Nafasi ya China katika ajenda ya ujenzi wa viwanda barani Afrika

Nafasi ya China katika ajenda ya ujenzi wa viwanda barani Afrika

Risen man

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
20,205
Reaction score
54,699
Na Eric Biegon – Nairobi

Ukuaji wa kasi wa uchumi wa China umekuwa tukio kuu katika karne ya 21. Historia ya taifa hilo unaashiria kuwa nguzo kuu ya mafanikio haya ni maendeleo ya viwanda vyake.

Uwekezaji huu katika eneo la viwanda ulichangia kuongezeka maradufu kwa pato la taifa la China kwa miaka kadhaa ambayo ulisaidia kukwamua zaidi ya watu milioni 800 kutoka minyororo ya umaskini.

Kwa upande mwingine, uchumi katika nchi nyingi za Afrika zimezorota. Hii ni licha ya kuwa na rasilimali nyingi, nguvu kazi ya mapato ya kadri na soko tayari.

Itakumbukwa kuwa China na Afrika zinafurahia mahusiano mema ya kidiplomasia na biashara yaliyodumu miongo kadhaa. Na hii ndiyo sababu taifa hilo la Asia Mashariki inaamini kwamba ili Afrika iweze kuafikia uhuru wa kiuchumi, haina budi ila kufuata nyayo zake, hasa katika maendeleo ya viwanda.

Na hii inaonekana sio gumzo tu kwani taifa hilo lenye uchumi mkubwa wa pili duniani iko tayari kushiriki katika maendeleo hayo barani Afrika.

Kama sehemu ya mipango minane mikubwa ya jukwaa la ushirikiano wa Afrika na China, maarufu FOCAC, Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian alifichua kuwa Beijing iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Afrika katika kutekeleza upanuzi wa viwanda.

Katika ujumbe wake wakati wa sherehe zinazoendelea kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mpango huo wa FOCAC, Balozi Zhou alisifia matamanio ya pamoja ya bara hilo kuharakisha viwanda na kuharakisha mabadiliko ya kiuchumi.

Pia alipongeza alichokitaja kuwa dhamira thabiti ya Afrika kwa ajili ya ajenda hii na kubainisha kuwa China ni mshirika wa kweli wa bara hilo hasa katika harakati zake za kutafuta kujiendeleza kiviwanda.

"Tunahimiza taasisi za kifedha kuongeza msaada kwa ajili ya ushirikiano wa viwanda wa China na Afrika." Alisema
Kwa mujibu wa Zhou, China inatazamia kuongeza msaada katika maendeleo ya viwanda pamoja na maeneo maalum za kiuchumi na viwanda barani Afrika.

Ili kufanikisha ndoto hii, alifichua kuwa taifa hilo linaloongozwa na Chama cha Kikomunisti haiko tu tayari kutoa fedha zaidi kwenye mradi huu ila pia itashiriki uzoefu wake kuhusu viwanda na Afrika.

"Tangu kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19, China na Afrika zimeshirikiana katika usambazaji wa barakoa, vifaa vya matibabu na dawa, na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa matibabu.

Tutaendelea kutekeleza sehemu yetu katika mpango wa maendeleo ya viwanda kwa Afrika kama ilivyoangaziwa na mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 25 Julai 2016." Zhou alisema kupitia kiungo cha video kutoka ubalozini jijini Nairobi.

Kwa hakika, mjumbe huyo wa China hayuko peke yake katika maono hayo kwani wataalamu wa uchumi kwa mara nyingi wamezungumzia uwezo mkubwa wa Afrika katika viwanda. Mahitaji makubwa ya bidhaa ambazo kimsingi zinapatikana kutoka mataifa ya nchi imekuwa suala la kawaida katika bara hilo.

Lakini, pamoja na kujaliwa na rasilimali nyingi, Zhou anaamini uhamisho wa China wa uwezo wake wa kiviwanda, vifaa na teknolojia utaleta mabadiliko makubwa barani humo.

Anasema viwanda vya Afrika vinahitaji uwekezaji mkubwa kutoka ndani na nje. Lakini kama mshirika mkuu, anaahidi kuwa China itatoa fursa na rasilimali za kuendesha ajenda hii.

"Viwanda vya Kichina sasa vinatekeleza ajenda muhimu ya usambazaji bidhaa na kupanua viwanda duniani. China ina idadi ya watu bilioni 1.4 na kikundi kilicho na kipato cha kati kimefikia milioni 400.

Mahitaji ya soko kubwa la ndani nchini China yataendelea kutoa uwezo usio na mwisho kwa ulimwengu mzima. Nchi za Afrika zitafaidika sana kutokana na maendeleo mapya ya China." Mwanadiplomasia huyo alitamka.

Tamko hili linajiri wakati ambapo China imewekeza zaidi katika viwanda vya viatu na nguo nchini Ethiopia na Rwanda miongoni mwa mataifa mengine. Na mataifa haya tayari yameshuhudia mafanikio makubwa.

Kuna uwezekano kwamba, kuanzisha mchakato huu China itaangazia macho yake kwenye sekta ya viwanda vidogo vidogo, ambavyo vinajumuisha shughuli nyingi.

Tayari, China, sawia na Umoja wa Afrika, imeanzisha mipango muhimu ya kimkakati ya maendeleo, kama vile ushirikiano mpya wa maendeleo ya Afrika, Mpango wa utekelezaji wa maendeleo ya viwanda ulioharakishwa wa Afrika, mpango wa maendeleo ya miundombinu barani Afrika na Ajenda 2063, kwa matumaini kwamba karne ya 21 itakuwa ya mafanikio makubwa barani Afrika.
 
Afrika inanufaika na China kuliko inavyonufaika na mataifa ya magharibi mkuu
Labda tunanufaika kwa kuletewa mchele wa plastiki na sato feki😀😀😀😀 huwezi kufanya biashara au kazi na China utegemee kufaidika. Mataifa ya Magharibi wanatunyonya lakini siyo Kama mchina ingawa Mchina Ni mjanja Sana kumgundua
 
Ni utumwa mamboleo kama ule wa mabeberu (shanga kwa almasi)

Tujikumbushe "kwanini korea kusini na China hawaivi? Kwanini Korea kaskazini swahiba wa uchina ina maendeleo ya silaha badala ya maendeleo endelevu?
 
Labda tunanufaika kwa kuletewa mchele wa plastiki na sato feki😀😀😀😀 huwezi kufanya biashara au kazi na China utegemee kufaidika. Mataifa ya Magharibi wanatunyonya lakini siyo Kama mchina ingawa Mchina Ni mjanja Sana kumgundua
Mchina ni rafiki wa watawala wa kiafrika kwakuwa anawapa 10% kwenye miradi anayopewa tender, na kubwa zaidi ni kitendo cha China kutokuhoji mambo ya ndani ya nchi za Afrika kama, demokrasia na haki za wanadamu. Lakini nchi za Magharibi zina faida maradufu kulinganisha na China.
 
China ni kikwazo kwa mataifa ambayo wanapenda sana kuingilia mambo ya ndani kwa mataifa ya africa,hasa mabeberu.ni dhahiri shairi kina beberu wana hali mbaya.
But hawana cha kumfanya china😂😂😂😂
 
Nini sasa umepost we mkongwe wa JF? China inawapa watawala 10%? Unauhakika na hili? Yaani mradi wa busisi tayari watawala wana bil 60 kibindoni? Upuuzi mtupu😤😤😤
 
Nini sasa umepost we mkongwe wa JF? China inawapa watawala 10%? Unauhakika na hili? Yaani mradi wa busisi tayari watawala wana bil 60 kibindoni? Upuuzi mtupu😤😤😤

Unauliza au unapigia jibu mstari? 10% ni neno linalotumika kuonyesha rushwa, sio lazima iwe exactly figure ya fedha ya mradi husika.
 
Zanzibar wamewapa kibali cha kuanza kuvua samaki, angalia walivyo vuruga west Africa wanjuta kwa maamuzi yao ya ovyo.
 
China ni kikwazo kwa mataifa ambayo wanapenda sana kuingilia mambo ya ndani kwa mataifa ya africa,hasa mabeberu.ni dhahiri shairi kina beberu wana hali mbaya.
But hawana cha kumfanya china😂😂😂😂

Kwa taarifa yako mchina ni beberu masikini, na mingi ya miradi yake ni substandard. Lakini miradi ya nchi za magharibi mingi ina viwango, na hata malipo na stahiki za wafanyakazi ni tofauti kabisa. Ukifanya kazi kwa mzungu utakuwa na mshahara mzuri na mazingira bora ya kazi, kuliko ukifanya kazi kwa mchina.
 
Unauliza au unapigia jibu mstari? 10% ni neno linalotumika kuonyesha rushwa, sio lazima iwe exactly figure ya fedha ya mradi husika.
Acha uongo unaotokana na hisia. Sio kila ukiona mwanamke na mwanaume wanaongozana ujue wametoka kuzini.
 
Acha uongo unaotokana na hisia. Sio kila ukiona mwanamke na mwanaume wanaongozana ujue wametoka kuzini.
Sina chembe ya shaka ya ninachokisema. Ni haki yako kutetea utakacho, lakini huna uwezo wa kubadili ukweli uliopo.
 
Kwa taarifa yako mchina ni beberu masikini, na mingi ya miradi yake ni substandard. Lakini miradi ya nchi za magharibi mingi ina viwango, na hata malipo na stahiki za wafanyakazi ni tofauti kabisa. Ukifanya kazi kwa mzungu utakuwa na mshahara mzuri na mazingira bora ya kazi, kuliko ukifanya kazi kwa mchina.
sawa sipingi,nikuulize kitu kimoja;unafikri ni kwanini USA (ambao ndio taifa tajiri na lenye sauti)wanafanya kila mbinu kumponda mchina??
Kwanini hawalali wanahangaika na uchina kila siku??
^kuanzia sakata la huawei
^suala la covid19
^android
^na mambo mengine kedekede??
Fikiria kwa kina, china anaenda kupindua mabeberu wote soon😁😁😁
 
Blah blah blah... Acha kukariri kishamba,Mchima anafanya biashara za kandarasi na kuuza bidhaa dunia nzima. Kama kupata vitu fake labda kama unalipa bei chee mlizozoea waafrika. Nenda Ulaya na Usa utakuta bidhaa za China zinaongoza kwa soko.
 
sawa sipingi,nikuulize kitu kimoja;unafikri ni kwanini USA (ambao ndio taifa tajiri na lenye sauti)wanafanya kila mbinu kumponda mchina??
Kwanini hawalali wanahangaika na uchina kila siku??
^kuanzia sakata la huawei
^suala la covid19
^android
^na mambo mengine kedekede??
Fikiria kwa kina, china anaenda kupindua mabeberu wote soon😁😁😁

Ni kweli China atawashinda hao wazungu, lakini hilo likifikiwa dunia itakuwa sehemu hatari kabisa kuishi. Wazungu pamoja na ushenzi wao wote, they are even better compared to Chinese.

Nakumbuka wakati Magufuli anaingia madarakani alikuwa anawasifia wachina kuwa ni rafiki zetu wa kweli, akiamini wana msaada wa kweli kuliko wazungu. Na kilichomfanya awakubali wachina ni kwakuwa hawahoji mwenendo wa utawala bora. Alikuwa hajawajua vizuri wachina, ila kwa sasa ndio amewajua vizuri.

China atakukopesha lakini ukishindwa kulipa inakula kwako, mzungu akikupoesha ukishindwa kulipa anaenda taratibu na ww, na ndio maana madeni yetu mengi kama taifa ni ya wazungu kuliko wachina.

Wachina ni matajiri uchwara, wakati wazungu ni matajiri walioshiba na kukinai na wana ustaarabu kwa kiwango cha kuridhisha kulinganisha na hao China.
 
Ni kweli China atawashinda hao wazungu, lakini hilo likifikiwa dunia itakuwa sehemu hatari kabisa kuishi. Wazungu pamoja na ushenzi wao wote, they are even better compared to Chinese.

Nakumbuka wakati Magufuli anaingia madarakani alikuwa anawasifia wachina kuwa ni rafiki zetu wa kweli, akiamini wana msaada wa kweli kuliko wazungu. Na kilichomfanya awakubali wachina ni kwakuwa hawahoji mwenendo wa utawala bora. Alikuwa hajawajua vizuri wachina, ila kwa sasa ndio amewajua vizuri. China atakukopesha lakini ukishindwa kulipa inakula kwako, mzungu akikupoesha ukishindwa kulipa anaenda taratibu na ww, na ndio maana madeni yetu mengi kama taifa ni ya wazungu kuliko wachina. Wachina ni matajiri uchwara, wakati wazungu ni matajiri walioshiba na kukinai na wana ustaarabu kwa kiwango cha kuridhisha kulinganisha na hao China.
Mkuu unaelekea kuupata ukweli,hasa juu ya nani rafiki wa kweli kati ya mabeberu na mchina.unakumbuka juzi juzi tu EU ametufanyia nini kama taifa?

Kulikuwa na sababu gani ya kutudhalilisha mbele ya uso wa kimataifa kama kweli watu hawa ni wastaarabu kweli?

Kumbuka hiyo hela waliyo tuzalilisha nayo sio mkopo ni just donation tu, je ingekuwa tumekopa hali ingekuwaje?

In short mikopo ya mabeberu inamasharti mengi na wanataka uifanyie kazi kama wanavyotaka wao.

Lakni ni mara ngapi china ametufanyia hivi?

Je, china hatoi msaada ??

#jr
 
Ni kweli China atawashinda hao wazungu, lakini hilo likifikiwa dunia itakuwa sehemu hatari kabisa kuishi. Wazungu pamoja na ushenzi wao wote, they are even better compared to Chinese.

Nakumbuka wakati Magufuli anaingia madarakani alikuwa anawasifia wachina kuwa ni rafiki zetu wa kweli, akiamini wana msaada wa kweli kuliko wazungu. Na kilichomfanya awakubali wachina ni kwakuwa hawahoji mwenendo wa utawala bora. Alikuwa hajawajua vizuri wachina, ila kwa sasa ndio amewajua vizuri. China atakukopesha lakini ukishindwa kulipa inakula kwako, mzungu akikupoesha ukishindwa kulipa anaenda taratibu na ww, na ndio maana madeni yetu mengi kama taifa ni ya wazungu kuliko wachina. Wachina ni matajiri uchwara, wakati wazungu ni matajiri walioshiba na kukinai na wana ustaarabu kwa kiwango cha kuridhisha kulinganisha na hao China.
Blah blah blah,jambo usilolijua ni usiku wa kiza,yaani msaada wa China kwa Watanzania utalinganisha na hao Mabeberu? Labda nchi za Nordic na Scandinavia.

Magufuli ameonyesha uwezo wa kujitegemea kwa kubana mafisadi na kukusanya mapato. Ndio maana hata wazungu hawakoromi hovyo. Mikopo inalipwa kwa pesa za ndani avha uzusi.
 
Hahaha tangu Tanzania mnewakaribisha wachina, wamejenga viwanda vingapi?!

Hawa wachina ni waharibifu, na wezi wa rasilimali na kazi yao ni kutafuta masoko ya bidhaa za viwanda vya china.

Marekani ilihamishia viwanda China ili kupata cheap labor na punguzo la kodi, leo wanahangaika na intellectual property rights, wana copy na kuiba idea za wawekezaji wao na kufungua viwanda below standard nchi za afrika na kuuza bidha afrika.

Wachina sio wawekezaji ni uongo tu.
 
Back
Top Bottom