Nafanyiwa figisu na wafanyabiashara wenzangu kwenye biashara yangu

Nafanyiwa figisu na wafanyabiashara wenzangu kwenye biashara yangu

azithromycim

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
288
Reaction score
714
Habari Wana jamiiforum.
Bila kuwachosha naenda kwenye mada moja kwa moja.

Nimejikamua Kama kijana nimeamua kufungua liquor store yangu mkoani Tanga ambayo inafanyakazi masaa 24 kila siku za wiki.
Sasa nauza vinywaji kwa bei ambayo Mimi napata faida
Mfano:-
Highlife -2000
Double kick -2000
Block Gin -2000
Hanson choice ndogo -3500
K vant ndogo -3500
Konyagi ndogo - 3500
K vant kubwa -9000
NK.

Sasa bei hizi zimefanya wafanya biashara wenzangu kuanza kuniundia figisu maana wao walikua wanauza Bei juu wanasema mimi nimewaharibia biashara zao.

Mfano wao huuza hivi
Double kick, Highlife na Black Gin kwa 3500
K vant ndogo, Hanson choice ndogo na konyagi ndogo kwa 5000.

Figisu wanazoniundia wafanya biashara wenzangu ni kama,
1. Kuniletea polisi
2. Imani za kishirikina, nikifungua ofisi nakuta hirizi mlangoni siku nyingine nakuta mayai yamepasuliwa au Nazi na makaratasi yaliyoandikwa Kama kiarabu hivi.
3. Kuniletea maafisa afya na TRA.
4. Kupanga vijana waniibie

Wakuu naombeni ushauri wenu kwa wazoefu wa biashara kipindi na nyakati Kama hizi ni zipi njia sahihi za kupita.
 
Weka bei SAWA na Yao but ongeza ubunifu mwingine wa kuwamiliki wateja.
Mfano kutengeneza group la wateja wako,kuwapelekea mzigo,kuwapa bonus mwisho wa mwezi walionunua zaidi,jitahidi uweke hesabu zako sawa,kuwa na nyaraka zote police,tra wasipate kosa.
Ukishindwa nawe kuwa Mafia.
Kuhusu ushirikina ni imani Yako TU
 
Nyaraka zote ninazo kaka

naunga mkono hoja ushauri mzuri sana
 
Hapo kwenye namba (1), na (3) nakushauri ufuate utaratibu wa nchi kwa kulipa kodi zote za serikali zinazoendana na biashara unayofanya.

Hapo kwenye namba (4) nenda karipoti polisi ili wahusika wachukuliwe hatua.

Hapo kwenye namba (2) ni upuuzi mtupu, na vitisho visivyokuwa na maana yoyote.

Kama uchawi ungekuwa na maana kama unavyohisi, basi mkoa wa Tanga ndio ungeongoza kuwa na matajiri wengi nchini.

Hakuna mtu mwenye haki ya kukulazimisha na kukupangia namna ya kufanya biashara yako.
 
Kwenye Kila maamuzi yanamatokeo yake,
Wewe hukujipanga kwa hilo au uli ignore,

Ulivyoamua tuu kufanya hivyo, uliamua vita pia..,
Kama hukujipanga au kutarajia chochote ni jambo la kushangaza.

Ukibadilisha na Ukaendana nao, Pia kua na matarajio ya kibiashara tofauti na sasa..., specifically mauzo, Jee upo tayari na huo utafauti?

Kama hupo tayari kwa hili, pambana nao kwa hali hio hio, na nina shaka uki switch kurudi wanakotaka, watakua wameshinda na pengine wasiishie hapo..

Kuna mdau hapo kakushauri, Ya kaisari mpe kaisari, namaanisha Zingatia usafi, lipa kodi, lipia michango n.k Baada ya hapo utakua umemuondoa adui mkubwa, hayo ya ndumba Yasikuwazishe, ukiyapa attention tuu, utayaona kweli.
 
Thanks kwa
Hapo kwenye namba (1), na (3) nakushauri ufuate utaratibu wa nchi kwa kulipa kodi zote za serikali zinazoendana na biashara unayofanya.

Hapo kwenye namba (4) nenda karipoti polisi ili wahusika wachukuliwe hatua.

Hapo kwenye namba (2) ni upuuzi mtupu, na vitisho visivyokuwa na maana yoyote.

Kama uchawi ungekuwa na maana kama unavyohisi, basi mkoa wa Tanga ndio ungeongoza kuwa na matajiri wengi nchini.

Hakuna mtu mwenye haki ya kukulazimisha na kukupangia namna ya kufanya biashara yako.
Ushauri wako mkuu
 
Hata Kama Ni kushusha Bei, hiyo zako Ni too much, kesho ukifilisika utakuja kusingizia wachawi wqnakuroga, kumbe unauza afu faida yenyewe haieleweki, hata haiwezi kuendesha ofisi yako. Hizo faida za jero jero unazofukuzia kwa biashara ya vileo kwa rejareja Ni upuuzi mtupu, Bora ingekua baa kubwa.
 
Cha kukushauri,
hizo Bei zako ungeweka kwa baadhi ya wateja wako, Tena wale wa kudumu na unawauzia personaly Kama bonus na sio Bei elekezi.

Kibiashara,
kwa hizo Bei zako ulizoweka hadharani, Wee ndo unawakaanga wenzio kwa TRA na manispaa wakakadiriwe parefu maana watajua hiyo biashara mnapata Sana.
 
Back
Top Bottom