Ukiwa Mkristo kuna namna ya kuilinda biashara yako bila hata kwenda kwa Shekhe au mganga.
Iko hivi :
Mshirikishe BWANA MUNGU kwenye biashara yako kwa kumpa hisa au gawio la asilimia 10% tu kila mwezi kutoka kwenye faida unayopata.
Kwa kufanya hivyo moja kwa moja unakuwa umemfanya BWANA MUNGU kuwa mmiliki halali wa biashara yako hivyo akiwa kama mmiliki atailinda na kuibariki biashara yako.
Namna ya kumlipa BWANA MUNGU ni wewe kutoa "fungu la kumi" kanisani kwako kila mwezi na kwa uaminifu.
Angalizo :
- hakikisha biashara yako ni halali kabisa na haina kona kona.
- hakikisha unaishi kwa kuzishika Amri zote kumi za MUNGU na imani ya KRISTO.
(Mwanzo 14:18-20) (Mwanzo 28:20-22) Malachi 3:10-12
"Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi".