Nafasi hizi za kazi zinaenda kupotea kuelekea mwaka 2030

Nafasi hizi za kazi zinaenda kupotea kuelekea mwaka 2030

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433
Wakuu,

Heri ya Mwaka Mpya 2026! Hii ni thread yangu ya kwanza mwaka huu na hivyo nimeona nianze kwa kuangalizia sekta ya ajira na ukuaji wa teknolojia na kinachoendelea kutokea kuelekea mwaka 2030.

ILANI: Endapo utakuwa na mashaka na nafasi yoyote na ukataka ufafanuzi wa nini hasa kinaenda kutokea eneo husika, tunaweza kuelezana na hata ufanye nini sasa kabla hujafikiwa. Najua kuna watu wako rigid na akili zao zinaweza kukataa uhalisia unaokuja ndani ya miaka 5 ijayo, lakini ukishupaza shingo utajishangaa sana huko mbele.

--------------

Mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR), yakiongozwa na akili mnemba (Artificial Intelligence - AI), roboti, na mifumo ya otomatiki (automation), yanabadilisha soko la ajira kwa kasi kubwa.

Kufikia mwaka 2030, kazi nyingi zinazohusisha urudiaji wa vitendo (repetitive tasks) au uchambuzi wa data za msingi zitachukuliwa na teknolojia.

Hapa nimeweka mchanganuo wa nafasi 30 za kazi ambazo ziko hatarini kupotea au kupungua kwa kiasi kikubwa:

1. Utawala na Kazi za Ofisini​

Hizi ni kazi zinazohusisha usimamizi wa nyaraka na data ambazo sasa zinaweza kufanywa na programu za kompyuta kwa usahihi zaidi.
  • Waingizaji Data (Data Entry Clerks): Mifumo ya AI sasa inaweza kusoma na kuingiza data kutoka kwenye makaratasi kwenda kwenye mifumo kidijitali.
  • Watunza Kumbukumbu/Wahasibu wa Ngazi ya Chini (Bookkeepers): Programu kama QuickBooks, Zoho na Xero zimeanza kufanya kazi hizi moja kwa moja.
  • Makatibu Muhtasi (Legal Secretaries): AI inaweza kuandaa mikataba na nyaraka za kisheria za msingi.
  • Wapokeaji wa Wageni (Receptionists): Vifaa vya kidijitali (kiosks) na roboti vinaanza kuchukua nafasi ya kutoa maelekezo na kusajili wageni na hata kufanya kazi kuwa rahisi zaidi kuliko ukiritimba uliokuwepo.
  • Wafanyakazi wa Posta (Postal Service Clerks): Barua pepe na mifumo ya usafirishaji ya kidijitali inapunguza hitaji la huduma za posta za asili.

2. Huduma kwa Wateja na Biashara​

Mifumo ya mazungumzo ya kiotomatiki (Chatbots) imekuwa na uwezo wa kutoa huduma saa 24.
  • Wahudumu wa Benki (Bank Tellers): ATM za kisasa na benki za mtandaoni zimepunguza hitaji la kwenda kaunta.
  • Watunza Fedha Madukani (Cashiers): Maduka makubwa (Supermarkets) yanahamia kwenye mifumo ya "Self-checkout".
  • Wauzaji kwa Njia ya Simu (Telemarketers): AI sasa inaweza kupiga simu na kuzungumza na wateja kwa sauti ya binadamu. Zaidi, teknonolojia imeboreshwa kwa kiwango inakuwa rahisi kupata kujua mteja na maongezi kuwa personalized hadi akaridhika na alivyohudumiwa
  • Mawakala wa Usafiri (Travel Agents): Tovuti nyingi mfano Booking.com na Expedia zimefanya watu wajihudumie wenyewe. Hata Kampuni za Ndege zimefanya tovuti zake kuwa rahisi na hivyo kuondoa watu wa kati kirahisi sana
  • Mawakala wa Bima (Insurance Underwriters): Kanuni za AI (algorithms) zinaweza kufanya tathmini ya hatari na kutoa bima papo hapo.

3. Uzalishaji na Viwanda​

Roboti zina uwezo wa kufanya kazi nzito na hatarishi kwa saa nyingi bila kuchoka.
  • Wafanyakazi wa Mistari ya Kuunganisha (Assembly Line Workers): Roboti viwandani zinafanya kazi ya kuunganisha magari na vifaa vya kielektroniki. Si viwanda vya magari tu, huu umetumika kama mfano wa tunakoelekea
  • Wafanyakazi wa Maghala (Warehouse Workers): Roboti kama zile za Amazon zinahamisha na kupanga mizigo kwa ufanisi na ufasaha zaidi kuliko binadamu.
  • Wapima Ubora (Quality Controllers): Kamera zenye uwezo wa AI zinaweza kubaini makosa madogo kwenye bidhaa kuliko jicho la binadamu.
  • Waendeshaji Mitambo ya Kuchapisha (Printing Press Operators): Uchapaji wa kidijitali unahitaji watu wachache zaidi. Kwanza ukiongea na kizazi cha sasa watashangaa kama kulikuwa bado kuna kitu kama hiki
  • Wasafishaji wa Viwandani (Industrial Cleaners): Roboti za kusafisha sakafu na maeneo hatari zimeanza kutumika.

4. Usafirishaji na Logistiki​

Maendeleo ya magari yanayojiendesha (Self-driving vehicles) yataleta mabadiliko makubwa.
  • Dereva wa Malori ya Masafa Marefu (Long-haul Truck Drivers): Malori yanayojiendesha tayari yanafanyiwa majaribio makubwa.
  • Madereva wa Teksi na Uber: Magari ya "Robotaxis" yanatarajiwa kuchukua nafasi hii katika miji mikubwa. Udereva wa Teksi au Uber tunakoelekea sio deal. Kama ndo ulikuwa unajipanga, tafakari upya ndugu
  • Wapeleka Vifurushi/Vyakula (Delivery Couriers): Ndege zisizo na rubani (Drones) na roboti ndogo za mitaani zitatumika. Kulikuwa na makosa mengi ya binadamu yanayopelekea ufanisi kwa wafanyabiashara kuwa mbovu na hivyo kupunguza tija kazini
  • Waongoza Ndege wa Kijeshi (Military Pilots): Ndege za kivita zinazojiendesha (UCAVs) zinachukua nafasi ya rubani. Kama ulikuwa unajiandaa kusomea hii, tafakari upya!

5. Sekta ya Habari na Ubunifu wa Msingi​

Hata kazi zinazoonekana kuhitaji akili sasa zinaguswa na AI.
  • Watafsiri wa Lugha (Translators): Programu nyingi mfano Google Translate na DeepL zinatoa tafsiri zenye ubora wa juu papo hapo.
  • Wahariri wa Kusahihisha (Proofreaders): Zana kama Grammarly na ChatGPT zinapunguza hitaji la wahariri wa makosa ya kawaida.
  • Wachambuzi wa Ripoti za Fedha za Msingi: AI inaweza kuchakata maelfu ya ripoti na kutoa ushauri wa uwekezaji.
  • Wapigaji Picha wa Matukio ya Kawaida: Simu janja na mifumo ya AI ya kuhariri picha zinapunguza soko hili.
  • Watayarishaji wa Ripoti za Habari za Michezo/Hali ya Hewa: Programu zinaweza kuandika habari hizi moja kwa moja kutoka kwenye data.

