Nafasi hizi za kazi zinaenda kupotea kuelekea mwaka 2030

Nafasi hizi za kazi zinaenda kupotea kuelekea mwaka 2030

Hizo ndio vitu vinaepushwa, kingetokea nini endapo ni mtu anaoperate direct, baada ya mda solution itakuja kama ku monitor displine ya mwamba (rock mechanics) ila Tech inakuja ondoa shaka mtaalam
Production output ndo itaamua bwashee nimekua kwenye hii industry since 2011 najua ninachokisema
 
Production output ndo itaamua bwashee nimekua kwenye hii industry since 2011 najua ninachokisema
Sawa, Nakubaliana na wewe kuhusu output, but now days ni safety first..mining industry ina fatality issue za kutisha. Your family is waiting for you! Be safe.
 
mining industry ina fatality issue za kutisha. Your family is waiting for you! Be safe.
Sawa bwana safety, ila fatalities nyingi pia husababishwa na malfunction ya mashine husika
 
ila Tech inakuja ondoa shaka mtaalam
Unajua mara ngapi seismic device zimewahi kutoa taarifa zisizo za kweli..? Vipi kwa bongo kuna audit na calibration za hizo device..?
 
Nilikua chuga pale crdb nimeona ATM ya kuweka hela .. Bank tellers watch out
 
Mimi naona umejikita kwenye kututisha bila kutoa suluhisho kipi kifanyike,na ni kazi zipi ambazo hazitaathiriwa pakubwa na AI,

Kwa mtazamo wangu naona Kazi ambazo hazitaathiriwa sana na AI ni zile zinazohitaji ubunifu wa hali ya juu, uhusiano wa kibinadamu wa karibu, au uamuzi wa kimaadili unaotegemea muktadha wa kijamii na kihisia, mfano:-

1. Waalimu na Walezi
- Sababu: Mafunzo ya watoto na vijana yanahitaji uhusiano wa kibinadamu, huruma, na uelewa wa kihisia.

2. Wahudumu wa Afya wa Moja kwa Moja,Sababu: Huduma ya afya inahitaji kugusa, kuangalia, na kuzungumza na wagonjwa kwa karibu.

3. Wataalamu wa Afya ya Akili na Ushauri: Ushauri wa kisaikolojia unahitaji uelewa wa hisia, huruma, na mawasiliano ya ana kwa ana.

4. Wasanii na Wabunifu: Ubunifu wa kipekee, hisia, na utamaduni haviwezi kurudiwa kikamilifu na AI.

5. Viongozi wa Jamii na Wanasiasa wa Ngazi ya zote: Uongozi wa kijamii unahitaji uaminifu, mawasiliano ya moja kwa moja, na uelewa wa muktadha wa jamii.

6. Wafanyakazi wa Huduma za Dharura: Maamuzi ya haraka katika mazingira ya hatari hayawezi kuachwa kwa mashine pekee.

7. Wataalamu wa Sheria na Majaji, Uamuzi wa kisheria unahitaji tafsiri ya sheria kulingana na muktadha na maadili ya jamii.
 
Back
Top Bottom