijamanisha wewe
 
wanaohudumu huko makanisani nao ni binadamu tu kama huyosheikh au mganga yoyote wa kienyeji.
Kwani hao wanaohidumu kuanzia pastor na wengine, nimeandika hao ndo tunaowategea na kuwaabudu?
Asante kwa kuchangia
 
Connection tafadhari.
 
Kama wewe ungekuwa ni Mungu ndio umekomenti hii hakika ningeogopa kumbe ni binadamu tu kama mimi, Mungu afikirii kama unavyofikiria wewe, acha niendelee kuweka mambo yangu sawa simlogi mtu lakini, naweka mambo sawa binadamu wabaya sana.
Kitendo cha kuja tu jukwaani ni kuwa haujiamini pamoja na ushirikina wako. Bahati mbaya unatafuta kuungwa mkono, na inapotokea unapingwa unajisikia vibaya. Kiufupi. Umechemka sana katika hilo.
 

1 Yohana : 5 : 4 - Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
1 Yohana : 5 : 5 - Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Hayo maandiko yana uhusiano na imani ya kristo?
 
Hivyo ni vitu viwili tofauti.
 
INAMAANA MASHEIKH NI WAGANGA.
WALOZI.
WACHAWI????.

Au ndio maana wanapenda ubani Nazi mayai na mafuta tofauti tofauti
 
Ungekuwa mchaga hapo ningekuelewa, lakini kama si mchaga wewe umpe hela yako huyo shehe wakichaga akutengenezee dawa
 
Hakuna Wala kosa Nini umesema hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…