6. Sekta Nyinginezo​

  • Wakulima wa Kupulizia Dawa (Crop Sprayers): Drones zinafanya kazi hii kwa ufanisi zaidi.
  • Wapishi wa Vyakula vya Haraka (Fast Food Cooks): Roboti sasa zinaweza kukaanga viazi na kutengeneza baga. Kwa Afrika hii inaweza kuchelewa isiwe mwaka 2030 lakini iko mbioni.
  • Wasimamizi wa Maegesho (Parking Attendants): Mifumo ya kamera na malipo ya simu imechukua nafasi yao.
  • Wapimaji wa Programu (Manual Software Testers): Mifumo ya "Automated testing" ndiyo inayotumika sasa.
  • Mafundi wa Saa za Mitambo (Watch Repairers): Saa nyingi sasa ni za kidijitali na hazihitaji ufundi wa ndani kama zamani.
Aidha, katika miaka michache iliyopita, tumeona kuwa hata kazi zinazohitaji ujuzi wa juu wa kiakili (white-collar jobs) kama uandishi na utengenezaji wa mifumo ya kompyuta haziko salama tena kutokana na uwezo mkubwa wa Akili Mnemba (Generative AI).

Chini ninaweka mchanganuo wa jinsi nafasi nyingine 4 zitakavyoathiriwa na mapinduzi haya kuelekea 2030:

1. Watengenezaji wa Tovuti (Web Developers)​

Zamani, kutengeneza tovuti ilihitaji mtaalamu anayejua lugha kama HTML, CSS, na JavaScript. Leo, mabadiliko ni makubwa:
  • Mifumo ya No-Code/Low-Code: Platform kama Wix, Framer, na Webflow sasa zinatumia AI kutengeneza tovuti nzima kwa kufuata maelekezo ya sauti au maandishi ya mteja.
  • AI Code Generation: Zana kama V0.dev au Claude zinaweza kuandika "frontend" ya tovuti ndani ya sekunde chache, jambo ambalo lingemchukua binadamu siku kadhaa.
  • Hatari: Mahitaji ya watengenezaji wa tovuti za kawaida (basic websites) yatapungua sana; watakaobaki ni wale wanaoshughulika na mifumo mikubwa na tata sana. Kama ulikuwa unajiandaa kusomea nafasi hii ili upate ajira kwa namna ya kizamani, tafakari mara mbili

2. Waandishi wa Habari (Journalists)​

Sekta ya habari inakabiliwa na changamoto ya kasi na wingi wa taarifa/habari (content volume). Vyuo vyetu hasa Tanzania viko nyuma sana na havitaweza kukimbizana na ukuaji wa teknolojia hivyo utayari wa wanananchi ni muhimu sana kwani tarajieni haya (ndani ya miaka 5 tu):
  • Uandishi wa Kiotomatiki: Mashirika makubwa kama Reuters na Associated Press tayari yanatumia AI kuandika habari za michezo na ripoti za kifedha ambazo zinategemea takwimu.
  • Habari za Papo kwa Papo: AI inaweza kuchambua mamilioni ya "tweets" au machapisho ya mitandaoni na kutengeneza habari (news story) kwa haraka kuliko mwandishi yeyote. Hapa wengi wanaweza kubisha ila nawahakikishia miaka 5 ijayo itawafurahisha!
  • Hatari: Waandishi wa habari za kawaida (reporting) wako hatarini zaidi kuliko waandishi wa uchunguzi (investigative journalists) ambao wanahitaji mahusiano ya kibinadamu na siri/faragha. Mwandishi asiyejiongeza na kubakia kuwa ripota atapoteza thamani ndani ya miaka isiyozidi 3.

3. Wahariri wa Habari (Media Editors)​

Kazi ya uhariri inahusisha kusahihisha makosa, kupunguza maneno, na kuhakikisha mtiririko. Kina Balile na wenzao waliozoea kuonekana kama wao ndo wasimamizi wa Sekta wanaenda kupoteza mazima!

