Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 72,020
- 129,293
mkuu unaelekea kuupata ukweli,hasa juu ya nani rafiki wa kweli kati ya mabeberu na mchina.unakumbuka juzi juzi tu EU ametufanyia nini kama taifa??
Kulikuwa na sababu gani ya kutudhalilisha mbele ya uso wa kimataifa kama kweli watu hawa ni wastaarabu kweli??
Kumbuka hiyo hela waliyo tuzalilisha nayo sio mkopo ni just donation tu, je ingekuwa tumekopa hali ingekuwaje??
In short mikopo ya mabeberu inamasharti mengi na wanataka uifanyie kazi kama wanavyotaka wao.
Lakni ni mara ngapi china ametufanyia hivi??
Je china hatoi msaada ??
#jr
Tatizo la wazungu kwa sasa ni demokrasia yetu na utawala bora. Usitake kukwepa hilo ukidhani hatulijui. Kabla ya uchaguzi wa 2015 uliopelekea uchaguzi wa Zanzibar kuporwa kimacho macho, kulikuwa na fedha za MCC toka US za bure kabisa kusambaza umeme nchini. Fedha hizi zilitoka wakati wa Kikwete tulishapokea na kutumia zaidi ya $600m kwenye awamu 2 za mwanzo, na zilibaki $300m kwenye awamu ya mwisho na ya tatu, niko tayari kusahihishwa kwenye figure, lakini baada ya Uchafuzi ule, wazungu walisema hawatoi hela hiyo mpaka mshindi halali atangazwe.
Kwa masikio yetu tulisikia rais akisema hayuko tayari kupokea hizo hela kwa sharti hilo, kwakuwa sisi ni taifa huru hivyo tusiingiliwe mambo yetu. Je taifa huru lisilotaka kuingiliwa mambo yake, ni ili kutoa nafasi ya ccm kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti? Hiyo ilikuwa ni sign namba moja mbaya kwenye utawala huu dhidi ya hao wazungu. Kilichofanywa na serikali yetu dhidi ya pesa ile, ni kiburi cha madaraka kwa maslahi ya ccm na sio heshima ya nchi. Nina mifano lukuki ila tusitoke nje sana ya mjadala.
Tuje kwa hao wachina ambao kwa kutokujua unadhani wao ni bora kwetu kuliko hata hao wazungu. Wakati serikali hii inaingia madarakani wachina walikuwa na miradi miwili mikubwa, mmoja wa $10b mradi wa bandari ya bagamoyo, na reli ya SGR ya $7b mkopo toka Exim bank ya China, kwa masharti kuwa mkandarasi wa ujenzi wa hiyo reli lazima atoke China. Mradi wa bagamoyo ukapigwa chini, na reli akapewa mturuki, japo tunakopa hela tena standard chartered ya China kwa porojo kuwa ni pesa za ndani. Toka hapo mchina akanuna. Nitajie uwekezaji wowote wa China unaozidi $100b ndani ya nchi hii baada ya serikali hii kuwapiga chini kwenye hiyo miradi ili nione ubora wao kwetu. Kama una hoja njoo na mrejesho.
Hitimisho, nenda kaangalie kwenye deni letu la taifa linakofikia 56t, 2/3 ni deni la wazungu, lililobaki ni la ndani na taasisi mbalimbali kama Afdb, wachina kidogo sana. Je ingekuwa wachina wanatudai 30t+ wangetuacha tutambe?