Nafasi ya China katika ajenda ya ujenzi wa viwanda barani Afrika


Tatizo la wazungu kwa sasa ni demokrasia yetu na utawala bora. Usitake kukwepa hilo ukidhani hatulijui. Kabla ya uchaguzi wa 2015 uliopelekea uchaguzi wa Zanzibar kuporwa kimacho macho, kulikuwa na fedha za MCC toka US za bure kabisa kusambaza umeme nchini. Fedha hizi zilitoka wakati wa Kikwete tulishapokea na kutumia zaidi ya $600m kwenye awamu 2 za mwanzo, na zilibaki $300m kwenye awamu ya mwisho na ya tatu, niko tayari kusahihishwa kwenye figure, lakini baada ya Uchafuzi ule, wazungu walisema hawatoi hela hiyo mpaka mshindi halali atangazwe.

Kwa masikio yetu tulisikia rais akisema hayuko tayari kupokea hizo hela kwa sharti hilo, kwakuwa sisi ni taifa huru hivyo tusiingiliwe mambo yetu. Je taifa huru lisilotaka kuingiliwa mambo yake, ni ili kutoa nafasi ya ccm kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti? Hiyo ilikuwa ni sign namba moja mbaya kwenye utawala huu dhidi ya hao wazungu. Kilichofanywa na serikali yetu dhidi ya pesa ile, ni kiburi cha madaraka kwa maslahi ya ccm na sio heshima ya nchi. Nina mifano lukuki ila tusitoke nje sana ya mjadala.

Tuje kwa hao wachina ambao kwa kutokujua unadhani wao ni bora kwetu kuliko hata hao wazungu. Wakati serikali hii inaingia madarakani wachina walikuwa na miradi miwili mikubwa, mmoja wa $10b mradi wa bandari ya bagamoyo, na reli ya SGR ya $7b mkopo toka Exim bank ya China, kwa masharti kuwa mkandarasi wa ujenzi wa hiyo reli lazima atoke China. Mradi wa bagamoyo ukapigwa chini, na reli akapewa mturuki, japo tunakopa hela tena standard chartered ya China kwa porojo kuwa ni pesa za ndani. Toka hapo mchina akanuna. Nitajie uwekezaji wowote wa China unaozidi $100b ndani ya nchi hii baada ya serikali hii kuwapiga chini kwenye hiyo miradi ili nione ubora wao kwetu. Kama una hoja njoo na mrejesho.

Hitimisho, nenda kaangalie kwenye deni letu la taifa linakofikia 56t, 2/3 ni deni la wazungu, lililobaki ni la ndani na taasisi mbalimbali kama Afdb, wachina kidogo sana. Je ingekuwa wachina wanatudai 30t+ wangetuacha tutambe?
 

Tena bidhaa zenyewe wanazouza Afrika zote ni substandard.
 
Ni ujinga mkubwa kwa Afrika kufikiria China italeta mapinduzi ya viwanda Africa.

Mageuzi ya uchumi wa China yalisababishwa na uwekezaji mkubwa wa America na Ulaya nchini China.

Mpaka leo hii, Waziri Mkuu wa China, kila wakati yupo Ulaya kutafuta wawekezaji, halafu viongozi wa Africa kwa ujinga tu, wanaamini Wachina wana uwezo mkubwa wa kuwekeza Africa.

Mpaka sasa, China inavutia uwekezaji wa dola bilioni 80 toka America na Ulaya. Na katika makampuni makubwa kabisa 10 yaliyopo China, ni kampuni moja tu ndiyo ya China. Mengine yote ni ya America na Ulaya.
 
Afrika inanufaika na China kuliko inavyonufaika na mataifa ya magharibi mkuu
Inabidi ujitafakari sana kuona kama unao uelewa wa kutosha.

Hakuna nchi hata moja Duniani ambayo ilikuwa maskini halafu ikaondoka kwenye umaskini kutokana na uwekezaji wa mchina. Mchina ni mnyonyaji mkubwa na mharibifu mkubwa katila uchumi wa Africa.

Leo hii ni kazi sana kupata bidhaa zenye ubora katika soko la Africa kutokana na kujazana bidhaa zenye kiwango hafifu kabisa toka China. Lakini China haipeleki bidhaa hizo duni Ulaya au America. America ya Kusini wana sera thabiti dhidi ya bidhaa duni za China.

Nilinunua boot Chile kwa dola 75 miaka 15 iliyopita, mpaka leo ipo ikiwa nzuri kabisa, na haijapoteza hata marks zake. Lakini nilinunua boot ya China Morogoro kwa sh 110,000. Baada ya mwezi mmoja ilibanduka sole yake na haikufaa chochote. Siyo kitu cha ajabu ukanunua kiatu toka China asubuhi, jioni siku hiyo hiyo kikawa kimebanduka.

Bidhaa zinazotengenezwa China zilizo bora ni zile zinazotengenezwa under license, na utengenezaji wake unasimamiwa na watengenezaji asilia. Nyingine karibia zote, ni takataka.

Kwa nchi kama Tanzania, nchi ambayo taasisi za kudhibiti ubora, nazo ni duni, kuna kila uchafu kutoka China kwenye maduka mbalimbali.
 

Bora umeweza kusema hilo kwa ufasaha. Ili nchi za kiafrika wangalau zipige hatua ya kuridhisha, ni bora zingeshirikiana na nchi za Scandinavia, kwani wale wana technology kubwa, nchi zao ni ndogo na tayari wameridhika na maisha. Pia nchi hizo hazina wale mabepari wenye tamaa kubwa kama walivyo mabepari wa kimarekani, Uingereza, Ufaransa nk.

Shida kubwa ninayoona kwa hizo nchi za Scandinavia dhidi ya hizi nchi hasa zenye mizizi ya kikomunisti ni demokrasia na Utawala bora. Nchi hizo hawana mchezo na utawala bora na demokrasia, jambo ambalo ni gumu kutekelezwa na nchi hasa hii yetu iliyotwaliwa na mfumo wa chama kimoja kwa muda mrefu, na hata sasa iko chini ya chama hicho hicho. Lakini ccm ikitolewa madarakani kwa vyovyote vile, ni vyema tushirikiane na nchi hizo, ili watume wataalamu wao kuanzishwe vyuo vya ufundi, badala ya wanafunzi kwenda sekondari za kukariri, nusu ya sekondari zilizopo ziwe vyuo vya ufundi, wajifunze elimu ya mitambo, ujenzi, kilimo, tehama, nk. Ndani ya miaka 10 tungezungumza mengine.

Nikiangalia zile 2 trilioni zilizonunuliwa ndege, natamani hata yangenunuliwa matractor 1,000 kila kijiji kiwe na tractor 2, na kulima shamba heka moja iwe chini ya 30,000 mambo yangebadilika.
 
Mchina hajawahi kuwa fala. Unampa tender ya barabara anakuachia 10% ila baada ya mwaka au miaka miwili barabara hiyo unakuta imejaa mashimo maana yakupiga na bado unamuita Tena aje kuirekebisha😀😀😀
 
Mchina hajawahi kuwa fala. Unampa tender ya barabara anakuachia 10% ila baada ya mwaka au miaka miwili barabara hiyo unakuta imejaa mashimo maana yakupiga na bado unamuita Tena aje kuirekebisha😀😀😀

Exactly, zunguka nchi nzima, barabara nyingi zilizojengwa na wachina, ndani ya miaka miwili nyingi zina mashimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…