AI imekuwa mahiri sana hapa:
  • Uhariri wa Maandishi: Zana kama ChatGPT na Grammarly sasa zinaweza kuhariri makala kwa kuzingatia "tone" au mtindo maalum (style guide) wa gazeti husika. Hata hivyo, nakiona kifo cha magazeti ndani ya miaka 5 ijayo.
  • Uhariri wa Video na Picha: AI inaweza kukata video (editing), kuondoa kelele kwenye sauti, na hata kuweka maneno ya tafsiri (subtitles) kiotomatiki kwa usahihi wa karibu 100%.
  • Hatari: Nafasi nyingi za wahariri wasaidizi (assistant editors) zitafutika, huku mhariri mkuu mmoja akitumia AI kufanya kazi iliyokuwa ikifanywa na timu ya watu kumi. Kama huamini, tukutane Januari 01, 2028.

4. Wapangaji wa Misimbo (Coders/Programmers)​

Hapa tunazungumzia wale wanaofanya kazi ya kuandika mistari ya kodi (writing boilerplate code) na kutatua makosa madogo (debugging):
  • AI Co-pilots: Zana kama GitHub Copilot na Cursor zinaweza kutabiri na kuandika mistari inayofuata ya kodi. Hii inaongeza ufanisi kiasi kwamba kampuni itahitaji "Coder" mmoja badala ya watano.
  • Uhamishaji wa Lugha (Language Migration): AI inaweza kubadilisha mfumo mzima kutoka lugha moja (mfano Java) kwenda nyingine (mfano Python) kwa muda mfupi sana, kazi ambayo zamani ilichukua miezi.
  • Hatari: "Junior Developers" ndio wako hatarini zaidi kwani kazi zao nyingi za mwanzo sasa zinaweza kufanywa na AI kwa haraka na gharama nafuu.
Naomba kwa leo niishie hapa, tutatafakari pamoja siku nyingine.

Kumbuka:
Usipojipanga, utapangwa!
 
Huko tayari kumefikiwa, system zinasomana.
Fuatilia underground mining operations za kampuni kubwa ni control room Tech ili kupunguza changamoto za UG, fumes, rock collapse na confined space.
Hii AI hii kila mtu atafikiwa kivyake mapema tu
Scada Dcs Hmi zinafanya real time monitoring.
Kila mtu atafikiwa kwa muda wake
 
Hii AI hii kila mtu atafikiwa kivyake mapema tu
Shida ya watanzania ni denial kwa reality iliyo mbele yao.

Na wengi wanadhani AI ni Generative tu.

Siasa zetu nazo zitalazimika kubadilika tokana na ukuaji wa Teknolojia.

Mambo ya kufungia mitandao kwa sasa yanawezekana, mbele watachanganyikiwa kwa wakati wao 😂
 
Vitu viwili;

1. Unadhani serikali zitaruhusu mapinduzi ya haraka namna hiyo kwenye kazi za watu? Watu wataandamana. Lazima sheria zitatungwa.

2. Kwa hapa Tanzania 76% ya ajira ni kwenye informal sector, AI haiwezi kusumbua huku.
 
Bado sekta gani?

Labda useme tusaidiane how to cope? That much tunaweza kuumiza kichwa mtu afanye nini.

Mambo ya kudanyanyana na “BADO” yatawagharimu wengi
Walishawahi kutuambia mwaka 2000 ni mwisho wa dunia,

Kompyuta zote zitazima na yatatokea majanga,

Hakuna lolote lililotokea, binadamu hawezi shindana na Mungu.
 
Huko tayari kumefikiwa, system zinasomana.
Fuatilia underground mining operations za kampuni kubwa ni control room Tech ili kupunguza changamoto za UG, fumes, rock collapse na confined space.
Hii AI hii kila mtu atafikiwa kivyake mapema tu
Bogger zinafukiwa kwenye open hole kila leo na zipo kwenye automation , unajua kwanini..?
 
Bogger zinafukiwa kwenye open hole kila leo na zipo kwenye automation , unajua kwanini..?
Hizo ndio vitu vinaepushwa, kingetokea nini endapo ni mtu anaoperate direct, baada ya mda solution itakuja kama ku monitor displine ya mwamba (rock mechanics) ila Tech inakuja ondoa shaka mtaalam
 
Back
Top Bottom